BURKINA FASO: KIONGOZI WA MAPINDUZI ATARAJIWA KUKABIDHI MADARAKA LEO

BURKINA FASO: KIONGOZI WA MAPINDUZI ATARAJIWA KUKABIDHI MADARAKA LEO

Like
211
0
Wednesday, 23 September 2015
Global News

KIONGOZI wa mapinduzi ya kijeshi ya wiki iliyopita nchini Burkina Faso Jenerali Gilbert Diendere hii leo anatarajiwa kukabidhi madaraka kwa rais aliyempindua, Michel Kafando baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa viongozi wa kikanda.

Makubaliano yamepatikana kati ya jenerali huyo na jeshi la nchi yake usiku wa leo, hii ikiwa ni kwa mujibu wa wawakilishi wa pande hizo mbili.

Makubaliano hayo yamejengwa juu ya vipengele vitano, ambavyo vinajumuisha kile kinachowataka wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa rais kilichojaribu kufanya mapinduzi – RSP, kurejea katika kambi yao, na kuondoka katika vituo walivyovikamata katika mji mkuu wa nchi, Ouagadougou.

Comments are closed.