Local News

BUJUMBURA: WAANDAMANAJI WACHOMA MOTO BASI
Local News

BASI  moja limechomwa moto mjini Bujumbura Burundi na waandamanaji waliorejea mabarabarani kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu. Kitongoji cha Kanyosha kimekuwa kitovu cha maandamano hayo dhidi ya awamu ya tatu ya rais Nkurunziza. Maandamano haya yanarejea baada ya kuuawa kwa kiongozi wa chama cha upinzani Zedi Feruzi nje ya nyumba yake katika mji mkuu Bujumbura....

Like
257
0
Monday, 25 May 2015
SIKU YA ALBINO DUNIANI KUADHIMISHWA ARUSHA JUNE 13 KITAIFA
Local News

WAKURUGENZI wa Halmashauri za wilaya  nchini wameombwa kuwagharamia watu wenye ulemavu wa ngozi ili kwenda kushiriki maadhimisho ya siku ya albino kote duniani ambayo kitaifa yatafanyika juni 13 mkoani Arusha ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo juu ya siku ya watu wenye ulemavu wa ngozi, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Kasim Kibwe amesema kuwa maadhimisho hayo yanakusudia kuongeza ufahamu juu ya...

Like
417
0
Monday, 25 May 2015
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YATANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI
Local News

TUME  ya Taifa ya uchaguzi leo imetangaza rasmi ratiba ya uchaguzi mkuu kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa kikatiba. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na mwenyeki wa tume hiyo jaji mstaafu DAMIAN LUBUVA imesema kuwa uteuzi wa wagombea katika vyama kwa ngazi ya urais, ubunge na udiwani utafanyika Agosti 21 mwaka...

Like
222
0
Monday, 25 May 2015
WABUNGE WA VITI MAALUM WATAKIWA KUELEKEZA NGUVU KUGOMBEA NAFASI ZA UBUNGE MAJIMBONI
Local News

WABUNGE wa Viti maalum Nchini wametakiwa kuelekeza Nguvu katika kugombea nafasi za ubunge Majimboni kama ilivyo kwa wanaume badala ya kuendelea kutegemea kupata nafasi hiyo kwa kuteuliwa. Wito huo umetolewa na Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoani Singida CHRISTOWAJA MTINDA wakati akizungumza na EFM ambapo amesema wakati wa Wanawake kusubiri kuteuliwa umepitwa na wakati hivyo ni vyema kufanya jitihada za kutosha kuwatumikia wananchi. MTINDA amesema Umefika wakati ambapo wanawake wanapaswa kuonyesha kwa vitendo kuwa wanaweza kupitia kugombea nafasi...

Like
480
0
Monday, 25 May 2015
SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA ZA MABASI YAENDAYO KASI NA FLYOVER
Local News

SERIKALI imeahidi kuendelea kuchukua jitihada za kutosha katika kuhakikisha inakamilisha miradi ya ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo kasi na za flyover ili kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es salaam. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Ujenzi dokta JOHN MAGUFULI wakati akijibu swali la mbunge wa kinondoni mheshimiwa IDD AZZAN aliyetaka kufahamu mikakati ya serikali katika kutekeleza miradi hiyo. Waziri MAGUFULI amesema kuwa jitihada za kufanikisha miradi hiyo zinaendelea kuchukuliwa  ambapo hadi sasa kuna...

Like
249
0
Monday, 25 May 2015
SHEREHE ZA KUMBUKUMBU YA WIKI YA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA ZAANZA LEO
Local News

SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la umoja wa Mataifa-UNESCO– kwa kushirikiana na wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo nchini wameungana kuongoza sherehe za wiki ya kumbukumbu ya wiki ya ukombozi wa bara la Afrika zinazoanza leo hadi mei 29 mwaka huu maeneo mbalimbali ya Afrika. Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika hilo sherehe hiyo hufanyika kila ifikapo mei 25 ya kila mwaka ndani na nje ya bara la Afrika kukumbuka siku ambayo viongozi wa bara hilo walipokutana mwaka...

1
267
0
Monday, 25 May 2015
SERIKALI YASHAURIWA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA MAHAKAMA
Local News

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya katiba, sheria na utawala bora imeishauri serikali kuwajengea uwezo watumishi wa mahakama pamoja na kuwapatia mahitaji yote muhimu ikiwemo vitendea kazi bora ili kufanikisha utendaji wao wa kazi. Ushauri huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mbunge wa Bukoba mheshimwa JASSON RWEIKIZA ambapo amesema kuwa uwekezaji wa kutosha katika sekta hiyo ya mahakama ni muhimu kwa kuwa ni miongoni mwa chombo maalumu cha kuleta haki na usawa...

Like
246
0
Thursday, 21 May 2015
KUBUKUMBU YA MIAKA 19 TANGU KUZAMA KWA MELI YA MV BUKOBA
Local News

TANZANIA leo inakumbuka miaka 19 tangu kutokea kwa ajali  ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba ambayo ilizama siku kama ya leo mwaka 1996 ambapo zaidi ya watu elfu moja walipoteza maisha yao. Tangu kuzama kwa meli ya Mv Bukoba limebaki kuwa tukio la kihistoria ambalo athari zake ziko wazi kwa mamia ya familia waliopoteza ndugu na wategemezi wao. Inakadiliwa zaidi ya watu 1000 walikufa kutokana na Meli hiyo kudaiwa kuwa ilijaza kuzidi uwezo...

Like
430
0
Thursday, 21 May 2015
CHADEMA: UFISADI UNALITAFUNA TAIFA NA KUWAFANYA WANANCHI WAZIDI KUWA MASIKINI
Local News

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, kimesema ripoti za CAG ambazo zimeanika ufisadi katika maeneo yaliyokaguliwa ikiwemo  Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, mashirika ya umma na miradi ya maendeleo, kwa mara nyingine zimedhihirisha wazi kile ambacho CHADEMA imekuwa ikisema kwa muda mrefu kwamba ufisadi huo unaoendelea kulitafuna taifa na kuwafanya Watanzania wazidi kuwa maskini.   Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na chama hicho kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumaini Makene, Chadema kimepokea kwa masikitiko...

Like
201
0
Thursday, 21 May 2015
JAMII YATAKIWA KUFUATILIA KWA UMAKINI ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Local News

JAMII imetakiwa kufuatilia kwa makini zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na kushiriki ipasavyo kutoa taarifa kwa vyombo husika endapo itagundua kasoro yoyote katika zoezi hilo ili hatua stahiki zichukuliwe. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri Mkuu mheshimiwa MIZENGO PINDA wakati akijibu swali la mbunge wa Mkanyageni mheshimiwa MOHAMED MNYAA juu ya uwepo wa uandikishaji wa watu wasiohusika kupiga kura hususani Zanzibar katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo. Waziri PINDA amesema...

Like
233
0
Thursday, 21 May 2015
WATANZANIA WAMETAKIWA KUEPUKA KUANDIKA AU KUTAJA TAKWIMU ZISIZO RASMI
Local News

WATANZANIA wametakiwa kuepuka  kuandika au kutaja takwimu zisizo rasmi kwani vitendo hivyo ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria mpya ya takwimu ya mwaka 2015. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu ofisi ya Takwimu Dokta Albina Chuwa amesema takwimu bora husaidia serikali yoyote duniani kupanga mipango ya maendeleo ya wananchi wake hivyo ni bora kuwekwa kwa chombo maalum kinachotoa takwimu kama ilivyo kwa ofisi ya Taifa ya Takwimu. Ameeleza kuwa ni vyema takwimu...

Like
247
0
Wednesday, 20 May 2015