KAMATI Ndogo ya maadili ya Chama cha Mapinduzi – CCM, leo inakutana kwa lengo la kuanza kazi ya kuwachunguza makada wake wakiwemo wajumbe wa NEC na Kamati kuu. Hatua ya kuanza kuchunguza kwa makada wa chama hicho hususani waliotuhumiwa kwenye sakata la Tegeta Escrow, ni utekelezaji wa agizo la Kamati Kuu ya CCM, iliyokutana Visiwani Zanzibar kujadili masuala mbalimbali wiki iliyopita. Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, amesema vikao vya kamati hiyo vitaanza leo na kasha...
MSAJILI wa Vyama Vya Siasa nchini, Jaji FRANCIS MUTUNGI amevitaka vyama vyote vya siasa kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa Sheria , Katiba na Kanuni ili kuepusha migogoro. Aidha msajili huyo amevitaka vyama hivyo view mfano mzuri wa kwa jamii kwa kudumisha Amani na Utulivu ndani ya vyama vya siasa. Kauli hiyo ameitoa leo katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari kufuatia kuwepo kwa wimbi la migogoro ndani ya vyama hivyo....
NAIBU WAZIRI wa Maliasili na Utalii mheshimiwa MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini amewataka vijana kujituma na kutumia fursa mbalimbali ambazo zinatolewa na Serikali. Akizungumza na EFM Mheshimiwa MGIMWA amesema kuwa vijana wengi wamekuwa wakibweteka kwa kutojituma kufanya kazi na kuendelea kuilaumu serikali. Mheshimiwa MGIMWA amewataka vijana wenye fursa ya kurudi au kuingia shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi wengi kutokana na mabadiliko ya Kiuchumi na Sayansi na Teknolojia na ndio sababu...
WAVUVI mkoani Kigoma wametakiwa kuacha tabia ya kuvua Samaki na Dagaa kwa kutumia zana haramu. Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Maendeleo ya Uvuvi na Mifugo Dokta TITUS KAMANI wakati wa ziara yake ya kutembelea Mialo ya kuhifadhia Samaki na Dagaa iliyopo Kibilizi Wilayani Uvinza mkoani Kigoma. Kwa mujibu wa Dr. Kamani, wavuvi wengi wanatabia ya kuvua samaki kwa kutumia taa zenye mwanga mkali nakusababisha samaki wengi kupofuka macho na...
WIZARA ya Maji Mjini Kibaha inatarajia kuanza mradi wa Maji wa Wami-Chalinze awamu ya tatu ifikapo mwezi Machi mwaka huu. Wizara hiyo imesema mradi huo unatarajia kugharimu shilingi Bilioni 60 mpaka utakapokamilika. Meneja wa Mamlaka ya Maji Chalinze (CHALIWASA), Christer Mchomba, amesema awamu hiyo itaongeza mitandao ya maji kwenye vitongoji 210 kutoka kwenye vijiji 47....
SERIKALI imeshauriwa kuandaa Sheria ya Mirathi kwa kuzingatia na kupitia Sheria za Dini, Mila na Desturi za Watanzania badala ya kuendelea kutumia Sheria namba 36 ya mwaka 1963 ya nchini India ambayo haikidhi Mahitaji ya Watanzania. Akizungumza na EFM Wakili wa Kampuni ya Uwakili ya MEGA PAUL KALOMO amesema kuwa Tanzania haina sheria yake ya Mirathi hali inayopelekea kuwepo na mikanganyiko katika suala la mirathi ambapo imekuwepo ya Dini na Mila ambayo inamkandamiza...
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa LAZARO NYALANDU amewakaribisha wafanyabiashara kutoka Saudi Arabia kuwekeza katika sekta ya Utalii nchini ambayo ina fursa nyingi za uwekezaji. Mheshimiwa NYALANDU ametoa wito huo kufuatia mazungumzo yake na Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara ya Saudi Arabia Dokta ABDULRAHMAN AL-ZAMIL yaliyofanyika Riyadh, Saudi...
JUMANNE JULIUS mwenye umri wa miaka 21 na JAFARI DIOMBA mwenye umri wa miaka 20 wakazi wa jijini Dar es salaam wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya kinondoni jana kwakosa la unyanganyi kwa kutumia silaha. Wakisomea shitaka hilo mbele ya hakimu IZ-HAQ KUPPA na mwendesha mashitaka MAGOMA MTANI amesema kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo Novemba 16 mwaka jana maeneo ya mbezi beach wilaya ya kinondoni. Mtani amebainisha kuwa washitakiwa hao kabla...
WAZIRI MKUU Mheshimiwa MIZENGO PINDA anazindua rasmi mkutano wa kibiashara wa Nchi ya Omani wenye lengo la kupanua wigo wa kibiashara na kuimarisha utafutaji wa masoko na uwekezaji leo, Jijini Dar esa salaam. Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Omani nchini Tanzania katika Sekta ya viwanda na biashara SAEED KIYUMI amesema kuwa mkutano huo utahudhuriwa na nchi Sita na Wataalamu wa masuala ya Biashara ambao watatoa mafunzo ya Kibiashara kwa wafanyabiashara wote nchini na Oman....
RAIS JAKAYA KIKWETE na mke wake Mama SALMA KIKWETE leo wanaungana na Viongozi wengine kutoka nchi mbalimbali wanaohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mpya wa Msumbiji FILIPE NYUSI mjini Maputo Msumbiji. Bwana NYUSI anachukua hatamu za uongozi kutoka kwa Rais anayemaliza muda wake ARMANDO EMILIO...
CHAMA cha maalbino nchini kimesifu uamuzi wa serikali wa kuwapiga marufuku waganga wa kienyeji wanaosababisha ongezeko la mauaji ya watu hao wenye ulemavu wa Ngozi nchini- Albino. Serikali ya Tanzania imeunda kikosi maalumu kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ukatili wanaofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi. Waziri wa mambo ya ndani, nchini , Mathias Chikawe amesema kwamba msako wa kitaifa utaanza hivi karibuni kuwakamata waganga hao na kuwafikisha mahakamani ikiwa wataendelea na kazi zao. Watu wenye ulemavu wa ngozi,...