SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda leo amelazimika kuahirisha kikao cha pili cha Mkutano wa bunge leo asubuhi, baada ya Mbunge wa kuteuliwa kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia kuwasilisha hoja ya kujadiliwa kwa dharula tukio lililotokea jana Wilayani Temeke Mkoa wa Dar es salaa, lililopelekea kupigwa na kukamatwa kwa Mwenyekiti wa chama cha Wananchi-CUF, Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na wafuasi wake.
Katika hoja yake ya msingi, Mheshimiwa Mbatia amesema jambo hilo linaondoa amani, Utulivu na kutokuaminiana na kuliomba bunge lisitishe kikao chake na kujadili tukio hilo.
Hata hivyo Spika wa bunge aliomba suala hilo lijadiliwe kesho, kauli ambayo baadhi ya wabunge walipingana nayo na kuzusha tafrani bungeni na hivyo kikao kuahirishwa hadi jioni leo saa kumi na moja.