WATANZANIA wameombwa kutunza miradi mbalimbali ya mandeleo inayoletwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau na wananchi wenyewe. Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Juma Chumu alipokuwa akizindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Ilala yenye gharama ya shilingi bilioni 14. Aidha amewataka watanzania kuepuka kutumiwa na wanasiasa ili kusababisha uvunjifu wa amani katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka...
IMEELEZWA kuwa kutokana na kitendo cha rais wa burundi pierre Nkurunziza kung’ang’ania madarakani na kusababisha machafuko ndani ya nchi hiyo, hali hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ongezeko la wakimbizi kutoka burundi Nchini Tanzania kwa kuwa ndiyo nchi jirani iliyopakana na nchi hiyo. Wakizungumza na EFM katika kambi ya muda ya wakimbizi hao iliyopo mjini kigoma katika uwanja wa Lake Tanganyika,wakimbizi hao wameeleza kuwa chama tawala kinachoongozwa na rais Nkurunziza kimekuwa kikitishia hali ya usalama wa...
MTANDAO wa kijinsia Tanazania TGNP umelaani kitendo cha baadhi ya Wabunge wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushindwa kuhudhuria Vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini dodoma huku wakitumia kodi za wananchi waliowachagua bila manufaa yoyote na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam Afisa mawasiliano kutoka TGNP MELCKDEZEL KAROLI amesema kuwa kitendo cha wabunge kutokuwepo ndani ya bunge wakati maamuzi mbalimbali yakiwa yanafanyika ni kuwanyima haki wananchi kwa kuwa wao ndio...
WATANZANIA wameshauriwa kuwa waangalifu na kuacha tabia ya kuiga matumizi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na mamlaka husika kwa kuwa ni hatari kwa Afya zao. Rai hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu waziri wa wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo mheshimiwa JUMA NKAMIA kwa niaba ya Waziri wa Afya, wakati akijibu swali la mheshimiwa RIZIKI JUMA aliyetaka kufahamu jitihada za serikali katika kudhibiti tatizo hilo nchini. Mheshimiwa NKAMIA amesema kuwa ni vyema kwa kila mwananchi kuchukua...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, amemwapisha Katibu Mkuu mpya, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Rutageruka Mulamula. Aidha, katika sherehe fupi ya uapisho iliyofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete amemwapisha Balozi Hassan Simba Yahya kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo. Katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri wa Mambo ya...
WAZIRI wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbaruok amesema ushirikiano katika Nyanja za utalii,utamaduni na michezo ndio njia pekee ya kukuza uhusiano uliopo kati ya Nchi ya Zanzibar na Malawi. Ameyasema hayo wakati alipokutana na Balozi mpya wa Malawi Nchini Tanzania Hawa Ndilowe alipofika ofisini hapo kwa kujitambulisha kwa waziri huyo. Amesema ushirikiano huo utafanya mataifa yao kutembeleana katika Nyanja hizo na kubadilisha mawazo Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk katikati akiwa katika...
WAZIRI wa Uchukuzi mheshimiwa SAMWEL SITTA ameagiza meneja wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini-SUMATRA-mkoa wa Katavi kushughulikia haraka tatizo la utozwaji wa nauli zisizo idhinishwa na mamlaka hiyo katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo. Mheshimiwa SITTA ametoa agizo hilo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Nkasi mheshimiwa ALLY KESSY aliyetaka kufahamu uhalali wa nauli hizo kutoka kwa mamlaka hiyo. Mbali na hayo waziri amesema kuwa ni muhimu kwa Sumatra katika kila...
SHIRIKA la kimataifa la kuhudumia watoto la Save the children leo limewakutanisha watoto pamoja na viongozi wa vyama vya Siasa nchini kwa ajili ya kusikiliza maoni ya watoto hao ili kuingiza katika ilani zao za uchaguzi pamoja na kutoa tamko la watakachofanya baada ya miaka 5 ijayo. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es salaam amesema kuwa kwa sasa wanafanya utaratibu wa kukutana na vyama vya Siasa ambavyo vimeshiriki katika mchakato wa uchaguzi na kuweza kuchukua maeneo 10 ambayo...
WAMILIKI wa vyombo vya habari nchini-MOAT na waandishi wahabri wamelaani muswada mpya wa sheria ya vyombo vya habari uliotaka kuwasilishwa katika kikao cha bunge kilichopita kwa hati ya dharula kwa kuwa baadhi ya vipengele kwenye muswaada huo unapunguza uhuru wa vyombo vya habari. Hata hivyo muswaada huo wenye kasoro nyingi unaonesha kuwa kuna hila chafu za kutaka kupitisha sheria hiyo bila kuhusisha wadau wa tasnia hiyo ili kudhibiti vyombo binafsi na wananchi wasiweze kutoa na kupata taarifa jambo ambalo ni...
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo –Chadema-dokta WILBROAD SLAA amewataka wasimamizi wa daftari la kudumu la wapiga kura kutoa kipaumbele kwa makundi maalum katika jamii ili waweze kujiandikisha bila kupata madhara. Dokta SLAA ameyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Hamugembe wilayani Bukoba ambapo amesema kuwa kitendo cha kuwatengenezea mazingira bora wahusika wa makundi hayo kutarahisishia kutumia nafasi hiyo kutimiza malengo yao ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu. Mbali na...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta JAKAYA KIKWETE amemteua ANTHONY MAVUNDE kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu jijini Dar es salaam imesema kuwa Rais amefanya uhamisho wa wakuu wa Wilaya kumi kwa nia ya kuongeza ufanisi katika uongozi wa Wilaya mbali mbali nchini. Katika mabadiliko hayo amemhamisha Luteni EDWARD OLE LENGA kutoka Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa...