BUNGE LIMEPOKEA NA KUTHIBITISHA UTEUZI WA KASSIMU MAJALIWA KUWA WAZIRI MKUU

BUNGE LIMEPOKEA NA KUTHIBITISHA UTEUZI WA KASSIMU MAJALIWA KUWA WAZIRI MKUU

Like
352
0
Thursday, 19 November 2015
Local News

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepokea na kuthibitisha Uteuzi wa jina la Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya Tano ambaye ni mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Mkoani Lindi kupitia chama cha mapinduzi-CCM.

Akitangaza jina hilo Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai amewaeleza wabunge kuwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa Rais Mamlaka ya kuteua jina la Waziri Mkuu na kuliwasilisha bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na wabunge.

Mheshimiwa Ndugai amesema kuwa barua ya Uteuzi wa Jina hilo imeandikwa kwa mkono na Rais dokta John Pombe Magufuli ikiwa ni uthibitisho kuwa hakuna yeyote aliyekuwa akifahamu jina la Waziri mteule.

Comments are closed.