MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka-DAWASO imeanzisha mfumo mpya wa kutuma na kulipia bili za maji kwa njia ya simu ili kurahisisha huduma za ulipiaji maji kwa wananchi. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Kaimu Meneja Uhusiano DAWASCO, EVERLASTING LYARO amesema kuwa kwa sasa huduma hiyo inapatakana katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Bagamoyo lakini pia ni maalum kwa watu wa...
KATIKA kuhakikisha huduma za afya ya uzazi zinawafikia akina mama na vijana waishio pembezoni mwa miji na Vijijini, Chama cha Uzazi na Malezi – UMATI, kimeanza kuendesha huduma mkoba itakayowarahisishia watu wa makundi hayo kufikiwa na huduma kiurahisi katika makazi yao. Akizungumza na EFM Mkurugenzi wa -UMATI- Lulu Mwanakilala amesema katika huduma Mkoba Wataalamu wa afya watawafata akina mama na Vijana katika makazi yao wakiwa na vifaa vyote vya kutolea huduma za afya ya uzazi kwa lengo la kuwapunguzia safari...
SERIKALI imeridhia kuanzishwa kwa baadhi ya wilaya na mikoa mipya kwa lengo la kusogeza karibu huduma muhimu kwa wananchi ili kuleta manufaa kwa Taifa. Akizungumza wakati akitoa hoja ya kuahirisha kikao cha bunge Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Mizengo Pinda amezitaja baadhi ya wilaya mpya kuwa ni Ubungo na Kigamboni za Jijini Dar es salaam. Waziri Pinda amesema kwamba mpango huo wa kuongeza wilaya na mikoa mipya utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha utendaji wa shughuli...
WATANZANIA wameshauriwa kutumia vyema elimu na ushauri unaotolewa na wataalam mbalimbali juu ya matumizi bora ya lishe ili kupunguza hali ya udumavu kwa watoto wanaozaliwa nchini. Hayo yamesemwa leo bungeni mjini Dodoma na Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii mheshimiwa Kebwe Steven Kebwe wakati akijibu maswali kutoka kwa baadhi ya wabunge yaliyoelekezwa katika wizara hiyo kuhusu ushiriki wa serikali katika kupunguza tatizo la udumavu. Mheshimiwa Kebwe amesema kuwa kwa kiasi kikubwa serikali inashiriki katika kuhakikisha kila mwananchi...
BODI ya utalii nchini imesema inatarajia kufanya maonyesho ya utalii Jiji Dar es salaam ambayo yanategemea kuanza mapema mwezi wa kumi mwaka huu . Akizungumza na Kituo hiki, Kaimu Mkurugenzi mwendeshaji bodi ya utalii Tanzania DEVOTHA MDACHI amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya maonyesho ya utalii ya meshaanza na bodi inategemea kupokea mawakala wa utalii zaidi ya 50 na wanahabari wasiopungua 10 kutoka Mataifa mbali mbali. Amebainisha kuwa, maonyesho hayo ni nafasi kubwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kutangaza kazi zao...
KAMATI Kuu ya chama cha Mapinduzi-CCM, leo inatarajiwa kufanya Zoezi la uchujaji wa majina ya watu waliotangaza nia ya kugombea nafasi ya urais ndani ya Chama hicho ambapo inatarajiwa leo itatoa majina ya wagombea watano. CCM inatakiwa kupitisha jina moja la mtu atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa wabunge na rais unaotarajiwa kufanyika tarehe 25 Oktoba mwaka 2015. Hapo kesho, Halmashauri kuu ya chama itakutana ambapo itachuja majina hayo matano hadi kufikia matatu kupitia mtindo wa kupiga...
VIJANA nchini wametakiwa kuacha kutumiwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa katika kuvuruga Amani ya nchi hususani katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Wakizungumza na kituo hiki waathirika wa dawa za kulevya ambao tayari wameacha matumizi ya dawa hizo wamesema kuwa viongozi wengi wamekuwa wakiwafuata na kuwapa fedha kwa ajili ya kuwalazimisha kuwapigia kura ili wapate nafasi wanazozihitaji. Aidha wamesema kuwa ni vema vijana kujitambua ili kuepukana na vitendo hivyo kwani viongozi hao wanawatumia wakati...
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limewasilisha bungeni muswada wa sheria ya tume ya walimu wa mwaka 2015 wenye lengo la kuboresha huduma za walimu nchini. Akisoma muswada huo kwa mara ya pili bungeni mjini Dodoma Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi mheshimiwa Shukuru Kawambwa amesema kuwa lengo kuu la muswada huo ni kutunga sheria ya usimamizi wa masuala muhimu ya walimu ili kuleta manufaa zaidi. Waziri Kawambwa amebainisha kuwa muswada huo utarahisisha pia uwajibikaji kwa walimu...
IMEELEZWA kuwa zaidi ya ajira elf 16 zinatarajiwa kuzalishwa kutokana na kuanzishwa kwa shughuli za ujenzi wa mitambo ya mafuta na gesi nchini Tanzania. Akizungumza na kituo hiki Jijini Dar es salaam Mkufunzi wa umeme kutoka chuo cha –VETA– mkoani Lindi MAJEO MGOE amesema shughuli hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza Ajira hususani kwa wahitimu wa chuo hicho. Magoe ameongeza kuwa mafunzo wanayopata wanafunzi kutoka katika chuo hicho yamewasaidia vijana kuongeza sifa za kuajiriwa hali ambayo inawawakwamua...
WIZARA ya Nishati na Madini nchini imewahakikishia wananchi wa jimbo la Nkasi kuwa ipo tayari kusimamia vyema suala la ujenzi wa mradi usambazaji wa umeme katika kipindi kifupi kijacho. Ahadi hiyo imetolewa leo Bungeni na Naibu waziri wa wizara hiyo mheshimiwa CHARLES MWIJAGE wakati akijibu swali la mheshimiwa ALLY KESSY aliyetaka kufahamu mikakati ya serikali juu ya utekelezaji wa suala hilo. Mheshimiwa Mwijage amesema kuwa ili kuhakikisha mradi huo unakamilika mapema serikali imejipanga kuwatumia wataalamu wazawa katika kukamilisha...
SERIKALI imeombwa kuona umuhimu wa kutafuta njia mbadala ya kuhakikisha inapunguza foleni katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kuruhusu maeneo ya bandari kavu kutumika kama barabara kuu ya kupitishia maroli ya mizigo. Ombi hilo limetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Amani Mkowa wa Dar es Salaam ALPHONCE TEMBA wakati akizungumza na kituo hiki juu ya namna ya kupunguza msongamano wa magari ya mizigo yanayosababisha foleni barabarani. Amesema kuwa maeneo kama Chalinze, Ruvu kigwaza na Mlandizi yanaweza...