Local News

BAADHI YA WAGOMBEA WALIOTANGAZA NIA YA KUWANIA UBUNGE ARUSHA WAPIGANA VIKUMBO
Local News

BAADHI ya Wagombea waliotangaza nia kuwania Ubunge katika majimbo mbalimbali mkoani Arusha  kupitia CCM,walionekana kupigana vikumbo na wengine wakijinadi mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli EDWARD LOWASSA. LOWASSA,ambaye anatajwa kuwania Urais kupitia CCM mwaka huu aliendesha harambee ya Ujenzi wa Msikiti wa Patandi uliopo Wilayani Arumeru mkoani Arusha,akimwakilisha makanu wa Rais,Dokta MOHAMMED BILLAL na kufanikiwa kukusanya zaidi ya Shilingi Milioni 200 ikiwa ni zaidi ya makisio ya Msikiti huo. Baadhi ya Watia Nia...

Like
383
0
Tuesday, 19 May 2015
SERIKALI YAWAASA VIJANA KUJIEPUSHA NA NGONO ZEMBE PAMOJA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA
Local News

SERIKALI imewaasa vijana kujiepusha na ngono zembe ikiwa ni pamoja na kujiepusha na matumizi ya  dawa zakulevya ili waweze kujiletea maendeleo yao na kujiinua kiuchumi. Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa mafunzo elekezi ya jinsi ya kujikwamua kiuchumi kwa vijana  wa halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Amesema vijana kujihusisha na ngono Zembe na Matumizi ya Dawa za kulevya kutawafanya kuwa dhaifu na kushindwa kuchangia katika Ujenzi wa taifa...

Like
868
0
Tuesday, 19 May 2015
OFISI ZA UMMA ZABAINIKA KUWA NA UBADHIRIFU WA FEDHA
Local News

MAMLAKA ya udhibiti na manunuzi ya Umma nchini PPRA imesema kuwa ndani ya kipindi cha miaka 10 imebaini kuwa katika ofisi nyingi za Umma kumekuwepo ubadhirifu mkubwa wa fedha kwenye masuala mbalimbali yanayohusiana na ununuzi. Hayo yamebainishwa leo Jijini  Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Doroth Mwanyika wakati wa ufunguzi wa semina  iliyoandaliwa na PPRA yenye lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari nchini kuandika habari zinazohusu manunuzi ya umma. Amebainisha kuwa katika kipindi ambacho taasisi...

Like
337
0
Monday, 18 May 2015
SERIKALI YASHAURIWA KUIWEZESHA TAKUKURU
Local News

KAMATI ya Bunge ya katiba, sheria na Utawala bora imeishauri serikali kuiwezesha Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini-Takukuru-kwa kuipatia nyenzo imara ili kufanikisha shughuli muhimu hususani katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na mwenyekiti wa kamati hiyo JASSON RWEIKIZA wakati akitoa maoni ya kamati juu ya mapendekezo ya bajeti ya ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma, utawala bora, uhusiano na uratibu ambapo amesema kuwa uwezeshaji wa kutosha wa...

Like
204
0
Monday, 18 May 2015
RAIS FILIPE NYUSSI AKUTANA NA RAIA WA MSUMBIJI WAISHIO TANZANIA
Local News

RAIS wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe  Nyussi ameendelea na ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania ambapo leo amekutana na Raia wa Msumbiji waishio nchini nakufanya nao mazungumzo juu ya masuala mbalimbali ya kisiasa, uchumi na kijamii. Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo, Mheshimiwa Filipe  Nyussi amesema Msumbiji na Tanzania ni ndugu wa karibu wa muda mrefu tokea enzi za mapambano ya uhuru wa nchi hiyo ambapo Tanzania iliwasaidia kikamilifu katika harakati za kudai uhuru wao. Mheshimiwa...

Like
248
0
Monday, 18 May 2015
VYOMBO VYA HABARI NCHINI VIMETAKIWA KUACHA MZAHA KUEPUSHA MACHAFUKO KAMA YA BURUNDI
Local News

VYOMBO vya Habari nchini vimetakiwa kuacha mzaha na kufanya kazi zake kisawasawa na kuboresha Demokrasia ili nchi isiingie katika machafuko kama yaliyotokea Burundi hivi karibuni. Imeelezwa kuwa Vyombo vya Habari vinao wajibu mkubwa wa kusimamia Demokrasia na kuhakikisha hali za Binadamu zinazingatiwa ili viweze kutekeleza majukumu yake. Hayo yamebainishwa na Mhadhiri wa Shule ya Uandishi wa Habari ya Chuo Kikuu cha Dar es salaa,Dokta AYOUB RIOBA,baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Saba wa wamiliki wa Vyombo vya Habari wa Nchi...

Like
248
0
Monday, 18 May 2015
AGIZO LA RAIS KUFANYIWA KAZI DAR
Local News

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, SAID MECKY SADICK kwa kushirikiana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, YUSUPH MWENDA wameanza kutekeleza agizo lililotolewa na Rais JAKAYA KIKWETE la kuondoa maji katika makazi ya watu kwenye maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo yaliyosababishwa na mvua zilizokuwa zikinyesha jijini hivi karibuni. Rais KIKWETE alitoa agizo hilo wiki iliyopita wakati alipofanya ziara katika maeneo ya Namanga, Nyaishozi, Dawasco na Basihaya kuangalia athari za mafuriko zilizosabaisha wananchi kuyakimbia makazi yao. Akizungumza wakati wa...

Like
205
0
Monday, 18 May 2015
SERIKALI YAOMBWA KUONGEZA WATAALAMU WA KUPANGA MADARAJA YA TUMBAKU
Local News

SERIKALI imeombwa kuongeza wataalamu wa kupanga madaraja ya Tumbaku ili kuwawezesha wakulima kupata bei nzuri kwenye soko la zao hilo. Pia imeombwa kutafuta wawekezaji wengine na masoko nchini China,baadala ya kutegemea kampuni tatu zinazonunua Tumbaku mkoani Tabora,jambo ambalo litawasaidia wakulima kupata soko la uhakika. Ombi hilo imetolewa na Mbunge wa Viti maalumMkoa wa Tabora,MAGRETH SITTA,alipokuwa akichangia makadirio ya Ofisi ya Waziri Mkuu,ambapo amesema zao hiloni muhimu kwa kuwa linaiingizia serikali asilimia 50 ya mapatoya fedha...

Like
440
0
Monday, 18 May 2015
AJALI MBILI ZA TRENI ZAPELEKEA KUSITISHWA KWA SAFARI YA TRENI YA DELUXE
Local News

AJALI mbili za Treni katika Stesheni za Ngeta mkoani Pwani na Kinguruwila mkoani Morogoro,zimesababisha kusitishwa kwa safari ya treni ya Deluxe. Pia,huduma za usafiri huo kwa wakazi wa Dar es salaam,hazitakuwepo kutokana na kutowasili kwa Vichwa viwili vya Treni baada ya njia za reli kuharibika Vichwa hivyo vilikuwa katika ukarabati wa kawaida kwenye karakana mkoani Morogoro,huku ajali hizo zikitokana na kuanguka kwa mabehewa matano wakati treni zote mbili stesheni hizo zilipokuwa safarini kuelekea mikoa ya...

Like
284
0
Monday, 18 May 2015
WATANZANIA WATAKIWA KUTOYUMBISHWA NA MISIMAMO  YA WANASIASA
Local News

WATANZANIA wametakiwa kutoyumbishwa na misimamo mbalimbali ya viongozi wa kisiasa na badala yake waendelee kuwa na imani na serikali yao kwakuwa imejidhatiti katika kusimamia maslahi ya Taifa. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Mbunge wa jimbo la Sengerema mheshimiwa WILLIAM NGELEJA wakati akichangia hoja ya Bajeti ya ofisi ya Waziri mkuu na kusema kuwa serikali imedhamiria kuboresha mipango mbalimbali itakayosaidia kuleta maslahi kwa kila...

Like
335
0
Friday, 15 May 2015
TGNP: VITUO VYA TAARIFA VIMESAIDIA KUFICHUA MAMBO YALIYOJIFICHA NA KUYAFANYIA KAZI
Local News

MTANDAO wa jinsia Tanzania TGNP umesema kuwa kuwepo kwa vituo vya taarifa na Maarifa katika vijiji na sehemu mbalimbali nchini, kumeweza kusaidia kuleta mabadiliko kwa kufichua mambo  yaliyojificha na kuyafanyia kazi. Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mtandao wa TGNP LILIAN LIUNDI amesema kuwa, kama Serikali za Vijijini ,Kata na Mitaa vitaona umuhimu wa kutoa vipaumbele, vituo hivyo wataweza kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hasa wa Vijijini. LIUNDI amewaomba Viongozi wa Serikali za Mitaa kutoa ushirikiano kwenye...

Like
285
0
Wednesday, 22 April 2015