Local News

SAMIA SULUHU AAHIDI NEEMA KWA WAKULIMA
Local News

MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu ameanza ziara yake mkoani Ruvuma akiinadi ilani ya chama hicho huku akiahidi neema kwa wakulima wa kahawa na mahindi wa mkoa huo.   Suluhu ambaye amehutubia mikutano mitatu katika majimbo mawili ya mkoa wa Ruvuma, Jimbo la Nyasa na Mbiga Vijijini, akizungumza katika mikutano yake amesema serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda itahakikisha inashusha umeme katika vijiji vyote vya mkoa huo kwa awamu ili kuchochea maendeleo ya...

Like
262
0
Wednesday, 09 September 2015
GWAJIMA AKANUSHA TAARIFA ZA DR SLAA
Local News

ASKOFU Mkuu wa kanisa la Ufufuo na uzima Josephat Gwajima amekanusha taarifa zilizotolewa dhidi yake na aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo-CHADEMA-dokta Wilbroad SLaa kuwa yeye alimpa taarifa kwamba maaskofu 30 wa kanisa katoliki walipewa fedha na mgombea urais kupitia vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya wananchi ukawa mheshimiwa Edward Lowasa ili wamuunge mkono katika harakati zake. Askofu Gwajima ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya taarifa hizo ambapo...

Like
257
0
Tuesday, 08 September 2015
NECTA YATAKA KUZIBWA KWA MIANYA YA UDANGANYIFU KWENYE MITIHANI YA DARASA LA SABA
Local News

IKIWA imesalia siku moja kuanza kwa mitihani ya taifa ya darasa la saba, baraza la mitihani nchini –NECTA– limezitaka kamati za mikoa na wilaya kuhakikisha taratibu zote za mitihani zinazingatiwa kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuzuia mianya inayoweza kusababisha udanganyifu. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo, Katibu mtendaji wa baraza hilo Dokta Charles Msonde amesema baraza hilo halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakaye jihusisha na udanganyifu katika mitihani hiyo ikiwemo kuwafutia matokeo watahiniwa...

Like
260
0
Tuesday, 08 September 2015
MZEE WA MIAKA 55 MABARONI KWA KUMBAKA MTOTO
Local News

JESHI la polisi mkoani Iringa lina mshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa jila la Augustino kavindi mwenye umri wa miaka 55 makazi wa Tanangozi kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka mitatu na kumsababishia maumivu makali mtoto huyo.   Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani humo Ramadhan Mungi amesema kuwa kuwa kabla ya jeshi la polisi kumkamata mtuhumiwa huyo alinusurika kuuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kutokana na kitendo hicho.   Wakati huo huo mwili...

Like
207
0
Tuesday, 08 September 2015
KINANA AWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUIAMINI CCM
Local News

WAKATI zoezi la uzinduzi wa kampeni za vyama mbalimbali likiendelea nchini Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi–CCM-ABDULRAHMAN KINANA amewaomba wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro kuendelea kukiamini chama hicho kwani kitaboresha shughuli za kuwaletea maendeleo.   Kinana ameyasema hayo mkoani humo wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge na Urais jimbo la Moshi mjini na kusema kuwa chama cha CCM kimeandaa Ilani yenye lengo la kusuluhisha na kumaliza kero za...

Like
206
0
Monday, 07 September 2015
TANESCO YAWATAKA WANANCHI KUFUATILIA KWA MAKINI TAARIFA ZINAZOTOLEWA NA SHIRIKA HILO
Local News

SHIRIKA la umeme Tanzania-TANESCO-limewataka watanzania kufuatilia kwa makini taarifa sahihi zinazotolewa na shirika hilo juu ya zoezi la uboreshaji wa huduma ya umeme linaloanza leo.   Akizungumza na kituo hiki, Meneja uhusiano wa Tanesco SEVELINE ADRIAN amesema kuwa oezi hilo litasaidia kuboresha kwa kiasi kikubwa huduma ya umeme na kwamba halitaathiri shughuli za wananchi kujiletea...

Like
210
0
Monday, 07 September 2015
MBAO ZAPANDA BEI
Local News

IMEBAINISHWA kuwa kutokana na kufungwa kwa Hesabu ya mapato ya mwaka 2014 kumesababisha ugumu wa upatikanaji wa mbao hali inayochangia bidhaa hiyo kuuzwa kwa bei ya juu. Wakizungumza na kituo hiki Jijini Dar es salaam wafanyabiashara wa mbao wamesema kuwa kuanzia mwezi june hadi sasa zimekuwa zikipatikana kwa shida kwenye misitu ikilinganishwa na kipindi kilichopita. Wafanyabiashara hao wamebainisha  kuwa  bei inapo kuwa juu inasababisha hata mwananchi wa kawaida kushindwa kununua  kwa sababu ya gharama zake....

Like
542
0
Monday, 07 September 2015
AZAKI YAZINDUA ILANI YA UCHAGUZI
Local News

ASASI za kiraia nchini–AZAKI-imezindua ilani inayoakisi malengo yatakayoinufaisha jamii katika kipindi cha kuelekea na baada ya uchaguzi mkuu ujao ambayo itakuwa dira na mwongozo kwa wananchi na vyama vyote vya siasa. Akifungua hafla hiyo ya uzinduzi jana katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu Bahame Tom Nyanduga amesema lengo la asasi hiyo ni kuhakikisha kunakuwa na kampeni za Amani na  uchaguzi usio wa vurugu. Aidha Nyanduga ameongeza kuwa tume imejipanga...

Like
304
0
Monday, 07 September 2015
MUZIKI MNENE BAR KWA BAR MKURANGA
Entertanment

Muziki mnene Mkuranga sherehe zilianza na ufunguzi wa mechi ya mpira wa miguu kati kikosi bora kabisa cha E-fm na Mkuranga Veteran ambapo mchezo huo ulimalizika kwa E-fm kuichabanga Mkuranga Veteran bao moja kwa sifuri, huku goli hilo la efm likiwekwa nyavuni na Rdj X five baada ya kupata pasi nzuri kabisa kutoka kwa John Makundi. Baadae moto wa burudani uliwaka pale High Way bar kwa kuwakutanisha wafanyakazi wa efm na mashabiki wake pamoja na wadau wa redio yetu Mkuranga...

Like
735
0
Monday, 07 September 2015
WATATU MBARONI KWA WIZI WA VIFAA VYA TRANSFOMA DAR
Local News

SHIRIKA la umeme nchini TANESCO kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamewakamata watu watatu wanaohusika na kuiba vifaa muhimu katika TRANSFOMA  mbili za wilaya ya Ilala na kupelekea wakazi wa maeneo hayo kukosa huduma ya umeme. Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Tanesco, Ilala ATHANASIUS MANGALI, Amesema kuwa kumekuwa na wizi wa vifaa muhimu katika transfoma ambavyo vinapelekea kifaa hicho  kushindwa kusambaza umeme ipasavyo. Amesema Tanesco kwa msaada wa karibu kutoka  jeshi la polisi jana majira ya usiku wameweza...

Like
360
0
Friday, 04 September 2015
TFDA YAZINDUA SEHEMU YA MAABARA YA UCHUNGUZI WA DAWA
Local News

MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania -TFDA imezindua sehemu muhimu ya maabara ya uchunguzi wa dawa ijulikanayo kama Microbiology Laboratory ambayo imelenga kutumika kwa ajili ya kuchunguza vijidudu  hatarishi kwa afya ya binadamu kwenye chakula, dawa, vifaa tiba pamoja na vipodozi. Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo baada ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo HIITI SILLO, amesema kuwa uchunguzi utakaofanyika katika maabara hiyo utakidhi vigezo vya uchunguzi wa kimataifa kwa mujibu wa viwango vya...

Like
387
0
Friday, 04 September 2015