Local News

MWILI WA BRIGEDIA JENERALI MSILU WAAGWA LEO DAR
Local News

MWILI wa aliyekuwa Brigedia Jenerali mstaafu Dismas Stanslaus Msilu umeagwa leo katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na mazishi yanatarajiwa kufanyika Mkoani Iringa kesho.   Brigedia Jenerali mstaafu Dismas alifariki dunia katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo July 19 mwaka huu. Marehemu Brigedia Jenerali Msilu alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania mwaka 1975 na Alistaafu utumishi Jeshini mwaka...

Like
369
0
Wednesday, 22 July 2015
WAKAZI DAR WAANZA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Local News

WAKAZI wa Mkoa wa Dar es salaam leo wameanza Zoezi la kujiandikisha katika Dafutari la Kudumu la mpiga kura kwa njia ya Kielektroniki- BVR. Efm imepita katika vituo mbalimbali vya kujiandikishia na kushuhudia misururu ya watu ambao wamewahi vituoni humo kwa lengo la kutimiza haki yao hiyo ya msingi kikatiba. Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wananchi wamedai kuchelewa kwa waandikishaji katika vituo, ikizingatiwa kuwa ni siku za kazi hivyo kuiomba Tume ya Uchaguzi kulizingatia hilo ili watu wapate nafasi...

Like
250
0
Wednesday, 22 July 2015
ZAIDI YA WATU LAKITANO KUFANYIWA UPASUAJI VIKOPE CHINI YA WIZARA YA AFYA KANDA YA KASKAZINI
Local News

WIZARA ya Afya na ustawi wa jamii inatarajia kuwafanyia upasuaji vikope zaidi ya watu laki tano nchini kipindi kifupi kijacho katika eneo la Kanda ya Kaskazini kufuatia Wilaya za Arusha kuongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi wa Trkoma. Hayo yamesemwa na mratibu wa kitaifa wa mpango wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele dokta Upendo Mwingira wakati akiwapokea wageni kutoka shirika lisilo la kiserikali la Ending Neglected Disease la nchini Marekani. Akizungumza na kituo hiki Jijini Sinya Longido dokta Mwingira amesema zoezi hilo la...

Like
190
0
Tuesday, 21 July 2015
NEC YATAKIWA KUREKEBISHA KASORO ZILIZOJITOKEZA KWENYE UANDIKISHWAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Local News

MTANDAO wa Asasi za Kiraia wa Kuangalia Chaguzi Tanzania-TACCEO unaoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu  umeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwenye mikoa mingine wakati wa uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ili kuepuka kufanya makosa hayo katika mkoa wa Dar es Salaam hapo kesho. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa mtandao huo MARTINA KABISANA amesema kuwa  ni vyema NEC ikahakikisha inatatua mapema changamoto ya kuharibika...

Like
211
0
Tuesday, 21 July 2015
ASILIMIA 70 YA WAGONJWA WA SARATANI HUPOTEZA MAISHA KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA
Local News

IMEELEZWA kuwa asillimia 70 ya wagonjwa wa saratani hupoteza maisha katika nchi zinazoendelea na katika Bara la Afrika lenye watu zaidi ya milioni 804 asilimia  12.4 wanapata saratani kabla ya kufikia umri wa miaka 75  na asilimia  90 wanapata ugonjwa huo wakiwa na  umri chini ya miaka 40.   Hayo yamesemwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati akifungua mkutano wa tisa wa Jukwaa la wake wa marais wa Afrika la kutokomeza magonjwa ya saratani za mfumo wa uzazi ambazo...

Like
233
0
Tuesday, 21 July 2015
MOSES MACHALI KUJIUNGA NA ACT LEO
Local News

KIONGOZI wa chama cha –ACT-Wazalendo Zitto Kabwe leo anampokea Mbunge wa Kasulu, mjini Moses Machali kutoka chama cha –NCCR-Mageuzi ambaye atajiunga na kutatambulishwa rasmi kuwa mwanachama wa –ACT-Wazalendo.   Machali anaambatana na Madiwani wawili, Kamishna wa mkoa mmoja na katibu wake pamoja na wenyeviti na makatibu wa kata 12 zilizo katika jimbo la Kasulu mjini., Pia katika mapokezi hayo kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe atawapokea makatibu uenezi 9 wa jimbo hilo lenye jumla ya kata 15 za uchaguzi.  ...

Like
241
0
Tuesday, 21 July 2015
WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO WAMETAKIWA KUTII SHERIA BILA SHURUTI
Local News

WAMILIKI wa vyombo vya moto hususani madereva wametakiwa kutii sheria bila shuruti kwa kufuata utaratibu wa usalama ili kuepusha madhara yanayojitokeza mara kwa mara barabarani.   Rai hiyo imetolewa na Askari wa usalama barabarani eneo la Kawe WIPI HAPPY wakati akizungumza na kituo hiki leo jijini Dar es salaam mara baada ya kutokea vurugu zilizosababishwa na mmoja wa madereva ambaye hakutaka kutii sheria iliyowekwa na Askari huyo.   Hali hiyo imekuja kufuatia Lori la mizigo kufunga barabara ya Mwai Kibaki...

Like
215
0
Monday, 20 July 2015
JESHI LA POLISI LIMEFANIKIWA KUKAMATA SILAHA ZILIZOPORWA NA MAJAMBAZI KATIKA KITUO CHA SITAKISHARI
Local News

JESHI la Polisi Nchini limefanikiwa kukamata silaha zilizoporwa na majambazi katika kituo cha Polisi Sitakishari pamoja na fedha kiasi cha shilingi milioni 170.   Katika Operesheni hiyo Jeshi lilifanikiwa kukamata watuhumiwa watano ambapo wawili walipoteza maisha katika mapambano pamoja na silaha 16,  14 zikiwa za Staki shari, risasi 53 ambazo kati yake 28 zinatoka katika kituo hicho cha polisi, Stakishari.   Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu wa Dar es salaam...

Like
563
0
Monday, 20 July 2015
ZOEZI LA KURA ZA MAONI KUANZA LEO CHADEMA
Local News

BAADA ya mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uteuzi wa ndani wa nafasi ya ubunge kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo kumalizika, imeelezwa kuwa zoezi la kura za maoni linaanza leo hadi julai 25 mwaka huu.   Katika hatua hiyo kila uongozi wa kanda umepanga ratiba yake ya kura za maoni katika majimbo mbalimbali kwa kuzingatia kuwa zoezi hilo limeagizwa kufanyika na kumalizika ndani ya siku 6 katika majimbo yote ya uchaguzi nchi nzima.   Hata hivyo  taarifa...

Like
269
0
Monday, 20 July 2015
KUSHIRIKISHA WANANCHI KIKAMILIFU KWENYE NGAZI ZA MAAMUZI NI CHACHU YA MAENDELEO
Local News

IMEELEZWA kuwa ili kuleta maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii katika majimbo mbalimbali yanayoongozwa na viongozi wa siasa nchini hususani wabunge, Viongozi hao wanapaswa kufuatilia kwa umakini shughuli zote za kiutendaji zinazofanyika kwenye majimbo yao pamoja na kuwashirikisha wananchi kikamilifu kwenye ngazi za maamuzi. Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi-CCM, CHRISTOPHER JAFET alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya nia yake ya kugombea nafasi ya ubunge wa Jimbo la Segerea kwa tiketi...

Like
175
0
Monday, 20 July 2015
FAMILIA ILIYOTELEKEZWA YAPATIWA MAKAZI YA MUDA NYAMAGANA, MWANZA
Local News

FAMILIA yenye watoto saba  iliyotelekezwa katika mtaa wa Igelegele wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza imepewa makazi ya muda na balozi wa mtaa huo baada ya kuteseka kwa muda mrefu. Akizungumza na kituo hiki mmoja wa mtoto wa familia hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Grece  amesema  makazi hayo ya muda yamewasaidia kwa kiasi kikubwa kwani mwanzo walikuwa wakilala nje na hawakuwa na chakula. Hata hivyo amesema kuwa kwa upande wa masomo  ameathirika kwa kiasi kikubwa kwani toka shule imefunguliwa  hajahudhulia masomo...

Like
275
0
Friday, 17 July 2015