Local News

MUSWAADA WA SHERIA YA KUUNDWA KWA BARAZA LA VIJANA UMEHITIMISHWA LEO BUNGENI
Local News

MJADALA kuhusu Muswaada wa Sheria ya Kuundwa kwa Baraza la Vijana Tanzania umehitimishwa leo Bungeni Mjini Dodoma, ambapo Waziri na Naibu Waziri wenye dhamana ya Vijana wamepata nafasi ya kupitia hoja mbalimbali zilizotolewa na Wabunge juu ya kuundwa kwa Mabaraza hayo. Akizungumza Bungeni Mjini  Dodoma  Waziri wa Habari,Utamaduni Vijana na Michezo Dokta FENELA MUKANGALA amesema Muswaada huo umekuwa halali baada ya kua umefuata taratibu sahihi tangu hatua ya awali ya kufanyiwa  matayarisho hadi kufikia hatua ya kupelekwa Bungeni. Amebainisha...

Like
310
0
Tuesday, 31 March 2015
CUF YATARAJIA KUMTANGAZA MAHARAGANDE KUGOMBEA NAFASI YA UBUNGE MOROGORO MJINI
Local News

KUELEKEA Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, imeelezwa kuwa Chama  cha Wananchi CUF kinachounda Umoja wa Katiba wa wananchi –UKAWA, kinatarajia kumsimamisha MBARARA MAHARAGANDE kuwa Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Morogoro mjini. Akizungumza na Kituo hiki MAHARAGANDE amesema kuwa anauhakika wa kushinda nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba  mwaka huu kwa kile alichodai kuwa wananchi wa Morogoro wamepania kufanya mabadiliko. Amesema kuwa wananchi wamechoshwa na ahadi zisizotekelezeka huku...

Like
387
0
Tuesday, 31 March 2015
WIZARA YA NISHATI NA MADINI YATANGAZA UGUNDUZI WA GESI ASILIA KWENYE BAHARI KUU YA TANZANIA
Local News

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imetangaza ugunduzi wa Gesi Asilia katika Miamba ya Mchanga kwenye Kisima kinachochimbwa na Statoil cha Mdalasini-1 kwenye Bahari Kuu ya Tanzania. Waziri wa Nishati na Madini, GEORGE SIMBACHAWENE amebainisha hayo kwenye mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dodoma baada ya kuthibitishwa na Makamu wa Rais wa Statoil, NICK MADEN pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania -TPDC. Statoil ni Mkandalasi katika Leseni ya Utafutaji ya Kitalu namba 2 kwa niaba ya TPDC...

Like
331
0
Tuesday, 31 March 2015
MKAPA ATARAJIWA KUHUDHURIA TAMASHA LA PASAKA DAR
Local News

RAIS wa  awamu  ya tatu, Benjamin  Mkapa  anatarajiwa kuwa ni  mmoja  wa  waalikwa  wa Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 mwaka huu kwenye  uwanja  wa  Taifa  jijini Dar es Salaam. Kwa  mujibu  wa  Mwenyekiti  wa  Kamati  ya  maandalizi  ya  tamasha  hilo, Alex  Msama   Mheshimiwa Mkapa  ni kiongozi wa kitaifa ambaye anastahili kuhudhuria tamasha hilo ambalo linatimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake. Msama  amesema  Viongozi wengine waioalikwa, ni Askofu  Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam,...

Like
237
0
Monday, 30 March 2015
SERIKALI YAONYESHA KUSIKITISHWA NA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI
Local News

SERIKALI imeoneshwa kusikitishwa na vitendo vya kikatili vinavyofanywa na baadhi ya watu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi  -ALBINO-vinavyojitokeza mara kwa mara katika maeneo mbalimbali nchini. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu waziri wa mambo ya ndani mheshimiwa PEREIRA SILIMA ambapo amesema kuwa mbali na jitihada nyingi zinazo chukuliwa na serikali amewaasa wananchi kushirikiana vyema ili kukomesha tatizo hilo nchini....

Like
264
0
Monday, 30 March 2015
WAKAZI WA MABONDENI DAR WATAKIWA KUHAMA
Local News

KUFATIA Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam baadhi ya Wananchi wamewataka watu waishio maeneo ya mabondeni, kuhama maeneo hayo ili kunusuru Maisha, Mali  pamoja na kuepusha gharama kwa Serikali pindi maafa yanapotokea. Wakizungumza na EFM kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema Jiji la Dar es salaam, bado lina maeneo mengi yaliyosalama, hivyo wanapaswa kuepuka utamaduni wa kwamba maisha bora yanapatikana katikati ya Mji bila kujali Usalama wa maeneo hayo. Wananchi hao wamesema imekuwa ni Desturi ya Watanzania kulaumu Serikali...

Like
201
0
Monday, 30 March 2015
JAMII YA WAISLAMU YASHAURIWA KUZITUMIA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO
Local News

MHADHIRI  na Mtafiti wa Masuala ya Kiislamu kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar -SUZA Dokta  ISSA HAJI ZIDI amesema, Dini ya Kiislamu haipingani na Uzazi wa Mpango kwani ulikuwepo  tokea wakati wa Mtume MUAHAMAD, hivyo amewashauri Waislamu kuzitumia kwa ajili ya kulinda afya zao. Akizungumza kwenye mjadala kuhusu Uzazi wa mpango katika Uislamu ulioandaliwa na Kitengo  Shirikishi cha Afya ya Uzazi na Mtoto, Dokta ZIDI amesema, lengo la Uzazi wa Mpango ni kulinda Afya ya Mama na Mtoto aliyezaliwa...

Like
357
0
Monday, 30 March 2015
JK AWATAKA WANANCHI KUIPIGIA KURA YA NDIO KATIBA INAYOPENDEKEZWA
Local News

RAIS JAKAYA KIKWETE amewataka Watanzania kuipigia kura ya ndiyo Katiba Inayopendekezwa, kwa kuwa ni bora kuliko inayotumika sasa. Pia amewaonya Viongozi wa Dini wanaohamasisha wafuasi wao kuipigia Kura ya Hapana  Katiba, kwa kufanya hivyo wanaingilia Uhuru binafsi wa mtu kuamua mambo yake. Rais KIKWETE ameeleza hayo katika Mkutano wa Viongozi wa Dini wanaounda Kamati ya Amani kwa Mkoa wa Dar es salaam ambapo mikoa mbalimbali...

Like
215
0
Monday, 30 March 2015
VIONGOZI WA DINI NA VYAMA VYA SIASA WAMETAKIWA KUTOTOA MATAMKO YENYE LENGO LA KUVURUGA AMANI
Local News

TAASISI ya Tanzania Islamic Peace Foundation-TIPF, imewataka Viongozi wa dini na Vyama vya siasa kutotoa matamko yenye lengo la kuvuruga Amani iliyopo nchini. Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Shekhe Sadiki GodiGodi ambapo amesema ni hasara kubwa sana kwa Watanzania watakapo ipoteza amani hiyo. Amesema TIPF, inalaani matukio yote ya kihalifu pamoja na kauli za baadhi ya viongozi wa dini na vyama vya siasa yanayoashiria kulipeleka Taifa...

Like
230
0
Friday, 27 March 2015
UGUMU WA MAISHA WATAJWA KUWA CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA MAADILI
Local News

UGUMU wa maisha nchini umetajwa kuwa ni miongoni mwa  chanzo cha kuporomoka kwa maadili katika jamii. Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wamedai kuwa hali ngumu ya kimaisha inasababisha wazazi kuishi chumba kimoja na watoto hali inayopelekea watoto hao kuiga baadhi ya vitu wanavyoviona kwa wazazi muda ambao wazazi wanadhani watoto hao wamelala. Wameongeza kuwa kumekuwa na matukio mbalimbali ya watoto kubakana wenyewe kwa wenyewe na hata baadhi ya watoto wa kiume kuingiliwa...

Like
537
0
Friday, 27 March 2015
CUF YASHUKIA MFUMO WA BVR
Local News

CHAMA cha wananchi- CUF kimesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kutumika kwa daftari la kudumu la wapiga kura lililoandikishwa mwaka 2010 kutokana na mapungufu yaliyopo katika mfumo mpya wa uandikishaji wa sasa wa BVR. Akizungumza na waandishi wa Habari leo katika ofisi za chama hicho buguruni jijini Dar es salaam, Naibu mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho Abdul Kambaya amesema kuwa hadi sasa serikali haijafikia lengo la uandikishaji walilojiwekea. Amesema kutokana na hali hiyo na msisitizo wa zoezi...

Like
299
0
Thursday, 26 March 2015