BWANA E AGAWA MAFUTA KISARAWE

BWANA E AGAWA MAFUTA KISARAWE

Like
301
0
Friday, 18 September 2015
Entertanment

Wasikilizaji wa 93.7 EFM kisarawe jana walijipatia mafuta ya bure, baada ya bwana E kutoka EFM kupita eneo hilo na kugawa mafuta. Kila mwananchi wa eneo hilo aliye na chombo cha moto kama bajaji, pikipiki alifurahia huduma hiyo ya bure na yenye manufaa.

Mchakato ulikuwa rahisi tu. Wasikilizaji walitakiwa kufika kituo cha mafuta alichopo  bwana E, wakiwa na stika ya EFM, wanasikiliza EFM na bwana E kuwazawadia mafuta ya bureee.

Huu ni mwanzo tu kwa wasikilizaji wa kisarawe. “Siku ya kesho tutashusha burudani ya aina yake kutoka kwa RDJ’s wetu , pia tutacheza mechi na veteran kisarawe na tunaamini tutarudi na ushindi wa kishindo”. Alisema Dennis ssebo mkuu wa idara ya mahusiano na mawasiliano EFM.

Mechi hiyo ya kesho itachezwa na katika uwanja wa Bomani kuanzia saa tisa alasiri na baaada ya hapo muziki mnene ndani ya tausi Bar kisarawe.

IMG-20150918-WA0077

 

madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wakiwa katika foleni wakisubiri kuhudumiwa

IMG-20150918-WA0053

 

madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wakiwa katika foleni wakisubiri kuhudumiwa

IMG-20150918-WA0074

 

madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wakiwa katika foleni wakisubiri kuhudumiwa

IMG-20150918-WA0076

picha ya pamoja ya Bwana E Jimmy Jiam na wadau wa Efm Kisarawe

 

 

IMG-20150918-WA0054

 

Selfie ya Bwana E

Comments are closed.