KAMATI ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imeeleza kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maji ya Kibiti na Ikwiriri iliyopo wilayani Rufiji mkoani Pwani kutokana na kuonesha mafanikio makubwa. Hayo yamesemwa na Kiongozi wa Wajumbe wa Kamati hiyo Amina Makilagi, Mbunge, baada ya kukagua miradi hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji Tanzania Bara inayofanywa na baadhi ya wajumbe wa kamati katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara. Mradi wa Kibiti wenye...
WAZIRI wa maji Jumanne Maghembe ametoa siku 90, kwa mkandarasi Megha Engineering Infrastructure Limited anaesambaza bomba la maji mradi wa Mlandizi Kimara kufanikisha mradi huo na kupeleka ripoti ya maradi kwenye Mamlaka ya maji safi na maji taka (Dawasco), kwalengo la kupata tathimini ya mradi. Ametoa agizo hilo jana akiwa mkoani Pwani wakati akikagua miradi minne ya Dawasco, yakusambaza maji Ruvu juu na Ruvu Chini kufikisha Jijini Dar es Salaam. Aidha amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Arcado Mutalemwa kuhakikisha pampu...
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) wamewataka madereva na makondakta wa daladala kuacha tabia ya kupandisha nauli kiholela wakati wa asubuhi na jioni. Akizungumza na kituo hiki Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Michael Kisaka amesema kuwa tabia hiyo imekuwa ikiwasumbua abiria. Amesema Sumatra imekuwa ikifuatilia na kufanikiwa kuikamata daladala inayofanya safari zake Kimara hadi Kariakoo ikiwatoza abiria nauli ya Shilingi 800 badala ya shilingi 500 tofauti na iliyopangwa na mamlaka hiyo....
VIJANA nchini wametakiwa kuachana na tabia ya kukaa vijiweni bila ya kujishughulisha na kazi yoyote, badala yake watumie fursa zilizopo za ujasirimali ili kujiajiri wao wenyewe na kupambana vilivyo na janga la umasikini. Wito huo umetolewa na Ofisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kibaha, Leah Lwanji kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Hajat Halima Kihemba, wakati wa mkutano maalumu wa uchaguzi mkuu wa Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki Kibaha – Chamawapiki. Lwanji amesema kuwa nia na madhumuni...
SERIKALI kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula- NFRA, imeandaa mpango wa utekelezaji wa muda mfupi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula kutoka tani laki moja na sitini elfu hadi kufikia tani laki nne katika kipindi cha mwaka 2016 na 2017. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa huduma za biashara wa NFRA, Mikalu Mapunda wakati akizungumza na Kituo hiki kuhusu hali ya utunzaji wa chakula kanda zote zilizopo nchini. Akizungumzia hali ya chakula cha ziada katika kipindi kilichopita, Mapunda amesema...
KATIBU MKUU wa Chama cha Mapinduzi –CCM, Abdulrahman Kinana, amewahimiza Wazanzibari kuipigia kura ya ndiyo Katiba mpya iliyopendekezwa kwakuwa inatatua kero nyingi za wanzanzibari katika muungano na kuwafanya wawe na uhuru zaidi. Bwana kinana amefafanua umuhimu wa kuipigia kura katiba hiyo pendekezwa huku akitolea mifano ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania iwapo Rais wa Jamhuri atatoka Bara, Zazibar kujiunga na jumuiya za kimataifa bila kikwazo, kuwa na uhuru...
JESHI la Polisi Mkoani Arusha limewakamata watu kadhaa kwa kuhusishwa na tukio la Ujambazi wa kuteka mabasi sita ya abiria yaliyokuwa yanatoka nchini Kenya kuelekea Arusha nchini Tanzania. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, amesema katika Msako huo ulioanza juzi, wamefanikiwa kukamata watu hao katika maeneo mbalimbali mkoani humo. Tukio la kutekwa kwa mabasi hayo lilitokea juzi usiku baada ya watu wanaodhaniwa kuwa majambazi kuvamia na kuteka mabasi hayo katika eneo la Mbuga Nyeupe, Wilaya ya Longido....
WANANCHI wameombwa kusaidiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa haraka pindi wanapoona tukio la uhalifu au kuona umiliki wa silaha kinyume na sheria ili kuweza kulinda amani na ulinzi wa Taifa . Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Temeke SOPHIA MJEMA kwenye sherehe ya utoaji sifa na zawadi kwa Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali. MJEMA amefafanua kuwa ni muhimu wananchi kushirikiana na Polisi ili kuweza kupunguza matukio ya uhalifu na kuongeza...
IDARA ya Ajira Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetoa rai kwa vijana wote nchini waliopo shuleni kujikita zaidi kwenye taaluma ya masomo ya sayansi kwani sekta ya Sayansi ni moja ya Sekta yenye uhitaji mkubwa wa wataalam hao katika Nyanja mbalimbali za utumishi wa umma. Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Msaidizi kutoka Idara ya Ajira katika Utumishi wa Umma MALIMI MUYA alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Bwana MUYA amefafanua kuwa uhaba wa...
WAPIGANAJI wa kundi la kigaidi la Boko Haram wamewateka nyara watu zaidi ya 60 baada ya kufanya shambulio kaskazini mwa nchi jirani ya Cameroon. Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, magaidi hao walifanya shambulio hilo hapo jana, yaani siku moja baada ya Chad kuwapeleka wanajeshi wake nchini Cameroon, ili kupambana na magaidi hao. Afisa mmoja wa polisi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba, wapiganaji wa Boko Haram walivivamia vijiji viwili vya kaskazini mwa Cameroon hapo jana na walizichoma moto...
MAMLAKA ya Utabiri wa Hali ya Hewa Tanzania-TMA, imetoa tahadhari ya kuwepo kwa vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 kati ya Januari 18 na 20 mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari jijini Dar es salaam, maeneo yatakayoathirika na Mvua hiyo ni pamoja na Mikoa ya Ruvuma, Mtwara, Lindi, Morogoro, Pwani, Dar es salaam na Kisiwa cha Unguja. Taarifa hiyo imeeleza kuwa hali hiyo inatokana na kuimarika kwa...