JUMUIYA ya Wazazi jimbo la Temeke, wamemkabidhi Mbunge wa Temeke, ABBAS MTEMVU kiasi cha Shilingi 200,000 kwa ajili ya kuchukua Fomu ya kugombea tena nafasi hiyo ya Ubunge. Akimkabidhi fedha hiyo kwa Niaba ya Jumuiya hiyo, Mwenyekiti SUDI MLIRO amesema kuwa hatua hiyo inatokana na ushirikiano unaofanywa na Kiongozi huyo kwa wananchi wake na kusababisha kupatikana kwa maendeleo ya haraka ndani ya jimbo. Katika hatua nyingine Mbunge huyo,amekabidhi Pikipiki 20 kwa kila Kata katika jimbo hilo kwa lengo la kurahisisha...
TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wawekezaji na Marais wa nchi 5 za Ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia Machi 25 hadi 26 mwaka huu. Akitoa taarifa ya mkutano huo Mkuu wa wa Mkoa wa Dar es salaam, SAIDI MECK SADIKI amesema kuwa,Marais hao PAUL KAGAME wa Rwanda, PIERRE NKURUNZINZA wa Burundi, YOWERI MUSEVENI wa Uganda, UHURU KENYATTA wa Kenya na JOSEPH KABILA wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, watahudhuria mkutano huo wakiwa wameambatana na ...
KATIKA kuadhimisha siku ya hali ya hewa duniani, Mamlaka ya hali ya hewa nchini-TMA imeanzisha mfumo ambao utawawezesha marubani wote kupata taarifa mbalimbali za safari za anga kwa njia ya mtandao ambapo kila shirika la ndege limepewa namba ya siri ya kuingia kwenye mfumo huo. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Meneja Masoko na Mahusiano kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa HELLEN MSEMO amesema kuwa kwa kufanya hivyo mamlaka imeweza kutekeleza mpango ujulikanao kama Quality Management...
SERIKALI kupitia Wizara ya Fedha imewasilisha Muswada wa sheria ya mfumo wa malipo ya Taifa ya mwaka 2015 wenye lengo la kuzuia, kuimarisha na kudhibiti athari zinazoweza kujitokeza katika mfumo wa malipo uliopo. Akiwasilisha rasmi muswada huo leo Bungeni mjini Dodoma waziri wa Fedha mheshimiwa SAADA MKUYA amesema kuwa mfumo huo utasaidia kuiweka nchi katika mazingira ya ushindani wa kibiashara na kutengeneza ufanisi mkubwa wa malipo. Mbali na hayo waziri MKUYA ameeleza kuwa katika kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi kwa...
UKOSEFU wa Damu katika hospital mbalimbali nchini unaweza kusababisha madhara makubwa,ikiwemo vifo vya Kinamama na watoto chini ya umri wa miaka mitano. Hayo yamesema na Shirika lisilo la kiresikali linalojishughulisha na masuala ya Afya la SIKIKA katika mkutano na waandishi wa habari kuelezea madhara yanayoweza kutokea kutokana na upungufu wa damu. Mkurugenzi wa SIKIKA IRENE KIWIA,amesema kuwa upungufu wa damu uliotangazwa na Mpango wa taifa wa damu salamu-NBTS,unapaswa kushughulikiwa ipavyo ili kuokoa maisha ya wagonjwa wengi hasa kinamama...
WAJUMBE wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali,wamemchagua Mbunge wa Viti Maalum,AMINA MWIDAU kupitia CUF,kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo. Katika Uchaguzi uliofanyika mjini Dodoma,Mheshimiwa MWIDAU amechaguliwa na Wajumbe wa PAC kwa kupata kura 15 dhidi ya mpinzani wake ,LUCY OWENYA kupitia CHADEMA aliyeambulia kura mbili. Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo,MWIDAU amesema atafanya kazi iliyoachwa na KABWE ZITTO wakati akiiongoza Kamati hiyo kwa kuzingatia maslahi ya nchi na siyo watu binafsi....
SERIKALI imesema imepata hasara zaidi ya Shilingi Bilioni Nane kutokana na risiti za ununuzi Bandia. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha ,Mheshimiwa SAADA MKUYA alipozungumza katika Majumuiyo ya Semina kwa Wabunge kuhusu Mfumo wa malipo nchini. MKUYA ameeleza kuwa kutokana na mfumo wa kutumia malipo hayo mtu huwasilisha risiti za orodha ya malipo mengi ambayo kwa uhalisia...
CHAMA cha Alliance for Democratic Change-ADC kimeanza kukusanya maoni ya katiba pendekezwa kwa wanachama wake kote nchini ili kutoa maamuzi ya chama kwa katiba hiyo. Akizungumza na Kituo hiki Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho DOYYO HASSAN amesema kuwa hatua hiyo inafuatia maamuzi ya mkutano mkuu wa Taifa kwa mujibu wa katiba ya chama kuwa kuwepo ushirikishwaji wa wanachama pale kunapokuwa na suala linalogusa maslahi ya Taifa. HASSAN amesema kuwa watakwenda kukusanya maoni ya wanachama wake kote nchini katika kanda...
SERIKALI imewasilisha Bungeni kwa mara ya pili Muswada wa Sheria ya usimamizi wa maafa ya mwaka 2014 itakayokuwa na malengo ya kuboresha na kuondoa mapungufu katika sheria iliyopo kwa manufaa ya Taifa. Akiwasilisha rasmi Muswada huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu ,Mheshimiwa JENISTER MHAGAMA amesema kuwa, sheria inayopendekezwa katika muswada huo itasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha uratibu na kutatua matatizo ya maafa katika eneo husika. Mheshimiwa MHAGAMA amebainisha kuwa kumekuwepo na mapungufu mengi katika sheria...
IDARA ya Uhamiaji nchini imetoa wito kwa Wamiliki wa Viwanda na Wazalishaji wa bidhaa mbalimbali kutafuta namna nzuri ya kutunza mazingira kwa kuangalia njia mbadala ya kuhifadhi vifaa vilivyokwisha kutumika. Akizungumza na wadau mbalimbali katika Semina ya mazingira Kamishna wa Uhamiaji, Utawala na fedha PANIEL MGONJA amesema lengo la Semina hiyo ni kuonyesha muongozo wa namna nzuri ya kutunza mazingira. MGONJA amesema kuwa wao kama taasisi ya Uhamiaji wameamua kutekeleza sheria ya Mazingira kwa kuhakikisha Majengo na Nyumba za makazi...
AZMA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini ,KABWE ZITTO kupitia CHADEMA,ya kutaka kujiuzulu Ubunge imegonga mwamba baada ya kuelezwa kuwa Spika wa Bunge ,ANNE MAKINDA amemzuia,kufanya hivyo. ZITTO ambaye alikuwa ameshafanya maandalizi ya kuaga Bunge March 19 ndani ya Bunge,amejikuta akigonga mwamba dakika za mwisho baada ya kuingia Bungeni na kuelezwa na mmoja wa Maofisa wa Bunge kuwa, suala lake la kutoa hotuba limeahirishwa na Spika MAKINDA, akitakiwa kwanza kuifanyia marekebisho. Kabla kuingia Bungeni,ZITTO alikuwa akibadilishana mawazo na...