IMEELEZWA kuwa Wanawake waliovijijini wanapambana na mifumo zaidi ya mmoja ikiwemo mfumo Dume, Utandawazi, Wizi pamoja na aina nyingine ya Ukandamizi wa Rangi ya Ngozi na Mwili. Akizungumza na EFM Mtafiti Shirikishi Jamii AGNES LUKANGA amesema kuwa mabadiliko katika mfumo Kandamizi na Unyonyaji yanaletwa na Wanaokandamizwa na kunyonywa hasa walio pembezoni wenyewe....
MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini-TMA imetoa taarifa ya mwelekeo wa Mvua za Masika kwa kipindi cha Mwezi Machi hadi Mwezi Mei mwaka huu ambapo inaonesha kuwa maeneo mengi ya nchi hayatakuwa na kiwango cha mvua cha kuridhisha. Akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dokta AGNES KIJAZI amesema kuwa ingawa hali ya mvua haitarajiwi kuwa ya kuridhisha lakini kuna baadhi ya maeneo yanatarajiwa kupata Mvua za wastani hadi juu ya wastani ikiwemo Kanda ya...
SERIKALI imesema itajitahidi kuhakikisha inalipa deni lote la Mahindi yaliyonunuliwa kutoka kwa Wakulima na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula-NFRA ifikapo March 30 mwaka huu. Akizungumza na Maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara Wilayani Mbozi, Waziri Mkuu Mheshimiwa MIZENGO PINDA amesema Serikali imedhamiria kufuata deni lote. Ameeleza kuwa tayari alishakwenda nchini Poland kwa maelekezo ya Rais KIKWETE na wao wameshakuja kuona hali halisi...
RAIS JAKAYA KIKWETE amesema Serikali itahakikisha inadhibiti Mtandao wa Mauaji ya watu wenye Ulemavu wa ngozi na kuitaka jamii iungane katika vita hiyo kwa kuwa ni vitendo visivyovumilika na vinalifedhehesha Taifa. Rais KIKWETE ameeleza hayo katika hotuba yake kwa Taifa ya Mwisho wa Mwezi ambapo amesisitiza suala la kutokomeza mauaji na ukataji wa viungo vya Albino ni jambo linalowezekana na litategemea watu kuacha imani za Kishirikina. Aidha katika Hotuba yake pia Rais KIKWETE amezungumzia suala la Uandikishaji wapiga kura na...
MTANDAO wa kijinsia Tanzania umefanya Tamasha la kijinsia ngazi ya Wilaya ya Tarime ikiwa na lengo la kutoa Elimu na uelewa kwa jamii juu ya kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia katika mimba za utotoni, ukeketaji vipigo na umiliki wa Rasirimali. Akizungumza na efm mtafiti shirikishi jamii kutoka TGNP AGNES LUKANGA amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa mtandao wa TGNP hapa nchini mnamo mwaka 1993 TGNP imekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki ikiwa ni pamoja na kupinga vitendo vya...
MKUU wa Polisi Wilaya ya Arusha Mrakibu wa Polisi -SP JUMANNE MULIRO amevitaka vikundi vya ulinzi shirikishi pindi wanapokuwa katika kazi za doria kutowabughudhi wananchi badala yake wanatakiwa kufanya kazi zao kwa kufuata sheria. Amesema utendaji bora wa kazi kwa kuzingatia nidhamu na sheria utaongeza imani kwa wananchi hali ambayo itawafanya wajitolee na kuendelea kuvichangia vikundi hivyo hatimaye kuboresha maslahi yao wenyewe na vikundi hivyo kwa ujumla Hayo yamesemwa wakati wa Uzinduzi wa vikundi viwili vya Ulinzi Shirikishi uliofanyika...
WAKATI Tanzania inatarajia kuingia katika zoezi muhimu la Uchaguzi mkuu wa Udiwani, Ubunge na Urais Oktoba mwaka huu, Wito umetolewa kwa waandishi wa habari kutojihusisha na upande wowote wa Vyama vya Kisiasa na badala yake wafuate maadili ya kazi kwa maslahi ya Taifa. Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Chama Cha –ADC SAID MIRAJI wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambapo amesema kuwa Uandishi wa Habari ni Taaluma inayopaswa kutumika bila kuegemea upande wowote. Ameeleza kuwa...
JUKWAA la sera na mtandao wa asasi za kiraia unaoshughulikia maswala ya utawala bora na uwajibikaji, umeandaa mjadala uliojadili na kuangazia namna uchimbaji wa madini unaofanywa na makampuni na kuangalia jinsi wanavyowajibika kwa jamii, kwa wafanyakazi wanao waajiri na jinsi wanavyotunza mazingira ili kuandaa mazingira bora na kuleta maendeleo endelevu. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mratibu wa jukwaa la sera Senkaye Kilonzo amesema kama asasi za kiraia zinazoangalia maswala hayo wameona kuna haja ya kukaa...
MWENYEKITI wa Taasisi ya Wanawake Tanzania-WAMA amekabidhi msaada wa mashine ya kisasa ya upimaji Saratani ya Matiti kwa akinamama katika hospitali kuu ya Jeshi la Ulinzi Tanzania LUGALO ili kuokoa maisha ya wanawake wengi wanaosumbuliwa na Saratani ya matiti nchini. Akizungumza na wadau mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam kwenye makabidhiano ya mashine hiyo Mama SALMA KIKWETE ambaye pia ni mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameeleza kuwa mashine imetolewa na kikundi cha wanawake watanzania waishio Marekani kijulikanacho kama Tano...
KAMPUNI ya simu ya Obi mobiles imedhamiria kusambaza teknolojia kwa watu wengi zaidi nchini Tanzania lengo ikiwa ni kufanya utendaji wenye tija katika vifaa vya simu za mkononi kwa maendeleo ya nchi na kusaidia kukuza uchumi. Hayo yamebainishwa na mwanzilishi ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa zamani wa Apple, John Sculley, ambapo amesema kampuni hiyo inalenga kuongeza mauzo kupitia mpango mkakati unaowalenga vijana na watumiaji wanaokwenda na wakati na matumizi ya simu za mkononi. Kampuni ya Obi mobiles imezindua aina...
JESHI la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamtafuta PETER MROSO mkazi wa Kijiji cha Ubetu Wilayani Rombo kwa tuhuma za kumuua mkewe kisha kuuzika mwili wake na kubakiza kichwa. Tukio hilo limetokea February 25 mwaka huu nyumbani kwa Marehemu maeneo ya Ubetu ambapo mtuhumiwa alimpiga mkewe JENIPHER PETER sehemu za kichwani. Mashuhuda ambao hawakutaka kutaja majina yao wamedai kuwa mara baada ya mume huyo kumpiga mkewe hadi kufa aliuchukua mwili wake na kwenda kuuzika katika boma la ng’ombe huku kichwa chake...