BURKINA FASO: WAZIRI WA MAMBO YA NJE ATAJWA KUWA RAIS WA MPITO

BURKINA FASO: WAZIRI WA MAMBO YA NJE ATAJWA KUWA RAIS WA MPITO

Like
325
0
Monday, 17 November 2014
Global News

ALIYEKUWA Waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso Michel Kafando, ametajwa kuwa rais wa mpito nchini humo.

Jitihada zimekuwa zikiendelea nchini humo kumchagua kiongozi wa mpito kufuatia kuidhinishwa hapo jana na jeshi na viongozi wa mashirika ya kiraia kwa mpango wa mwaka mzima utakaohakikisha kufanyika uchaguzi.

Kafando alikuwa mmoja kati ya watu wanne ambao wangechukua wadhifa huo, wakiwemo waandishi wawili na msomi mmoja.

Michel Kafando, Sasa anatakiwa amchague waziri mkuu ambaye anaweza kuwa raia au afisa wa jeshi kuongoza serikali ya watu 25 ya mpito.

 

Comments are closed.