BURKINA FASO KUFANYA UCHAGUZI MKUU NOVEMBER 2015

BURKINA FASO KUFANYA UCHAGUZI MKUU NOVEMBER 2015

Like
340
0
Thursday, 06 November 2014
Global News

VYAMA vya siasa nchini Burkina Faso vimekubaliana kuwa na uchaguzi mkuu mwezi Novemba 2015 ikiwa ni harakati za kurejesha utawala wa kiraia na demokrasia..

Hata hivyo mazungumzo hayo yameisha bila kuwa na ufumbuzi kuhusiana na nani atakayekuwa kiongozi wa mpito hadi kufikia muda wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kufuatia kuangushwa kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo la Afrika Magharibi Blaise Compaore.

Jeshi la nchi hiyo limekuwa likishikilia madaraka tangu aondolewe madarakani kiongozi huyo kutokana na maandamano ya raia.

 

Comments are closed.