Muziki mnene Mkuranga sherehe zilianza na ufunguzi wa mechi ya mpira wa miguu kati kikosi bora kabisa cha E-fm na Mkuranga Veteran ambapo mchezo huo ulimalizika kwa E-fm kuichabanga Mkuranga Veteran bao moja kwa sifuri, huku goli hilo la efm likiwekwa nyavuni na Rdj X five baada ya kupata pasi nzuri kabisa kutoka kwa John Makundi. Baadae moto wa burudani uliwaka pale High Way bar kwa kuwakutanisha wafanyakazi wa efm na mashabiki wake pamoja na wadau wa redio yetu Mkuranga...
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 03/09/2015 BAADA ya kumalizika kwa Tamasha la muziki mnene Mtaa kwa Mtaa awamu ya kwanza, (Muziki mnene bango) ambapo mashabiki na wasikilizaji wengi wa EFM wamejishindia zawadi kabambe, Sasa ni zamu ya wapenzi wa burudani na mambo ya party. Muziki mnene bar kwa bar ni tukio ambalo lina wakutanisha wasikilizaji na mashabiki wa EFM na wakali wa EFM kutoka wilaya za kinondoni, Ilala na Temeke katika mkoa wa Dar er Salaam, na kwa sasa...
Bondia mwenye tambo zaidi duniani Floyd Mayweather amefanikiwa kununua gari la ndoto zake. Gari hilo ambalo limekua likitajwa na bondia huyo toka mwezi June kwa sasa lipo kwenye mikono yake baada ya kukamilisha malipo yote na kuwa mmiliki halali wa gari hilo la kipekee na la thamani zaidi duniani Gari hiyo aina ya Koenigsegg CCXR Trevita linalokwenda 0-60 kwa sekunde 2.9 na kutembea umbali wa miles 250 kwa saa Mwenyewe Floyd amelipa jina la Hyper car huku gharama za manunuzi...
Muigizaji maarufu duniani Terrence Howard amesema amebadilika saana baada ya kutarakiana na aliyekuwa mpenzi wake Michelle Ghent. Terrence ambae kwa sasa anatamba na series ya Empire amesema alipokuwa pamoja na Michelle kwenye mahusiano amejikuta akiingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya ikiwa pamoja na uvutaji wa bangi na cocaine. Terrence amesema kuwa yeye na Michelle wamekuwa wakitumia aina hizo za dawa za kulevya na kutazama sinema za pono. Muigizaji huyu amesema amebadilika baada ya kuachana na mpenzi...
Tukipata picha na mashabiki wa EFM maeneo ya Kibaha kuwashukuru na kuwatunza kuwapa zawadi kwa kutusikiliza ikiwa ni maandalizi ya ujio wa Muziki mnene bar kwa bar. Bango la MUZIKI MNENE lilionekana maeneo ya mjini Kibaha, lilowekwa na mmoja wa mashabiki wa EFM Radio 93.7. Kushoto ni Jimy Jam mfanyakazi wa efm akipozi kwa pamoja na Mmoja kati ya washindi wa kwanza kutoka kulia, bwana Halid, akipewa zawadi yake baada ya kuweka bango la EFM MUZIKI MNENE eneo la Kibaha jana....
Wimbo mpya kutoka kundi la Waswazi waliomshirikisha Rich Mavoko Song Nakosa Imani Producer Abba Process Video directed by Adam Juma...
BAADA ya kumalizika kwa Tamasha la muziki mnene Bar kwa bar awamu ya kwanza, na mashabiki kuomba Burudani hiyo iendelea tena, Uongozi Efm umekubali ombi hilo na sasa Tamasha hilo linarudi tena kwa kishindo likiwa limeboreshwa kwakuongeza wigo wa kuwafikia watu wengi zaidi. Muziki mnene bar kwa bar awamu hii bila kuwasahamu wasikilizaji na mashabiki wa EFM katika wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala kwa umuhimu wake na Wilaya mpya katika mkoa wa Dar es salaam, Muziki mnene sasa utapelekwa...
Will smith amekana uvumi uliosambaa kuwa ametalikiana na mkewe Jada Baada ya taarifa hizo kusambaa kwenye mitandao muigizaji huyu alitumia akaunti ya facebook kufunguka juu ya ukweli wa mambo. Katika post hiyo Will alisema hana muda wa kujibu upuuzi huo kwa sababu akifanya hivyo ataongeza kasi ya uvumi. Lakini mwishoe star huyu aliamua kusema ukweli kuwa hajaachana na mkewe na hana mpango huo na iwapo itatokea wameachana basi yeye mwenyewe atatoa taarifa hiyo kwa...
Mama mzazi wa Samira ambae ni mpenzi wa muimbaji Weasel kutoka Uganda huenda akawa kwenye list ya wazazi wanaojivunia kuwa na watoto wa kike wanaowajali na kuwafanikishia ndoto zao. Hili linakuja mara baada ya mchumba huyo wa mwimbaji Weasel kuwekewa masharti iwapo atahitaji kumuoa mrembo huyo basi moja ya vitu vikubwa atakavyolazimika kuvifanya ni pamoja na kumjengea nyumba mama wa binti huyu. Chanzo cha karibu kimeeleza kuwa Weasel ana mapenzi ya dhati kwa binti huyu ikiwa ni ndoto yake kubwa...
Bendi ya muziki wa afro pop kutokea Kenya hivi karibuni imeingia kwenye Headlines za vyombo vikubwa vya habari ulimwenguni baada ya kutumbuiza katika hafla ya chakula cha usiku katika ikulu ya nchi iliyoandaliwa na rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta akimakrimu rais wa marekani Barack Obama alipotembelea taifa hilo lililobeba histaoria ya maisha ya kiongozi huyu. Katika show hiyo ya Sauti Sol aliyofanyika ikulu Rais Obama pia aliungana na vijana hao kucheza muziki mzuri kutoka kwenye bendi hiyo. ...
Mkali wa r&b kutoka Marekani ambae pia ni muigizaji wa wa movie ya Fast and Furious Tyrese amevifungukia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na watu weupe nchini humo kuwa na ubaguzi wa rangi. Tyres amesema kuwa redio hizo zinapiga nyimbo za R&B/Soul ambazo zimeibwa na watu weupe tu lakini sio watu weusi ambao kimsingi ndio wanafanya vizuri kwenye chart za muziki huo akiwemo yeye mwenyewe ambae albamu yake imeshika namba moja kwenye chart za muziki wa R&B/Soul album. Tyrese...