BUNGE la Jamhuri ya muungano wa Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi wa mwaka 2015 wenye lengo la kuwezesha nchi kunufaika na mapato yanayotokana na mafuta hayo.
Awali akitoa ufafanuzi wa masuala muhimu katika muswada huo, Naibu waziri wa fedha mheshimiwa Mwigulu Nchemba amesema kuwa serikali itahakikisha mapato yote yatokanayo na mafuta yanasaidia katika kuleta maendeleo ya Taifa.