BURKINA FASO: JESHI LAIPUUZA AU

BURKINA FASO: JESHI LAIPUUZA AU

Like
375
0
Friday, 07 November 2014
Global News

KIONGOZI wa mpito wa Burkina Faso ametupilia mbali muda wa wiki mbili wa kukabidhi madaraka uliotolewa na Umoja wa Afrika wa kukabidhi madaraka kwa Raia.

Luteni Kanali Isaac Zida amesema haogopi vikwazo , na kuwa wanajali zaidi kuhusu uimara wa nchi yao.Zida alifanya mazungumzo na upinzani na asasi za kiraia na kukubaliana kuitisha uchaguzi mwakani.

Jeshi lilishika madaraka baada ya kifo cha Rais Blaise Compaore ambaye alishinikizwa kujiuzulu baada ya kutokea maandamano wiki iliyopita.

 

 

Comments are closed.