Local News

BANZA STONE AFARIKI DUNIA
Entertanment

MSANII  mkongwe wa muziki wa dance Tanzania, Ramadhan Masanja maarufu  Banza Stone  amefariki dunia leo mchana baada ya kuugua kwa muda mrefu. Akizungumza na efm kwa njia ya simu, kaka wa Marehemu Jabir Masanja amethibitisha kutokea kwa msiba huo na kwamba taratibu zote zinafanyika nyumbani kwao Sinza jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, Banza alikuwa anasumbuliwa na fangasi waliokuwa wanamshambulia kichwani (ubongo) na shingoni. EFM  inatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki na Wapenzi wa Muziki...

Like
338
0
Friday, 17 July 2015
JK: UTETEZI WA BARA LA AFRIKA NI WAJIBU WA MABALOZI KWENYE UMOJA WA MATAIFA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa Mabalozi wa Afrika katika Umoja wa Mataifa kulitetea Bara hilo kwa sababu hamna mtu mwingine atakayetetea maslahi ya Afrika. Aidha, Rais Kikwete  amesema kuwa ni wajibu wa kila nchi kuamua aina ya mfumo wa kisiasa ambao unaifaa nchi husika bila kulazimika kuwepo ukomo wa kiongozi kukaa madarakani. Rais Kikwete ametoa ufafanuzi huo jana wakati alipozungumza na Mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao katika Umoja...

Like
254
0
Friday, 17 July 2015
MBIO ZA UBUNGE CCM ZAANZA DAR
Local News

JUMLA ya wanachama 36 wa chama cha mapinduzi-CCM-wamejitokeza kutaka kugombea nafasi za ubunge kupitia chama hicho katika majimbo manne ya Kinondoni, Kawe, Ubungo na Kibamba.   Hayo yamesemwa na katibu wa –CCM– wilaya ya kinondoni ATHUMAN SHESHA alipokuwa akizungumza na kituo hiki ambapo amesema kuwa hadi sasa jimbo la Kawe linaongoza kwa kuwa na wagombea wengi wapato 15.   SHESHA amesema kuwa kila mgombea aliyefika kuchukua fomu amepewa mashariti ya kugombea nafasi hiyo ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo...

Like
216
0
Friday, 17 July 2015
SHIRIKA LA THE FOUNDATION FOR TOMORROW LAZINDUA KAMPENI KUSAIDIA ELIMU YA WATOTO WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU
Local News

SHIRIKA lisilo la kiserikali la The Foundation for Tomorrow limezindua kampeni ya kuchangia SHAMIRI ya kusaidia elimu ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu lengo ni kuchangisha kiasi cha shilingi milioni 50 zitakazowawezesha kupata elimu bora na kuondokana na mazingira yanayowakabili.   Meneja Mahusiano wa shirika hilo Anton Asukile ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampeni maalumu ya SHAMIRI inayolenga kusaidia ustawi wa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.   Asukile ameiomba jamii ya Watanzania kushiriki katika...

Like
207
0
Friday, 17 July 2015
POLISI YAPANGA KUIMARISHA ULINZI TEMEKE KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU
Local News

JESHI la Polisi mkoa wa kipolisi wa Temeke limesema kuwa limejipanga kuimarisha ulinzi kwenye maeneo yote katika kipindi hiki cha sikukuu kuanzia katika maeneo ya Ibada. Akizungumza na Efm kamanda wa Polisi mkoa huo Andrew Satta amewataka wananchi kudumisha ulinzi wa mali zao katika kipindi hiki cha sikukuu ya Iddy el fitri. Kamanda Satta amewataka wananchi kutojisahau na kuacha nyumba zikiwa zimefungwa na badala yake waache mtu mzima ili kuzuia vitendo vya uhalifu....

Like
311
0
Thursday, 16 July 2015
JK AKUTANA NA KOFI ANNAN
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan. Katika mkutano huo kwenye Hoteli ya Intercontinental, viongozi hao wawili wamezungumzia masuala mbali mbali ya kimataifa, ikiwamo hali ya Burundi. Hapo jana Mwenyekiti huyo  wa Jopo la Kimataifa Linalopendekeza Jinsi Dunia inavyoweza kukabiliana na majanga yajayo ya magonjwa ya milipuko, ameongoza vikao vya Jopo hilo ambalo kazi yake imeungwa mkono na nchi 21 ambazo zilichangia mapambano...

Like
181
0
Thursday, 16 July 2015
NYUKLIA: OBAMA ATOA SHUKRANI ZAKE KWA RAIS WA URUSI
Local News

RAIS wa Marekani Barack Obama amezungumza na mwenzake Vladmir Putin, akimshukuru rais huyo wa Urusi kwa mchango wake katika kufanikisha makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran. Ikulu ya Marekani ya White House imesema viongozi hao wawili waliahidi kuendelea kuwa na mawasiliano ya karibu, na watashirikiana pamoja . Lakini hakukuwa na kauli yoyote kuhusu mgogoro unaoendelea nchini Ukraine....

Like
178
0
Thursday, 16 July 2015
TARIME: MADIWANI WAITAKA HALMASHAURI KUJENGA SHULE ZA KUTOSHA KWA AJILI YA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM
Local News

KATIKA kutambua umuhimu wa watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo  walemavu wa vioungo mbalimbali , Madiwani wa Halmshauri ya Mji wa Tarime Mkoani  Mara wameitaka Halmshauri hiyo kujenga shule za kutosha  kwa ajili ya walemavu hao. Hata hivyo wameitaka pia jamii nzima kuondokana na utamaduni wakudhani kuwa ulemavu ni mkosi katika familia na kutowaficha watu hao na badala yake wawapeleke shule kwa lengo la kupata Elimu kwani ni haki yao ya Msingi. Kauli hiyo ya Madiwani imetolewa katika kikao chao cha kuvunja...

Like
213
0
Thursday, 16 July 2015
WATANZANIA WATAKIWA KUZIDISHA MSHIKAMANO NA UMOJA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Local News

WAUMINI wa Dini  ya  Kiislamu pamoja  na Watanzania kwa ujumla wametakiwa kuzidisha  mshikamano na umoja  hasa katika  kipindi  hiki  ambacho  nchi  inaelekea kwenye uchaguzi mkuu.   Hayo yamesemwa  Jijini  Dar es salaam na  Sheikh  Mkuu wa Mkoa huo ALHAD MUSSA SALIM alipo kuwa anatoa  mwaliko wa kuswali pamoja  swala ya idd el fitr kwa  waumini wa dini hiyo katika viwanya vya mnazi mmoja  ambayo itategemea na kuandama  kwa mwezi kati ya tarehe 17 au 18.   Alhad  amesema kuwa sikukuu...

Like
214
0
Thursday, 16 July 2015
WAPIGANAJI WANAOMUUNGA MKONO RAIS WA YEMEN WAUTWAA MJI WA ADEN LEO
Local News

TAARIFA za kijeshi zimesema wapiganaji tiifu kwa upande wa rais wa Yemen wamefanikiwa kuyadhibiti maeneo kadhaa ya mji wa Aden leo, baada ya kuukomboa uwanja wa ndege wa mji huo ambao ulikuwa ukishikiliwa na waasi wa kihuthi kwa zaidi ya miezi minne. Operesheni hiyo iliyopewa jina “Operesheni ya Mshale wa Dhahabu” ni ya kwanza kupata mafanikio makubwa, tangu wanamgambo wa kihuthi walipoingia mji huo wa bandari na kumlazimisha rais Abedrabbo Mansour Hadi kukimbilia nchi jirani ya Saudi Arabia. Rais wa...

Like
277
0
Wednesday, 15 July 2015
KINGUNGE: MCHAKATO WA KUMPATA MGOMBEA URAIS CCM ULIKUWA BATILI
Local News

MWANASIASA Mkongwe na Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi- CCM -Kingunge Ngombale Mwiru ameeleza kusikitishwa kwake na mchakato mzima wa kumpata Mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho kuwa ulikua ni batili na kulikua na ukiukwaji mkubwa wa katiba ya chama hicho. Ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam alipozungumza na Waandishi wa habari, ambapo amesema kwa Mujibu wa Taratibu za Chama hicho Kamati kuu ndio yenye jukumu la kuteua Tano bora katika wanachama wote waliojitokeza kutangaza nia ya kugombea...

Like
237
0
Wednesday, 15 July 2015