BURKINA FASO: MWILI WA THOMAS SANKARA KUFUKULIWA

BURKINA FASO: MWILI WA THOMAS SANKARA KUFUKULIWA

Like
267
0
Monday, 25 May 2015
Global News

RIPOTI za mahakama nchini Burkina Faso zinasema kuwa mwili ambao unahisiwa kuwa wa raisi wa zamani aliyeuawa Thomas Sankara utafukuliwa hii leo katika jaribio la kutaka kubainisha ikiwa ni wake.

Familia na marafiki wa rais Sankara wamekuwa na shauku iwapo mabaki hayo ni yake.

Sankara ambaye aliuawa wakati wa mapinduzi mwaka 1987, alichukuwa uongozi baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1983 na baadaye alipinduliwa na Blaise Compaore ambaye aliitawala Burkina Faso hadi mwaka uliopita alipolazimishwa kuondoka na maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Ouagadougou.

Comments are closed.