BUNGE LAAHIRISHWA KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE WA JIMBO LA UKONGA EUGENE MWAIPOPO

BUNGE LAAHIRISHWA KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE WA JIMBO LA UKONGA EUGENE MWAIPOPO

Like
391
0
Tuesday, 02 June 2015
Local News

NAIBU spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa JOB NDUGAI amelazimika kuahirisha shughuli za bunge hadi june 4 mwaka huu kufuatia kifo cha mbunge wa jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa kilichotokea nyumbani kwake Chaduru mjini Dodoma kwa shinikizo la damu.

Naibu spika Ndugai amesema kuwa mwili wa marehemu umepelekwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi ambapo shughuli za kuaga mwili huo itafanyika kesho mjini humo.

Awali kabla ya bunge kupokea taarifa hiyo wizara ya Afya na ustawi wa jamii nchini imewasilisha makadilio ya matumizi yake kwa kipindi cha mwaka 2015 hadi 2016.

Comments are closed.