Local News

JK AWASILI GENEVA KUENDESHA VIKAO VYA JOPO LINALOCHUNGUZA JINSI DUNIA INAVYOWEZA KUJIKINGA NA MAJANGA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa linalochunguza jinsi dunia inavyoweza kujikinga na majanga ya magonjwa ya milipuko katika miaka ijayo, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete, amewasili mjini  Geneva, Uswisi, kwa ajili ya kuendesha vikao vya Jopo hilo. Vikao hivyo vitakuwa ni awamu ya pili kwa Jopo  ambalo liliteuliwa Mwezi Aprili, mwaka huu, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , Ban Ki Moon. Wajibu mkuu wa Jopo hilo ni kutoa mapendekezo ya kuimarisha mifumo...

Like
314
0
Wednesday, 15 July 2015
VYOMBO VYA HABARI VIMEOMBWA KUTOA TAARIFA SAHIHI ZISIZO NA UPENDELEO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Local News

VYOMBO vya Habari nchini vimeombwa kutoa taarifa sahihi zisizo na upendeleo ili kuepuka uchochezi katika wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu. Akizungumza na kituo hiki Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili nchini Bonaventure Mwalongo amesema kuwa vyombo vya habari ndiyo nguzo muhimu katika kulinda Amani ya nchi kupitia shughuli zao. Amewataka waandishi nchini kuepuka ushabiki na badala yake wawaunganishe watanzania ili wafanye maamuzi sahihi katika uchaguzi mkuu kupitia taarifa sahihi zinazotolewa na vyombo...

Like
245
0
Wednesday, 15 July 2015
NYALANDU ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SINGIDA KASKAZINI
Local News

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amechukua fomu ya kugombea Ubunge katika jimbo la Singida Kaskazini kwa tiketi ya chama cha mapinduzi-CCM. Nyalandu amechukua fomu hiyo ikiwa ni siku ya kwanza kuingia kazini baada ya kutoka kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho. Nyalandu anaimani kwamba akisimama kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo hilo atashinda kwani ana vigezo vyote vinavyostahili kumpa nafasi hiyo lakini pia...

Like
338
0
Wednesday, 15 July 2015
MATHEW YUNGWE ATANGAZA KUGOMBEA UBUNGE BAGAMOYO KWA TIKETI YA CCM
Local News

WAKATI viongozi mbalimbali wakijitokeza kugombea nafasi za uongozi kada wa chama cha mapinduzi Mathew Yungwe ametangaza rasmi nia ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo Bagamoyo kupitia chama cha mapinduzi –CCM-ambalo linaongozwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi dokta Shukuru Kawambwa.   Akizungumza na viongozi na wanachama wa chama hicho mjini Bagamoyo mkoani Pwani Yungwe amesema ameamua kugombea nafasi hiyokwa lengo la kusukuma maendeleo ya jimbo hilo ambayo yamekwama kwa muda mrefu.   Yungwe amesema kuwa mambo...

Like
292
0
Tuesday, 14 July 2015
JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 50 KWA RAIA MWEMA ATAKAYETOA TAARIFA YA UHAKIKA ITAKAYOPELEKEA KUKAMATWA KWA MAJAMBAZI WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA SITAKI SHARI
Local News

JESHI la Polisi nchini limetangaza kutoa zawadi ya shilingi milioni hamsini kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa ya uhakika itakayofanikisha kukamatwa kwa majambazi waliowaua askari na raia pamoja na kuiba  silaha katika kituo cha polisi cha sitaki shari kilichopo Ukonga jijini Dar es salaam. Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamishna wa Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam SULEIMAN KOVA amesema kuwa jeshi la polisi limeona ni muhimu kuwashirikisha wananchi kikamilifu kwa kutoa zawadi hiyo kwa kuwa suala la...

Like
404
0
Tuesday, 14 July 2015
WANAWAKE WATAKIWA KUJITOKEZA KUWANIA NAFASI MBALIMBALI KATIKA VYAMA VYA SIASA
Local News

CHAMA cha Sauti ya Umma kimewataka wanawake wenye uwezo wa uongozi kujitokeza katika kuwania nafasi mbalimbali kwenye vyama vya siasa  na  kuleta uwiano sawa wa  hamsini kwa hamsini katika uongozi hapa nchini ili kuiondoa asilimia 30 iliyopo sasa.   Akizungumza na kituo hiki Katibu Mkuu wa Chama hicho Ally Kaniki amesema kuwa wapo wanawake wenye uwezo mkubwa wa kuongoza lakini wamekuwa nyuma na kushindwa kuthubutu kutokana na uoga na kutokujiamini.   Aidha amewataka wanawake kote nchini kuondoa dhana ya kusubiri...

Like
186
0
Tuesday, 14 July 2015
MAGUFULI KUZUNGUMZA NA WANANCHI DSM LEO
Local News

MGOMBEA wa Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi-CCM-dokta John Magufuli anatarajiwa kuwahutubia wananchi wa mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kutambulishwa kwake. Akizungumzia suala hilo katibu wa siasa na Uenezi wa chama hicho Mkoani hapa Juma Simba amesema kuwa dokta Magufuli atawahutubia wananchi katika viwanja vya Mbagala Zakheim, hotuba itakayolenga kuonesha vipaumbele vya chama katika kipindi kijacho cha uongozi. Dokta Magufuli alipitishwa kuwa mgombea wa nafasi hiyo kupitia –ccm- baada...

Like
210
0
Tuesday, 14 July 2015
WANANCHI WAIPONGEZA CCM KWA KUPATA MGOMBEA WAKE
Local News

BAADHI ya Wananchi wamekipongeza Chama cha Mapinduzi -CCM- kwa Kumpitisha Dokta John Magufuli kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya Tano kwa tiketi ya chama hicho. Wakizungumza na EFM kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema Chama hicho  kimewapatia Watanzania aina ya Mtu ambae wamekua wakimhitaji kwa kipindi kirefu kwani Watanzania wanahitaji mtu mwenye ujasiri mkubwa wa kutoa maamuzi kama alivyo Dokta Magufuli kwani mara nyingi amekua akichukua maamuzi magumu katika utendaji wake...

Like
224
0
Monday, 13 July 2015
7 WAPOTEZA MAISHA BAADA YA WATU WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI KUVAMIA KITUO CHA POLISI CHA STAKISHARI
Local News

JUMLA ya watu saba wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ambao wamevamia kituo cha polisi cha Stakishari usiku wa kuamkia leo kilichopo ukonga jijini Dar es salaam. Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini –IGP-ERNEST MANGU amesema kuwa miongoni mwa watu waliouawa ni Askari 4 na raia 3 ambapo kati ya raia hao watatu waliouawa mmojawapo ni jambazi. IGP Mangu amebainisha kwamba watu wengine watatu waliokuwa katika eneo...

Like
443
0
Monday, 13 July 2015
WAZAZI WATATUA TATIZO LA UKOSEFU WA MATUNDU YA VYOO SHULENI IRINGA
Local News

WAZAZI wa wanafunzi wanaosoma shule za msingi Mgongo na Kigonzile, Kata ya Nduli manispaa ya Iringa wamefanikiwa kutatua tatizo la ukosefu wa matundu ya vyoo lililokuwa linawasumbua kwa kipindi kirefu.   Wakizungumza na kituo hiki wazazi hao wamesema kwa kipindi kirefu shule hizo zilikuwa zikikabiliwa na uhaba mkubwa wa matundu ya vyoo jambo ambalo lingeweza kusababisha magonjwa ya mliuko.   Naye diwani wa kata hiyo Bashir Mtove amesema kutokana na tatizo hilo kukithiri shuleni hapo mikakati mbalimbali imetumika ikiwemo...

Like
261
0
Monday, 13 July 2015
TRA KUKUSANYA KODI KUFIKIA MALENGO YA KUIWEZESHA SERIKALI
Local News

MAMLAKA ya mapato Tanzania –TRA– imedhamiria kufikia malengo yake katika ukusanyaji wa kodi ili kuiwezesha serikali kufikia shilingi trilioni 22.3 iliyojiwekea katika bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016.   Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  Rished Bade wakati wa Semina ya wahasibu iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi –NBAA– kwa lengo la kujadili kuhusu masuala ya kodi, bajeti na uchumi kwa ujumla.   Naye...

Like
455
0
Monday, 13 July 2015