BUNGE la Ujerumani limeanza kujadili kuhusu maamuzi ya mwisho ya kulipwa kwa deni la Ugiriki wakati ambapo kansela Angela Merkel anakabiliana na changamoto ya upande wa upinzani na wale wa chama chake kujadili juu ya deni la dola bilioni tisini na nne.
Mambo ambayo yalipewa kipaumbele na wabunge wa upinzani ni kuhusiana na deni la ugiriki kulipwa na Ujerumani huku kukiwa na wasiwasi juu ya maamuzi ya shirika la fedha duniani IFM, kutoshiriki katika kulilipa deni hilo.
Waziri wa fedha ,wolfgang Schauble alipendekeza kuwa hakuna uhakika wa kufanikiwa katika mjadala huo bali alisisitiza kuwa Ugiriki imeonesha kuwa na nia ya kutatua tatizo hilo hivyo haitakuwa sawa kutowapa nafasi nyingine ili waweza kurekebisha makosa yao na kuanza upya.