JENERALI aliyeongoza mapinduzi ya serikali nchini Burkina Faso wiki iliyopita ametoa mapendekezo yake ya kuendelea kuongoza taifa hilo hadi kukamilika kwa kipindi cha uchaguzi.
Mapendekezo hayo yaliwasilishwa na Jenerali Gilbert Diendere kwa wapatanishi kutoka nchi za Afrika Magharibi akiwemo Rais Macky Sall wa Senegal na Rais wa Benin Yayi Boni, katika mji mkuu wa Ouagadougou.
Mapinduzi hayo ya serikali yaliyotekelezwa na kikosi cha walinzi wa rais yameshutumiwa vikali, huku Burkina Faso ikiondolewa rasmi kutoka Muungano wa nchi za Afrika.