MKURUGENZI wa Taasisi ya Takwimu nchini dokta Albina Chuwa amesema kuwa suala la takwimu zinazohusu hali ya mazingira, ikiwemo uharibifu unaotokana na uchafuzi wa maji, hewa chafu na kupotea kwa uoto wa asili bado ni ngeni katika nchi zinazoendelea, hususan za bara la Afrika. Dokta Chuwa ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya takwimu za hali ya mazingira kwa nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki jijini Arusha uliohudhuriwa na viongozi wa Takwimu wa nchi hizo. Amesema kuwa mafunzo...
WATANZANIA wametakiwa kutofanya makosa katika uchaguzi mkuu ujao kwa kuchagua wabunge watakaoweza kuhimili changamoto na kujenga hoja katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Rai hiyo imetolewa leo na Naibu katibu Mkuu wa Chama cha-Alliance For Democratic Change–ADC– Doyyo Hassan Doyyo wakati akizungumza na EFM juu ya sakata la wabunge wa Upinzani kutoka nje ya Bunge kwa kupinga miswada iliyowasilishwa bungeni kwa hati ya dharula. Aidha amesema kuwa kutokana na umuhimu wa miswada...
TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini-NEC-imetoa wito kwa wananchi wote wa Mikoa ya Pwani kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili wapate haki yao ya kupiga Kura na kuchagua Viongozi bora katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Tume hiyo imeeleza kwamba uboreshaji wa daftari hilo kwa mkoa wa Pwani unaanza leo hadi julai 20 mwaka huu kabla ya kuanza mkoa wa Dar es salaam. Mbali na kutoa ratiba...
Kutana na Debora charles mkazi wa kinondoni mkwajuni ambae ni mshindi wa shindano la sakasaka Wilaya ya Kinondoni aliyejibebea kitita cha shilingi milioni moja na nusu za kitanzania kupitia shindano hili lenye msisimko wa kipekee. Hata wewe pia waweza kuwa mshindi na kuweza kubadilisha maisha yako kwakusikiliza efm na kufuata maelekezo. Debora charles ...
BUNGE la Jamhuri ya muungano wa Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi wa mwaka 2015 wenye lengo la kuwezesha nchi kunufaika na mapato yanayotokana na mafuta hayo. Awali akitoa ufafanuzi wa masuala muhimu katika muswada huo, Naibu waziri wa fedha mheshimiwa Mwigulu Nchemba amesema kuwa serikali itahakikisha mapato yote yatokanayo na mafuta yanasaidia katika kuleta maendeleo ya...
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imewahukumi kifungo cha Miaka mitatu jela Mawaziri waandamizi wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona. Hata hivyo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja ameachiwa huru baada ya Mahakama kumwona hana hatia. Viongozi hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni...
KITUO cha Sheria na Haki za binadamu nchini –LHRC– kimeiomba Serikali kutoa elimu ya uraia katika mchakato wa katiba mpya kwa viongozi wa kimila wa mkoa wa Manyara ili waifikishe kwa jamii inayowazunguka. Mwanasheria wa kituo hicho Lengai Merinyo ameyasema hayo wakati akizungumza na jamii ya wafugaji wa kata ya Partimbo wilayani Kiteto juu ya elimu ya uraia kwa mpiga kura kuhusu katiba pendekezwa. Merinyo amesema ili kuwezesha jamii ya mkoa wa Manyara kunufaika na kuuelewa mchakato wa katiba mpya...
SERIKALI imeahidi kushirikiana vyema na sekta binafsi katika masuala ya kuinua utalii wa nchi kwa lengo la kuhakikisha Taifa linaingiza mapato ya kutosha kupitia sekta hiyo. Hayo yamesemwa leo bungeni mjini Dodoma na naibu waziri wa maliasili na utalii mheshimiwa MAHMOUD MGIMWA wakati akijibu swali la mbunge wa Ilala mheshimiwa Mussa Zungu aliyetaka kufahamu mikakati ya serikali juu ya suala hilo. Mheshimiwa Mgimwa amesema kuwa ingawa sekta ya utalii imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi lakini serikali ipo tayari kuhakikisha...
“Argentina haikustahili kushindwa dhidi ya Chile katika mchezo wa fainali za michuano ya Copa America kutokana na timu zote kucheza sawa katika viwango” alisema kocha Gerardo Martino Chile imejishindia taji lake kubwa la kwanza kwakuitandika Argentina kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana ndani ya dakika 120. katika mchezo wa uliochezwa kwa kiwango cha juu na timu hizo lakini kwa mtazamo wake anaona Argentina walistahili kutwaa taji hilo alisema Martino wakati akizungumza na vyombo vya habari...
MKUU wa Mkoa wa Manyara dokta JOEL BENDERA amewataka raia wa nchi za kigeni wa mkoa huo kutojitokeza na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwani atakayebainika atamchukulia hatua kali za kisheria. Mkoa huo unatarajia kufanya zoezi hilo la uandikishaji wa kutumia vifaa vya kielekrtoniki –BVR– kwa mwezi mmoja ambapo wapiga kura takribani laki saba na elfu hamsini wanatajia kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura la mkoa wa Manyara. Dokta Bendera ameyasema hayo wakati alipokuwa akikagua utekelezaji wa...
WABUNGE wameishauri serikali kuweka muda rasmi wa kufanya uchunguzi wa makosa mbalimbali ili kuokoa ucheleweshwaji wa kutoa hukumu kwa watuhumiwa kulingana na makosa. Akichangia maoni yake leo bungeni mjini Dodoma mbunge wa Singida Mashariki mheshimiwa TUNDU LISSU amesema kuwa ni muhimu kwa serikali kuweka kipengele hicho ili kutatua changamoto za ucheleweshwaji wa kesi kutokana na uchunguzi mbovu. Naye mbunge wa ubungo mheshimiwa JOHN MNYIKA amewataka wabunge wa chama tawala kutotumia wingi wao katika kupitisha hoja bila kusikiliza upande wa...