CAF YAPATA MDHAMINI MPYA

CAF YAPATA MDHAMINI MPYA

Like
461
0
Friday, 22 July 2016
Slider

Shirikisho la Soka barani Africa (CAF) limepata mdhamini mpya baada ya kumalizika kwa mkataba wake na kampuni ya mawasiliano ya Orange.

Orange imekuwa mdhamini mkuu wa mashindano makubwa ya CAF kwa miaka minane tangu 2009.

Kabla ya hapo, kampuni nyingine ya mawasiliano ya MTN ndiyo iliyokuwa mdhamini kwa miaka minne.

Sasa, mdhamini mpya atakuwa kampuni ya mafuta na gesi ya Total kutoka Ufaransa.

Kampuni hiyo itaanza kwa kudhamini michuano ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika mwaka 2017 ambayo itaandaliwa nchini Gabon.

Thamani ya mkataba huo haijafichuliwa.
Total itakuwa mdhamini mkuu wa:

Kombe la Taifa Bingwa Afrika
Ligi ya Klabu Bingwa Afrika
Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN)
Super Cup ya Afrika
Kombe la Mashirikisho
Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa Wanawake
Kombe la Futsal Afrika
Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 23
Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 20
Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 17

Comments are closed.