Local News

WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI YAWASILISHA MAKADILIO YA MATUMIZI YAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2015 HADI 2016
Local News

WIZARA ya maendeleo ya mifugo na uvuvi nchini imewasilisha rasmi makadilio ya matumizi yake katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015 hadi 2016 yanayokadiliwa kuwa ni zaidi ya bilioni 68 kwa lengo la kuboresha na kuimarisha utendaji kazi kwa maendeleo ya Taifa.   Akiwasilisha makadilio hayo Waziri wa wizara hiyo dokta TITUS KAMAN amesema kuwa endapo fedha hizo zitapitishwa, zitaisaidia Wizara katika utekelezaji wa shughuli muhimu kwa kipindi cha mwaka mzima  kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi....

Like
333
0
Wednesday, 20 May 2015
SERIKALI KUSHIRIKIANA NA UNESCO KUADHIMISHA WIKI YA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA
Local News

SERIKALI ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni- UNESCO inatarajia kuadhimisha wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika Mei 25 hadi 29 mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Assah Mwambene ,amesema maadhimisho hayo yanatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe. Katika ufunguzi huo, Mwambene ameeleza kuwa maadhimisho hayo yatatanguliwa...

Like
296
0
Wednesday, 20 May 2015
WABUNGE WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KUHAMASISHA WANANCHI KUCHANGIA UJENZI WA VITUO VYA POLISI
Local News

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya nchi imewataka wabunge kushirikiana vyema na wizara hiyo katika kuhakikisha wanatoa hamasa kwa wananchi ili wapate mwamko wa kuchangia ujenzi wa vituo vya polisi katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuimarisha usalama. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu waziri wa wizara hiyo mheshimiwa PEREIRA SILIMA wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu jimbo la Mbeya dokta MARY MWANJELWA aliyetaka kufahamu jitihada za ujenzi wa kituo cha polisi cha Ilembo mkoani humo....

Like
196
0
Wednesday, 20 May 2015
AFRIKA KUIMARISHA UTAWALA BORA UNAOZINGATIA UWAJIBIKAJI NA UWAZI
Local News

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania dokta JAKAYA KIKWETE anafungua mkutano wa Kanda ya Afrika kuhusu Mpango wa Uendeshaji wa  Shughuli za Serikali kwa uwazi –OGP. Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano  Ikulu inaeleza kuwa mkutano huo wenye kauli mbiu isemayo “Kuimarisha Utawala Bora Unaozingatia Uwajibikaji na Uwazi” unafunguliwa leo na kuhitimishwa kesho mei 21,  katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Lengo la mkutano huo ni kuleta ufanisi katika utekelezaji wa masuala...

Like
187
0
Wednesday, 20 May 2015
INTER MILAN YATANGAZA DAU KUMNYAKA YAYA TOURE
Local News

Klabu ya soka ya Inter Milan imetangaza kumuwania kiungo wa Manchester United Yaya Toure kwa kitita cha pound milioni 15 katika kipindi cha miaka mitatu. Inter imepanga kumpatia kiungo huyo pound milioni 4.3 baada ya makato ya kodi katika mshahara. Toure mwenye miaka 31 anatarajiwa kuthibitisha mpango wake wa kuondoka kwenye klabu ya Manchester City mapema wiki ijayo kwenye tamati ya msimu wa ligi Klabu ya Manchester City kwa upande wake imesisitiza kuwa haitasukumwa na uhamisho badala yake inampango wa...

Like
197
0
Wednesday, 20 May 2015
NHC YASHIRIKIANA NA CELCOM KUZINDUA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA KWA NJIA YA SIMU
Local News

SHIRIKA  la Nyumba la Taifa-NHC–  kwa kushirikiana na kampuni ya CELCOM limezindua kituo cha Huduma kwa wateja kwa njia ya simu na malipo ya kodi kwa mfumo wa simu za mkononi. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo NEHEMIA MCHECHU amesema kuwa kituo hicho kitasaidia kufikisha huduma kirahisi kwa wateja wao kwa kupiga simu ambayo haitatozwa  kiasi chochote cha fedha. MCHECHU ameongeza kuwa huduma hiyo pia itasaidia uwajibikaji kwani mitambo iliyofungwa inasafirisha...

Like
304
0
Tuesday, 19 May 2015
JK ATARAJIWA KUFUNGUA MKUTANO WA KANDA YA AFRIKA WA UENDESHAJI WA SHUGURI ZA SERIKALI KWA UWAZI
Local News

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania dokta JAKAYA KIKWETE anatarajia kufungua mkutano wa Kanda ya Afrika kuhusu Mpango wa Uendeshaji wa  Shughuli za Serikali kwa uwazi –OGP. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu inaeleza kuwa mkutano huo wenye kauli mbiu isemayo “Kuimarisha Utawala Bora Unaozingatia Uwajibikaji na Uwazi” utafanyika Mei 20 hadi 21 katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.   Aidha taarifa imeeleza kuwa dhumuni la  mkutano huo ni kuleta ufanisi katika utekelezaji wa...

Like
194
0
Tuesday, 19 May 2015
RAIS WA MSUMBIJI AAHIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO ULIOPO KATI YA NCHI HIZI MBILI
Local News

RAIS wa Msumbiji mheshimiwa FILIPE NYUSSI ameahidi kuendeleza na kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji ili kuleta manufaa ya kutosha kwa wananchi wan chi hizo mbili. Rais NYUSSI ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akiwahutubia wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni hatua ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu aliyoifanya nchini tangu mei 17 mwaka huu. Mbali na hayo mheshimiwa NYUSSI amewaasa watanzania kuilinda na kuiendeleza amani iliyopo kwa kuwa ni hazina...

Like
164
0
Tuesday, 19 May 2015
HONGERA DAVIDO KWAKUPATA MTOTO
Local News

Star wa muziki kutokea Nigerian Davido amebahatika kumpokea mtoto wa kike baada ya mpenzi wake Sophie Momodu kujifungua mtoto wa kike siku kadhaa zilizopita Idadi ya mastar wa Afrika wanaotarajia kupata watoto inazidi kuongezeka ambapo mbali na Diamond kutoka Tanzania, Tiwa Savage kutokea Nigeria pia amefanya baby shower ikiwa ni maandalizi ya kumpoea mtoto wake Sherehe hiyo ilihudhuriwa na marafiki wa karibu wa msanii huyo akiwemo Elohor Aisien  ambae baadae alishea taarifa hizo kwenye ukurasa wake wa instagram na kuweka...

Like
235
0
Tuesday, 19 May 2015
UKOSEFU WA TAKWIMU SAHIHI UNACHANGIA KUKWAMISHA MIPANGO YA KIMAENDELEO NCHINI
Local News

UKOSEFU wa Takwimu sahihi katika Masuala mbalimbali umeelezwa kuchangia kutopiga hatua kwenye mipango ya Kimaendeleo inayopangwa na Serikali juu ya Wananchi. Aidha upotoshaji wa Takwimu hizo unaofanywa na baadhi ya Watendaji kwa kutaka kujinufaisha wao wenyewe, pia umekuwa ukichangia kuchelewa hatua za Kimaendeleo. Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Zanzibar, AMINA SHAABAN,wakati akifungua Semina ya siku moja ya kujadili Malengo ya Millenia baada ya 2015 iliyofanyika mjini hapa. Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia...

Like
308
0
Tuesday, 19 May 2015
MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI YASHAURIWA KUWA MAKINI NA UJENZI UNAOENDELEA KATIKA KIWANJA CHA KIMATAIFA CHA JULIUS NYERERE
Local News

UONGOZI wa Mamlaka za Viwanja vya Ndege Tanzania wameshauriwa kuwa makini katika Ujenzi unaoendelea wa Jengo la kutua na Kupaa Ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere -JNIA. Ujenzi huo unaotarajiwa kuongeza uwezo wa Uwanja wa mara tatu zaidi umejikita katika sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya abiria kupumzika, sehemu ya abiria kupanda na kushuka kwenye ndege, Ofisi za Uhamiaji na huduma nyingine muhimu. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo SULEIMAN  SULEIMAN amesema Kiwanja cha Kimataifa cha...

Like
276
0
Tuesday, 19 May 2015