MKUTANO wa ngazi za juu wa kujadili hali nchini Burundi utaanza leo mjini Brussels, Ubelgiji huku mada kuu ikiwa ni msukosuko wa kisiasa nchini humo na uhusiano wake na Umoja wa Ulaya.
Mkutano huo, ambao utashirikisha viongozi wa ngazi za juu kutoka mataifa ya Afrika Mashariki, unafanyika kutokana na Umoja wa Ulaya kukusudia kuiwekea vikwazo vya kibiashara nchi ya Burundi.
Umoja wa mataifa umesema kwamba kufuatia Burundi kushindwa kuheshimu vipengele muhimu katika mkataba wa ushirikiano umoja huo unatarajia kuanzisha utaratibu wa kufungua kifungu cha 96 cha mkataba wa Cotonou utakaoisaidia Burundi kuchukua hatua za haraka kujiimarisha kidemokrasia