Local News

MASABURI AWACHAMBUA WATU WANAOJIPITISHA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI
Local News

MWENYEKITI  wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania-ALAT na Meya wa jiji la Dar es salaam,Dokta DIDAS MASABURI,amewachambua watu mbalimbali wanaojipitisha kugombea nafasi mbalimbali za uongozi,ikiwemo ya Urais. Dokta MASABURI amewataka Watanzania hasa vijana kuwa macho na watu wanaojipitisha mtaani na kujiita wao wagombea,huku akifafanua hivi sasa kuna wagombea na wale wanaoupapatikia uongozi nchini. Mwenyekiti huyo  ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa Baraza la Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi-UVCCM,Kata ya Sandal,ambapo...

Like
268
0
Monday, 20 April 2015
MAWAZIRI WA FEDHA WAWEKA MISIMAMO YAO JUU YA SERA ZINAZOWEKWA NA BENKI YA DUNIA
Local News

WAKATI Mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Kifedha la Kimataifa ikiendelea Mjini Washington DC,Mawaziri wa Fedha wameweka misimamo yao juu ya sera ambazo zinawekwa na Benki ya Dunia. Akizungumza na Vyombo vya Habari,Waziri wa Fedha wa Tanzania SAADA SALUM MKUYA, amesema wao kama nchi wamewasilisha walichoona katika utekelezaji wa mipango ya Benki. Amesema wanaishukuru sana Benki ya Dunia kwa kuendeleza mipango ya kuweza kusaidia nchi za Kiafrika ,hususan kwenye mipango ya kujenga Miundo Mbinu ya Kiuchumi kama vile...

Like
218
0
Monday, 20 April 2015
TAMWA YAMPONGEZA DOKTA BILAL
Local News

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania-TAMWA, kimempongeza Makamu wa Rais Dokta MOHAMED BILAL,kwa kutambua umuhimu wa kuchangia Elimu ya Mtoto wa Kike kwa kuchangia Shilingi Milioni 10. Dokta BILAL amekuwa mfano wa kuigwa kutokana na mchango wake wa Shilingi Milioni 10 ili kuwarejesha shule watoto ambao wazazi wao wameshindwa kuwagharamia  masomo na kupambana na unyanyasajiwa jinsia. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA,VALERIA MSOKA,ameeleza hayo katika taarifa yake kwa Vyombo vya...

Like
242
0
Monday, 20 April 2015
CHADEMA YAITAKA SERIKALI KUONGEZA NGUVU KUPAMBANA NA AJALI
Local News

CHAMA cha Demokrasia na maendeleo -CHADEMA- Kimeitaka Serikali kuongeza nguvu ya Kupambana na Ajali za Barabarani kama ilivyo katika vita dhidi ya Mauaji ya Walemavu wa Ngozi kwani ajali zimekuwa na mchango mkubwa wa kumaliza nguvu kazi ya Taifa kila siku. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho kwa Upande wa Bara John Mnyika amesema badala ya Serikali kuwa ni sehemu ya kutuma salamu za rambirambi pindi ajali zinapotokea ni vyema...

Like
241
0
Wednesday, 15 April 2015
BASI LA AIR JORDAN LAPATA AJALI MTU MMOJA AFARIKI DUNIA
Local News

MTU mmoja amefariki Dunia, na wengine ishirini kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha basi kampuni ya Air Jordan na gari ndogo  baada ya kuacha njia na kuanguka katika eneo la migua wilaya ya Nzega mkoani Tabora. Efm imezungumza na kamanda wa mkoani humo Suzan Kaganda, amesema kuwa chanzo cha awali cha kutokea kwa ajali hiyo kinaonesha ni mwendo kasi wa basi hilo ambalo lilikuwa likitokea jijini Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam. Kamanda Kaganda ameeleza kuwa hadi sasa maiti imeshatambuliwa na ndugu...

Like
572
0
Wednesday, 15 April 2015
MIILI YA WATU WALIOFARIKI BAADA YA KUPIGWA NA RADI YAAGWA LEO KIGOMA
Local News

MIILI ya watu nane wakiwemo wanafunzi sita wa shule ya msingi Kibirizi, Manispaa ya Kigoma, Ujiji, Mwalimu mmoja na Mkazi mmoja wa eneo la Bangwe, waliofariki jana baada ya kupigwa na radi imeagwa leo mchana katika Viwanja vya shule hiyo ya Kibirizi. Pamoja na Viongozi na wananchi, Shughuli hiyo pia imehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa Machibya ambaye ametumia nafasi hiyo kutoa salamu zake za rambirambi kwa wanakigoma, pamoja na familia zilizopoteza wapendwa wao....

Like
288
0
Wednesday, 15 April 2015
ESCROW: OFISA MTENDAJI MKUU WA RITA ASIMAMISHWA KAZI
Local News

OFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili,Ufilisi na Udhamini-RITA,PHILIP SALIBOKO,amesimamishwa kazi. Hatua hiyo inatokana na kesi inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu, inayohusu kupokea mgawo wa fedha kutoka Akaunti ya Tegeta ESCROW. Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana na kuthibitishwa na SALIBOKO mwenyewe,kusimamishwa...

Like
327
0
Wednesday, 15 April 2015
JAMII YATAKIWA KUITAMBUA TASAF KUWA NI CHOMBO CHA SERIKALI
Local News

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF,LADISLAUS MWAMANGA,ameitaka jamii kuelewa kuwa, chombo hicho ni cha Serikali na hakina mwingiliano wa Dini,wala itikadi yoyote ya Kisiasa. Amesema lengo la TASAF ni kuonyesha uwajibikaji na kuwezesha Wananchi wote kuwa na maisha bora. MWAMANGA ameeleza hayo alipokuwa akizindua kikao kilichojumuisha Waandishi wa Habari,Waratibu,Wahasibu na Maofisa wanaofuatilia shughuli za mfuko...

Like
195
0
Wednesday, 15 April 2015
SERIKALI YAMALIZA RASMI MGOGORO WA ARDHI BAINA YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII NA HALMASHAURI YA WILAYA YA BAGAMOYO
Local News

HATIMAYE Serikali imeumaliza rasmi mgogoro wa ardhi uliodumu kwa kipindi kirefu baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo,unaohusisha eneo la hifadhi ya Taifa ya Saadani. Aidha,Serikali imeiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo,kukaa na Shirika la Hifadhi ya Taifa-TANAPA sanjari na wadau,kurejea mipaka ya zamani ya eneo hilo,ili kuepusha mgongano usio na tija. Mgogoro huo umeibuka mwaka 2005,baada ya Serikali kuipandisha hadhi Mbuga ya wanyamapori ya Saadani kuwa Hifadhi ya Taifa na kumpa...

Like
311
0
Wednesday, 15 April 2015
RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA MOROGORO KUFUATIA AJALI YA BASI NA LORI
Local News

RAIS JAKAYA KIKWETE,amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Dokta RAJABU RUTENGWE,kutokana na vifo vya watu 18 na wengine 11 kujeruhiwa katika ajali ya  basi na lori,iliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita. Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Msimba,barabara kuu ya Morogoro-Iringa,kilometa chache kutoka Ruaha Mbuyuni na kusababisha watu 18 kuteketea kwa moto. Dokta KIKWETE amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu 18 kutokana na ajali ya barabarani iliyosababisha miili yao kuungua...

Like
266
0
Wednesday, 15 April 2015
UKUMBI WA NKURUMAH WA CHUO KIKUU CHA UDSM WAINGIZWA KWENYE URITHI WA TAIFA
Local News

SERIKALI imeuingiza kwenye urithi wa taifa,Ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam,UDSM. Tukio hilo la kihistoria limefanyika katika ukumbi huo,ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii,LAZARO NYALANDU,ametia saini makubaliano ya kuingiza ukumbi huo kwenye urithi wa Taifa. Akizungumza katika hafla hiyo,Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam,Profesa RWEKEZA MUKANDALA,anesema tukio hilo ni muhimu kwa...

Like
355
0
Tuesday, 14 April 2015