Local News

NCCR YAKANUSHA KUJITOA UKAWA
Local News

CHAMA cha NCCR-MAGEUZI kimekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi wa NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura amesema kuwa chama hicho kimejitoa katika Umoja wa Katiba ya wananchi-UKAWA. Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Nccr, Nderakindo Kessy ambaye amesema kuwa wananchi waamini kuwa chama hicho hakiwezi kujitoa...

Like
216
0
Thursday, 20 August 2015
JAMII IMEOMBWA KUTAMBUA UWEPO WA WATOTO YATIMA NA WALIOTELEKEZWA
Local News

UONGOZI wa Kituo cha kulelea watoto wadogo wakiwemo yatima na waliotelekezwa na wazazi, Msimbazi centre wameiomba serikali, jamii na Taasisi mbalimbali kutambua uwepo wa watoto hao.   Akizungumza na EFM jijini Dar es Salaam mlezi wa kituo hicho sista Anna Francis amesema miongoni mwa watoto waliopo hapo ni wale waliotupwa na mama zao pindi wanapojifungua kwa visingizio mbali mbali.   Aidha sista Anna amesema kuwa mbali na kutopata misaada kutoka sehemu mbalimbali kwa sasa kituo hicho kina watoto arobaini na...

Like
238
0
Thursday, 20 August 2015
SERIKALI IMEOMBWA KULIPATIA HATI MILIKI SOKO LA NDIZI LA URAFIKI
Local News

SERIKALI  imeombwa kulipatia Hati Miliki soko la Ndizi na Matunda lililopo mabibo  urafiki jijini dar es salaam kutokana na soko hilo kukosa ufadhili wa mikopo katika benki kwa sababu ya kukosa hati hiyo.   Akizungumza na Efm Mwenyenye kiti wa Soko hilo  Bwana  KIBWANA  ALFAN  PAZI amesema kuwa endapo watapata hati miliki ya soko hilo itawasaidia  kupata wafadhili kutoka sehemu mbalimbali watakao wawezesha katika biashara yao.   PAZI amebainisha kuwa vijana wengi wameweza kujiajili wenyewe kupitia nafasi wanazo zipata katika...

Like
281
0
Thursday, 20 August 2015
MAITI YA MTOTO YAGEUKA NA KUWA MZEE ANAEKADILIWA KUWA NA MIAKA 60
Local News

KATIKA hali isiyo ya kawaida mtoto mwenye umri wa miaka 12, Neema Maginga katika Manispaa ya Musoma Mkoani Mara amefariki dunia na wakati wa maandalizi  ya mazishi yake  marehemu akabadirika kutoka umbo lake la kawaida na kuwa mzee mwenye umri unaokadiliwa kuwa miaka( 60). Akizungumzaa  na EFM katika eneo la tukio mama mzazi wa marehemu amesema ni katika hali isiyofahamika wakati wa maandalizi ya kwenda kupumzisha mwili wa marehem ndipo ilipotokea sitofahamu katika mwili wake na kubadilika katika maumbo tofauti...

Like
322
0
Wednesday, 19 August 2015
CHUO CHA SOKOINE KINATARAJIA KUWA CHUO RASMI CHA KILIMO
Local News

CHUO cha Kilimo cha Sokoine SUA kinatarajia kugeuza kitivo cha Kilimo cha chuo hicho kuwa Chuo cha Kilimo rasmi kitakachokuwa kinatoa mafunzo ya Kilimo cha kawaida na Kilimo cha Biashara ili kuboresha mfumo wa utawala na utendaji uwe wa kifanisi zaidi. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo Mgeni Rasmi Naibu Makamu Mkuu wa SUA Utawala na Fedha Profesa Yonika Ngaga amesema lengo hasa ni kuboresha taaluma kwa kurekebisha mfumo mzima wa uendeshaji, usimamizi na utendaji wa...

Like
302
0
Wednesday, 19 August 2015
JAMII IMEOMBWA KUTOWADHARAU NA KUWANYANYAPAA WAGONJWA WA SIKO SELI
Local News

JAMII imeombwa kutowadharau na kutowanyanyapaa Wagonjwa wa Siko Seli na badala yake kuwasaidia kutibu hali zao kwa kuwa asilimia 13 ya Watu wote Nchini wana vinasaba vya ugonjwa huo ambapo Tanzania imetajwa kuwa nchi ya 5 duniani kuwa na Wagonjwa wengi zaidi.   Wito huo umetolewa leo katika Uzinduzi wa Mpango wa Miaka 3 wa kupima Watoto wachanga Siko Seli utakaoenda Sanjari na Bonanza la Michezo kuadhimisha Mwezi wa kuongeza uelewa juu ya ugonjwa huo uliondaliwa na Taasisi binafsi ya...

Like
303
0
Wednesday, 19 August 2015
TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO YATAJWA KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAPATO YA SERIKALI
Local News

MATUMIZI ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali imeelezwa kuwa yamepunguza upotevu wa mapato uliokuwa ukisababishwa na watendaji wasio waaminifu. Kauli hiyo jijini Arusha  na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bwana Adorf Mapunda wakati akifunga awamu ya kwanza ya mkutano wa mwaka wa Serikali Mtandao uliowahusisha maafisa TEHAMA, Rasilimali watu, Utawala na Maafisa Habari kutoka maeneo mbalimbali nchini. Amesema mabadiliko hayo ya ukusanyaji wa fedha kielektroniki yameongeza ufanisi kwa kuongeza ukusanyaji...

Like
192
0
Wednesday, 19 August 2015
TGNP YAWATAKA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KUHUSISHA SUALA MAJI KATIKA SERA ZAO
Local News

MTANDAO wa jinsia Tanzania TGNP umeandaa warsha iliyowashirikisha wanaharakati wa masuala ya maji safi na mazingira kutoka maeneo mbalimbali ambapo wamewataka viongozi wa vyama vya siasa kuhusisha suala la maji katika sera zao. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam katika warsha hiyo Mkurugenzi wa TGNP LILIAN LIUNDI amesema kuwa maji ni tatizo sugu ambalo huwaathiri sana...

Like
162
0
Wednesday, 19 August 2015
CCM YAKAMILISHA UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE SINGIDA MASHARIKI NA KITETO
Local News

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi –CCM– Taifa katika kikao chake cha siku moja jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake Rais dokta Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto.   Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Ndugu Jonathan Njau –Singida Mashariki na Ndugu Emmanuel Papian John mgombea wa jimbo la Kiteto.   Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi...

Like
519
0
Tuesday, 18 August 2015
WANANCHI WATAHADHARISHWA KIPINDUPINDU DAR
Local News

WATANZANIA hususani wakazi wa Jiji la Dar es salaam wameombwa kuwa makini katika matumizi ya vyakula na mazingira wanayo ishi kutokana na uwepo wa ugonjwa wa kipindupindu ambao mpaka sasa umeshasababisha vifo kwa watu watatu. Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya kuenea kwa ugonjwa huohatari. Naye mganga Mkuu wa wilaya hiyo dokta Azizi Msuya amewataka wananchi kuchukua tahadhari mapema hasa wanapohisi uwepo wa dalili...

Like
264
0
Tuesday, 18 August 2015
WANANCHI WALIA NA DAWASCO KUKOSEKANA KWA MAJI KINONDONI
Local News

BAADHI ya Wananchi wa mtaa wa Mkunguni A Kinondoni Jijini Dar es salaam wameilalamikia Mamlaka ya maji safi na maji taka-Dawasco kwa kutokuwa na huduma ya maji kwa muda mrefu katika eneo hilo. Wakizungumza na kituo hiki Jijini Dar es salaam wananchi hao wamesema kuwa tatizo la kukosa maji eneo lao lipo kwa muda mrefu ingawa bado hawajui sababu japokuwa mabomba ya maji yapo. Kwa upande wake Kaimu Meneja Uhusiano wa Dawasco Evertasting Lyaro ameeleza kuwa tatizo hilo si la...

Like
368
0
Tuesday, 18 August 2015