Local News

SERIAKALI YA MTAA WA KAMBANGWA YALALAMIKIWA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
Local News

WANANCHI  wa kata ya Makumbusho wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam wameilalamikia serikali ya mtaa wa Kambangwa kwa kitendo cha watendaji hao kujichukulia sheria mkononi ya kuwatoza faini juu ya matumizi ya huduma za kijamii ambazo kwa mujibu wa halmashauri huduma hizo hutolewa bure. Aidha wanachi hao wameshindwa kufahamu mapato na matumizi ya ofisi ya serikali yao kutokana na kutoitwa katika vikao tangu kupatikana kwa uongozi mpya mwishoni mwa mwaka jana. Akizungumza na kituo hiki jijini hapa mwenyekiti wa...

Like
228
0
Tuesday, 11 August 2015
KAMPUNI ZINAZOTUMIA MITANDAO ZIMETAKIWA KULINDA TAARIFA ZAO
Local News

KUTOKANA na ongezeko la uhalifu katika mitandao ya kijamii, kampuni mbalimbali nchini zinazojihusisha na shughuli zake kwa kutumia Mitandao zimetakiwa kuongeza umakini katika kulinda taarifa zao dhidi ya watumiaji wabaya wa mitandao hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano uliowakutanisha wataalamu mbalimbali wanaoshughulika na mifumo ya k ompyuta, mtendaji mkuu wa wakala wa serekali mtandao Dokta GABRIEL BAKARI amesema kuwa sekta ya teknolojia inakuwa kwa kasi nchini hivyo ni vyema tahadhari za kulinda mitandao hiyo...

Like
212
0
Tuesday, 11 August 2015
WANASIASA WATAKIWA KUWA NA MSIMAMO NA VYAMA VYAO
Local News

KUFUATIA matukio kadhaa ya wanasiasa kuvihama vyama vyao baada ya kuenguliwa katika kinyang’anyilo cha  kugombea nyadhifa mbalimbali Msanii wa sanaa ya Uigizaji Nchini Steven Mengere amewataka Wanasiasa kuwa na Msimamo ndani ya vyama vyao.   Mengere ameyasema hayo wakati akizungumza na kituo hiki  na kudai  kuwa mfumo huo umekuwa ndio kimbilio la Wanasiasa wanaokosa sifa za kugombea kupitia vyama vyao wakidhani kwamba hiyo ndio njia ya kupata uongozi.   Amebainisha kuwa  pamoja na kushindwa katika kinyang’anyilo hicho ni...

Like
194
0
Tuesday, 11 August 2015
WATUMISHI WA SERIKALI WAASWA KUWA NA NIDHAMU YA MATUMIZI YA RASILIMALI FEDHA
Local News

WATUMISHI wa Serikali wameaswa kuwa na nidhamu ya matumizi bora ya rasilimali fedha ili kuleta ufanisi na maendeleo endelevu kwa manufaa ya wananchi.\   Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha dokta Servacius Likwelile alipokuwa akiongea na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya wafanyakazi wa Hazina Ndogo mkoani Lindi .   Dokta Likwelile amesema kuwa Serikali inafanya mapitio ya Mkakati wa Kupunguza Umasikini Tanzania –MKUKUTA- na kuhakikisha kuwa changamoto zilizokuwepo awali zinapatiwa ufumbuzi ili kuleta tija na...

Like
280
0
Tuesday, 11 August 2015
MUZIKI MNENE BAR KWA BAR 2015
Entertanment

BAADA ya kumalizika kwa Tamasha la muziki mnene Bar kwa bar awamu ya kwanza, na mashabiki kuomba Burudani hiyo iendelea tena, Uongozi Efm umekubali ombi hilo na sasa Tamasha hilo linarudi tena kwa kishindo likiwa  limeboreshwa kwakuongeza wigo wa kuwafikia watu wengi zaidi. Muziki mnene bar kwa bar awamu hii bila kuwasahamu wasikilizaji na mashabiki wa EFM katika wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala kwa umuhimu wake na Wilaya mpya katika mkoa wa Dar es salaam, Muziki mnene sasa utapelekwa...

Like
652
0
Monday, 10 August 2015
WATANZANIA WAMEOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUCHANGIA MFUKO WA UWEZESHAJI WATU WENYE ULEMAVU
Local News

WATANZANIA wameombwa kujitokeza kwa wingi katika kuchangia mfuko wa uwezeshaji watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali kwa lengo la kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili watu hao.   Akizungumza na kituo hiki Jijini Dar es salaam makamu mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu wilaya ya Temeke Shany Zubery amesema kuwa endapo suala la uchangishaji litafanikiwa litasaidia kwa kiasi kikubwa kuwasaidia watu hao.   Aidha amesema kuwa shirikisho hilo limekuwa likikabiliwa na changamoto nyingi ambazo husababisha kushindwa...

Like
324
0
Monday, 10 August 2015
CHADEMA KUFANYA MAANDAMANO KUMSINDIKIZA LOWASA KUCHUKUA FOMU
Local News

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimesema hakijapata taarifa ya Jeshi la polisi inayowazuia kufanya maandamano ya kumsindikiza mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi –UKAWA– Edward Lowasa anayetarajia kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo leo katika ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC- akiambatana na Mgombea mwenza Juma Duni Haji.   Jeshi la Polisi kanda  Maalumu ya Dar es salaam limepiga marufuku maandamano ya mgombea huyo kwenda kuchukua fomu NEC kwa maandamano yanayoanzia ofisi za CUF...

Like
281
0
Monday, 10 August 2015
VIONGOZI WA VIJIJI MANYARA WATAKIWA KUFANYA MAAMUZI KWA KUFUATA SHERIA KUMALIZA MIGOGORO
Local News

VIONGOZI wa vijiji katika Wilaya ya Babati Mkoani Manyara wametakiwa kufanya maamuzi kwa kufuata sheria ili kumaliza migogoro ya ardhi kwa kutotoa nafasi kwa watu wanaotumia fedha kujipatia ardhi. Mkuu wa wilaya hiyo Crispin Meela ameyasema hayo katika kijiji cha Kiongozi wakati akizungumza na wakazi wa eneo hilo kuhusiana na migogoro ya ardhi ambayo imekithiri vya kutosha wilayani humo. Aidha amesema sheria inapaswa kusimamiwa kwani watendaji hao wanatambua wazi kuwa mtu mwenye fedha hana haki kwenye mgogoro lakini wanajipa upofu...

Like
267
0
Friday, 07 August 2015
JESHI LA POLISI DODOMA YATANGAZA KUTOA MILIONI 5 KWA ATAKAEFANIKISHA KUKAMATWA KWA WAUAJI KATIKA KITUO CHA MAFUTA
Local News

JESHI la polisi mkoani Dodoma limetangaza kutoa zawadi ya shilingi milioni tano kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa majambazi waliohusika na tukio la mauaji ya walinzi wawili katika kituo cha mafuta cha state oil kilichopo eneo la kisasa manispaa ya Dodoma. Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma DAVID MISIME amesema majambazi hao wamefanya uharifu huo na kufanikiwa kupora vitu mbalimbali pamoja na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 10 Aidha kamanda misime ameiasa jamii...

Like
327
0
Friday, 07 August 2015
WAGOMBEA URAIS KUPITIA CCK NA ADC WANATARAJIWA KUCHUKUA FOMU NEC LEO
Local News

WAGOMBEA urais kupitia chama cha Kijamii-CCK na Alliance for Democratic Change-ADC, leo wanatarajiwa kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC , Jijini Dar es salaam. Hivi karibuni ADC ilimtangaza Chifu Lutalosa Yemba kuwa mgombea wake wa urais huku Mwenyekiti wa chama hicho Said Miraji Abdallah akitajwa kuwa mgombea mwenzake. Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi-NEC, baada ya vyama hivyo viwili kuchukua fomu leo, itafuatiwa na na ACT Wazalendo ambapo mgombea wake anatarajiwa kuchukua...

Like
210
0
Friday, 07 August 2015
RAIS KIKWETE KUZINDUA RASMI BENKI YA KWANZA YA MAENDELEO YA KILIMO
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete leo anazindua rasmi benki ya kwanza ya Maendeleo ya Kilimo ambayo inalenga kuanzisha mtazamo mpya wa kukiendeleza kilimo kupitia kushirikisha wadau mbalimbali kwa kuangalia kila mnyororo wa thamani kwa ukamilifu wake pamoja na kuwa na ubunifu katika kuchangia fedha kwenye miradi mbalimbali ya sekta ya Kilimo. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kwa awamu mbili ambapo kwa awamu ya kwanza atazindua Makao Makuu ya Benki hiyo leo Jijini Dar es salaam...

Like
264
0
Friday, 07 August 2015