CANADA: CHAMA CHA UPINZANI CHASHINDA UCHAGUZI MKUU

CANADA: CHAMA CHA UPINZANI CHASHINDA UCHAGUZI MKUU

Like
181
0
Tuesday, 20 October 2015
Global News

CHAMA cha upinzani nchini Canada cha Liberal kimeshinda uchaguzi mkuu na kufikisha kikomo uongozi wa karibu mwongo mmoja wa chama cha Conservative.

Chama hicho kinachoegemea siasa za mrengo wa kati, chini ya uongozi wa Justin Trudeau, kilianza kampeni kikishikilia nafasi ya tatu kwa mujibu wa kura za maoni lakini sasa kimeongoza kwa kura.

Trudeau, mwenye umri wa miaka 43, ambaye ni mtoto wa aliyekuwa waziri mkuu Pierre Trudeau, amesema raia wa Canada walipigia kura mabadiliko halisi ambapo pia Waziri Mkuu Stephen Harper wa chama cha Conservative amekubali kushindwa.

Comments are closed.