BURKINA FASO: VIONGOZI WA MAPINDUZI WAKATAA KUSALIMU AMRI

BURKINA FASO: VIONGOZI WA MAPINDUZI WAKATAA KUSALIMU AMRI

Like
257
0
Tuesday, 22 September 2015
Global News

VIONGOZI wa mapinduzi nchini Burkina Faso wamekataa kutii matakwa ya kusalimu amri na kutishia kupigana vita endapo watashambuliwa.

Walinzi wa rais walioongoza mapinduzi walikuwa wamepewa hadi saa nne kwa saa za Afrika kuweka chini silaha na wanajeshi ambao walifika katika mji mkuu Ouagadougou.

Hayo yamejiri huku marais wa mataifa ya Afrika Magharibi chini ya muungano wa Ecowas wakikusanyika Abuja, Nigeria kwaajili ya kufahamishwa na Rais wa Senegal Macky Sall kuhusu hatua zilizopigwa katika kutatua mzozo huo.

Comments are closed.