BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA SHERIA WA TUME YA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI MWAKA 2014

BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA SHERIA WA TUME YA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI MWAKA 2014

Like
302
0
Wednesday, 25 March 2015
Local News

BUNGE limepitisha Muswada wa  sheria wa Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini wa mwaka 2014 wenye lengo la kuleta matokeo chanya ya shughuli za kudhibiti Ukimwi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

 

Awali akiwasilisha rasmi muswada huo leo Bungeni mjini Dodoma Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na Bunge mheshimiwa JENISTA MHAGAMA amesema kuwa muswada huo utaimarisha kwa kiasi kikubwa mikakati ya serikali katika kutatua tatizo la maambukizi ya Ukimwi.

 

Waziri MHAGAMA amesema kuwa katika kuhakikisha mikakati hiyo inafanikiwa serikali kupitia muswada huo inatarajia kuanzisha mfuko maalumu wa kupambana na Ukimwi.

 

Comments are closed.