BUNGE LA IRAQ LAUNGA MKONO VITA DHIDI YA UFISADI

BUNGE LA IRAQ LAUNGA MKONO VITA DHIDI YA UFISADI

Like
378
0
Tuesday, 11 August 2015
Global News

BUNGE la Iraq limepiga kura kwa wingi kuunga mkono mapendekezo yaliotolewa na waziri mkuu Haider al Abadi kwa lengo la kukabiliana na ufisadi pamoja na kupunguza matumizi ya fedha serikalini.

Spika wa bunge hilo Salim al Juburi amesema kuwa muswada huo umepitishwa bila upinzani wowote ambao unalenga kupunguzwa kwa baadhi ya nyadhfa serikalini, kumaliza ubaguzi wa kidini pamoja na wa kisisasa.

Hatua hiyo imefikiwa wakati ambapo kumekuwa na maanadamano ya raia kuhusu kukatika mara kwa mara kwa umeme wakati ambapo kuna joto jingi mbali na ufisadi serikalini unaosababishwa na uzembe.

 

Comments are closed.