Local News

3 MBARONI TUHUMA ZA MAUAJI YA AFISA WA POLISI ELIBARIK PALANGO
Local News

JESHI la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwatia  mbaroni watuhumiwa watatu kwa  tuhuma za mauaji ya aliyekuwa afisa wa polisi ELIBARIK PALANGO yaliyotokea nyumbani kwakwe Yombo kilakala tarehe 4 mwezi huu. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es  salaam leo Naibu kamishna wa polisi kanda maalum Dar es salaam SIMON SIRRO amesema kuwa watuhumiwa hao ambao ni madereva bodaboda wamekamatwa baada ya jeshi kufanya msako mkali katika jiji la Dar es salaam. Aidha Kamishna SIRRO amewataja...

Like
459
0
Thursday, 06 August 2015
PROF. LIPUMBA AJIENGUA UWENYEKITI CUF
Local News

MWENYEKITI wa chama cha wananchi –CUF, Profesa Ibrahim Lipumba leo ametangaza rasmi kujiengua nafasi hiyo kutokana na umoja wa katiba ya wananchi –UKAWA, kushindwa kuenzi na kuzingatia tunu za Taifa juu ya rasimu ya katiba pendekezwa.   Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam, Profesa Lipumba ameeleza kuwa tunu hizo ni pamoja na kushindwa kufahamu utu wa watanzania juu ya kuipata katiba pendekezwa uzalendo, uadilifu umoja, uwazi na uwajibikaji.   Amefafanua kuwa kutokana na maudhui ya rasimu ya...

Like
207
0
Thursday, 06 August 2015
SERIKALI YAAHIDI KUBORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WA MAHAKAMA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa JAKAYA MRISHO KIKWETE amesema kuwa serikali itaendelea kushughulikia ipasavyo suala la uboreshaji wa maslahi kwa watumishi wa mahakama kwa manufaa ya utumishi wao. Rais Kikwete ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuwaaga rasmi viongozi na watumishi mbalimbali wa mahakama nchini Tanzania. Katika hafla hiyo rais Kikwete amesema kuwa kwa kipindi cha miaka kumi aliyokaa madarakani amejitahidi kuboresha shughuli za mahakama kwa kuongeza idadi ya...

Like
394
0
Thursday, 06 August 2015
MAONYESHO YA UGUNDUZI WA KISAYANSI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI KUFANYIKA LEO DAR
Local News

MASHINDANO maalum ya maonyesho ya kazi za kigunduzi na kisayansi zilizofanywa na baadhi ya wanafunzi wa shule za Sekondari nchini yanafanyika leo nchini. Maonyesho hayo ambayo yanafanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na rais Mstaafu wa awamu ya pili  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ALLY HASSAN MWINYI yameandaliwa na Taasisi ya Young Scientist Tanzania-YST yakiwa na lengo la kuwatia moyo vijana wakitanzania waliopo shuleni kupendelea kusoma masomo ya sayansi  ambayo yatachangia kupata wagunduzi na watafiti wa kutosha katika...

Like
359
0
Thursday, 06 August 2015
RAIS KIKWETE KUWAAGA VIONGOZI NA WATUMISHI WA MAHAKAMA LEO
Local News

RAIS wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete anawaaga rasmi viongozi na watumishi wa Mahakama leo.   Akiwa katika hatua za kumaliza muda wake madarakani, Rais Kikwete pia jana aliwaapisha Majaji 14 akiwamo Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani Tanzania katika sherehe iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.   Rais Kikwete aliwateua majaji hao hivi karibuni katika mwendelezo wake wa kuhakikisha kuwa Muhimili wa Mahakama unakuwa na raslimali watu ya kutosha ili kuendelea kutoa haki kwa haraka na...

Like
276
0
Thursday, 06 August 2015
INDIA YATOA NAFASI YA MASOMO YA HABARI NA TEKNOLOJIA KWA WANAFUNZI WA TANZANIA
Local News

IMEELEZWA kuwa Kutokana na ushirikiano uliopo katika sekta ya Elimu kati ya Tanzania na India wanafunzi wanaosoma masomo ya Teknolojia ya habari, mawasiliano na Maendeleo wamepewa nafasi ya kujiendeleza zaidi katika Ngazi ya shahada ya Udhamivu katika chuo cha Avinashillingam University nchini India. Akizungumza na waandishi wa Habari katika mahafali ya 9 ya chuo cha usimamizi wa fedha IFM jijini Dar es salaam, Mkuu wa chuo hicho Profesa GODWIN MJEMA amesema kuwa  nafasi hiyo itawasaidia wanafunzi wa Tanzania kuweza kujiendeleza...

Like
295
0
Wednesday, 05 August 2015
BODI YA USAJILI WAHANDISI YATENGENEZA AJIRA 1600
Local News

BODI ya Usajili wa Wahandisi nchini Tanzania –ERD, imefanikiwa kutengeneza ajira elfu 1,600 kwa Watanzania kufuatia usajili wa kampuni 160 ya ushauri wa kihandisi zilizoanzishwa kote nchini katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2005 hadi 2015.   Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuelezea mafanikio ya Bodi hiyo kwa kipindi cha miaka 10, Msajili wa Wahandisi nchini,  Muhandisi Steven Mlope amesema kuwa kwa kusajili kampuni 160 katika kipindi cha miaka 10 pia wamefanikiwa kusajili wahandisi wapatao elfu...

Like
269
0
Wednesday, 05 August 2015
MAGUFULI ACHUKUA FOMU NEC KUWANIA URAIS
Local News

Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi –CCM-dokta JOHN MAGUFULI leo amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika ofisi ya uchaguzi-NEC. Akizungumza mbele ya mamia ya wanachama na wananchi mbalimbali waliojitokeza kwaajili ya kumpa salam dokta Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa hatowaangusha endapo atapewa ridhaa na wananchi kuliongoza Taifa. Awali akimkaribisha dokta Magufuli mwenyekiti wa chama hicho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kwa kipindi kirefu chama hicho...

Like
199
0
Tuesday, 04 August 2015
RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MZEE PETER KISUMO
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini Mzee Peter Kisumo. Marehemu Mzee Kisumo alishawahi kuwa kiongozi wa Chama cha TANU, Muasisi na mdhamini wa Chama cha CCM na aliyeshikilia nafasi nyingi za uongozi ndani ya Serikali na utumishi wa umma ukiwemo uwaziri. Katika salamu zake Rais Kikwete amesema kwamba taifa limeondokewa na kiongozi wa kuigwa katika utumishi uliotukuka wa umma na Chama cha Mapinduzi....

Like
379
0
Tuesday, 04 August 2015
CHAMA CHA MADEREVA KIMETISHIA KUFANYA MAAMUZI MAZITO AGOSTI 9
Local News

CHAMA cha Wafanyakazi madereva Tanzania-TADWU kimesema endapo vipengele viwili vya maboresho ya mishahara na posho havitazingatiwa kulingana na makubaliano walioafikiana katika kikao cha juni 21 mwaka huu baina ya kamati ya kudumu, Sumatra na Wamiliki wa vyombo vya usafiri chama hicho kitatoa maamuzi mazito ifikapo tarehe 9 Agosti mwaka huu. Akizungumza na Efm jijini Dar es salaam Katibu na Msemaji wa TADWU Rashid Salehe amesema kikao cha mwisho kilikubaliana kuwa ifikapo tarehe 1 Julai mikataba mipya iliyoundwa kwa pamoja ianze...

Like
180
0
Tuesday, 04 August 2015
MAGUFULI KUCHUKUA FOMU NEC LEO
Local News

MGOMBEA wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi-CCM dokta JOHN POMBE MAGUFULI leo anatarajia kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC. Katika Zoezi la uchukuaji wa fomu pia Mheshimiwa MAGUFULI ataambatana na mgombea mwenza wa chama hicho kutoka Zanzibar SAMIA SULUHU HASSANI. Mbali na kuchukua fomu mheshimiwa Magufuli atapata nafasi ya kukutana na wadau wa siasa wakiwemo wananchi katika ofisi ndogo za CCM ili aweze kuwapa...

Like
222
0
Tuesday, 04 August 2015