BURUNDI WAPIGA KURA KUMCHAGUA RAIS

BURUNDI WAPIGA KURA KUMCHAGUA RAIS

Like
207
0
Tuesday, 21 July 2015
Global News

BAADA ya ghasia na maandamano ya miezi kadhaa iliyopita hatimaye raia nchini Burundi sasa wamefika katika vituo vya kupiga kura ili kumchagua rais wao atakayewaongoza kwa muhula ujao.

Taarifa zinasema kuwa watu wawili wameuwawa usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu Bujumbura kufuatia vurugu zilizoambatana na gruneti pamoja na milio ya risasi.

Kiongozi wa sasa wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza anawania muhula wa 3 kama rais licha ya madai kuwa anakwenda kinyume na katiba ya nchi hiyo huku viongozi wanne wa upande wa upinzani wameapa kususia uchaguzi huo.

BURUND2

Foleni zimeonekana katika vituo vya kupigia kura

Comments are closed.