BURUNDI: ALIEKUWA MWENYEKITI WA CNDD-FDD AMTUHUMU RAIS KUPANGA NJAMA ZA KUMFUNGA JELA

BURUNDI: ALIEKUWA MWENYEKITI WA CNDD-FDD AMTUHUMU RAIS KUPANGA NJAMA ZA KUMFUNGA JELA

Like
257
0
Monday, 09 March 2015
Global News

ALIYEKUWA mwenyekiti wa chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD Hussein Rajabu aliyekuwa ameripotiwa kutoroka jela amemlaumu rais Pierre Nkurunziza kwa kumpangia njama ya kumfunga jela ili kutokomeza demokrasia nchini humo.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji la BBC, Bwana Rajabu amesema kuwa yeye yuko salama na wala hakutoroka jela kama ilivyodhaniwa bali alitoka jela rasmi baada ya kushirikiana na wafuasi wa chama chake.

Rajabu amesema kuwa wazalendo wenzake wa CNDD-FDD ndio walifanikisha kuondoka kwake gerezani kwa ”heshima.

 

Comments are closed.