MARAIS wawili wa mataifa ya Afrika Magharibi, Macky Sall wa Senegal na Thomas Boni Yayi wa Benin, wanaelekea Burkina Faso kufanya mashauriano na viongozi waliopindua serikali.
Mapinduzi hayo yalitangazwa baada ya walinzi wa rais kuvamia mkutano wa baraza la mawaziri na kuwawekea kizuizi rais Michel Kafando na waziri mkuu wake Isaac Zida.
Rafiki wa karibu wa kiongozi wa zamani Blaise Compaore, Jenerali Gilbert Diendere, alitangazwa kiongozi mpya jana, Alhamisi.