UKAWA umetangaza rasmi kumkaribisha waziri Mkuu wa zamani Edward Lowasa kuungana na Umoja huo nakusema kuwa wapo tayari kushirikiana naye na kumpa nafasi. Akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti mwenza wa UKAWA, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha NCCR –Mageuzi Mheshimiwa James Mbatia amesema Ukawa wanamkaribisha na yuko huru kuamua chama anachotaka kuungana nacho. Tamko hili la leo limekuja baada ya kuwepo na vuta nikuvute katika vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya...
MUUNGANO wa Taasisi zinazoshughulikia maradhi yasiyoambukiza Zanzibar –ZNCDA- umeishauri Serikali na Mashirika wahisani kuelekeza nguvu zao katika mapambano dhidi ya maradhi hayo kwani yamekuwa tishio kwa maisha ya wananchi kuliko maradhi mengine Zanzibar. Mratibu wa –ZNCDA– Omar Abdalla Ali ametoa ushauri huo wakati wa zoezi la kuwapima afya wananchi wa shehia za Karakana, Chimbuni na Muembemakumbi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Omary amesema maradhi ya Shinikizo la damu, Kisukari na Saratani ...
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni –UNESCO- limeahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na wananchi wenye uwezo mkubwa wa uvumbuzi kupitia elimu bora. Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa Unesco nchini Al Amin Yusuph wakati akizungumza na washiriki wa kongamano maalumu wa kupitia waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu. Kongamano hilo ni moja ya mradi wa CFIT unaoendeshwa na shirika hilo na serikali...
SERIKALI imeshauriwa kutoa elimu ya uhifadhi mazingira kwa kuzingatia sera ya mazingira kwa wananchi wanaoishi katika mkoa wa Lindi na Mtwara ambayo itasaidia kuongeza uwekezaji katika mikoa hiyo. Akizungumza na Kituo hiki leo Afisa msimamizi kutoka baraza la taifa la hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC Muhandisi JAMES NGELEJA amesema kuwa kutokana na kugundulika kwa gesi katika mikoa hiyo hali hiyo itachangia kuongeza kiwango cha uwekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya utalii. Amebainisha kuwa mbali na kutoa elimu ya utunzaji...
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaa Muheshimiwa SAID MECK SADIKI amewataka Wamiliki wa Viwanda ambao bado hawajatoa Taarifa za viwanda vyao kwa wadadisi na wasimamizi wa zoezi hilo kufanya hivyo mara moja kwani muda wa kukamilisha zoezi hilo umeongezwa hadi mwisho mwa mwezi wa nane mwaka huu. Ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa lengo kuu la sensa ya viwanda ni kukusanya takwimu sahihi zinazohusu sekta hiyo hapa nchi pamoja na mkoa kwa...
KAMISHINA wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa amesisitiza haja ya kuhakikisha kwamba viwango vya umahiri vya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini vinakua vya juu kukidhi haja ya matumizi ya kufundishia na kujifunza nchini. Ametoa kauli hiyo mjini Bagamoyo wakati akifungua kongamano linalohusu upitiaji waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu. Katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa amesema kwamba changamoto ya Tehama inaonekana wazi katika matumizi yake na...
ZAIDI ya kaya 260 waathirika wa mafuriko wanaoishi kwenye mahema katika eneo la mateteni wilayani kilosa mkoani morogoro wanaishi maisha magumu kwa kutegema viazi vitamu na wengine wanalazimika kulala nje na familia zao kutokana na uchakavu wa mahema. wakizungumza kwa uchungu waathirika hao wamelalamikia kuendelea kuishi maisha magumu kutokana na uchakavu wa mahema ambapo baadhi yao wanalala nje na watoto na kuishi kwa kutegemea viazi vitamu kusukuma maisha. Hata hivyo, wameiomba Serikali kuwaonea huruma kwa watu hao kutokana na maisha...
ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Wawi kisiwani Zanzibar kupitia chama cha wananchi-CUF– Mheshimiwa HAMAD RASHID leo amekabidhiwa rasmi kadi ya kuwa mwanachama wa chama cha Alliance for Democratic Change-ADC. Akizungumza wakati wa kumkabidhi kadi hiyo ya uwanachama, Mwenyekiti wa –ADC- Taifa SAID MIRAJI amesema ni muda muafaka sasa kwa watanzania kuwa wamoja ili kuleta maendeleo kwa Taifa. Aidha amevihakikishia vyama vingine vya siasa kuwa chama chao kipo tayari kushirikiana kwa masuala muhimu na yenye maslahi kwa wananchi...
WATU kumi wamefariki dunia papo hapo na wengine 47 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya simiyu express lililokuwa likitokea bariadi mkoani simiyu kuelekea jijini dar es salaam kupasuka tairi la mbele na kupoteza mwelekeo na kisha kuparamia mti katika kijiji cha Wilunze eneo la Chalinze nyama wilayani Chamwino Mkoani Dodoma. Kwa mujibu wa mashuhuda wamesema kabla ya ajali, basi hilo lenye namba za usajili T 318 ABM Scania lilikuwa kwenye mwendo mkali na wakasikia kishindo cha kupasuka kwa tairi....
ALIEKUA Diwani wa Kata ya Kunduchi kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA- ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama hicho -BAWACHA-jimbo la Kawe Janeth Rithe ameachana na chama hicho na kujiunga na chama cha ACT WAZALENDO akiambatana na Viongozi wenzake 12 wa jimbo la Kawe. Akiongea na Waandishi wa Habari Mara baada ya kukabidhiwa kadi ya Chama cha ACT WAZALENDO Rithe amesema amechukua uamuzi huo baada ya kusoma sera na kugundua kua hicho ndio chama kinachosimamia...
JOPO la Madaktari kutoka Hospitali mbalimbali za Marekani wameanza kutoa huduma za kiafya katika Hospitali ya Serikali ya Mwananyamala kwa Wagonjwa mbalimbali wenye matatizo ya kansa, kinywa, macho, kisukari pamoja huduma nyingine za kiafya Wataalam hao walioshirikiana na Jumuiya ya Watanzania waishio Marekani na Taasisi ya Wanaawake wa Afrika ya Kupambana na Kansa-AWCA wanatarajia kuhudumia wagonjwa zaidi ya 600 katika maeneo ya Dar es salaam na Zanzibar ambapo Jopo hilo limechangia dawa zenye thamani ya takribani Milioni 200 kwa Watanzania....