VIJANA nchini wametakiwa kuacha kubweteka na kusubiri kuajiriwa na badala yake wajiajili wenyewe kwa ujasiliamali pamoja na kilimo cha kisasa. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara wa kutembelea shamba lenye ukubwa wa Ekari 300 lililopo katika kijiji cha Ngarambe wilayani Mkuranga mkoani Pwani ambalo linamilikiwa na Shirikisho la Wasanii Tanzania- SHIWATA, Mwenyekiti wa Mtandao huo Casim Taalib amesema kuwa mashamba hayo ni fursa nzuri kwa vijana kujiajiri. Taalib amesema vijana wamekuwa na dhana tofauti ya kusubiri...
MADEREVA wa mabasi ya abiria na malori ya mizigo nchini,wako kwenye mikakati mizito ya kuingia kwenye mgomo mkubwa, unaotarajiwa kuanza Ijumaa. Makakati huo unalenga kushinikiza Serikali kuingilia kati na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu malalamiko yao dhidi ya Mamlaka za serikali, ikiwemo kikosi cha usalama Barabarani na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na nchi Kavu-SUMATRA. Aidha madereva hao wameomba kukutana na Waziri wa Uchukuzi,SAMWEL SITTA,ili kuwasilisha malalamiko yao na kwamba ombi hilo likishindikana,hakutakuwa na maongezi zaidi...
JESHI la Zimamoto na Uokoaji mkoani Iringa,limetoa misaada mbalimbali kwa Kituo cha kulelea watoto Yatima Cha Sister Theresia, kilichopo Tosamaganga. Akikabidhi msaada huo,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto mkoani humo,KENNEDY KOMBA,amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuwa karibu na jamii. Amesema Watoto Yatima,wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kupata mahita muhimu ikiwemo chakula, Afya na malazi, hivyo ni jukumu la kila mmoja kuwasaidia ili kuondokana na hali ya utegemezi....
MBUNGE wa Moshi Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, PHILEMON NDESAMBURO, anatarajia kuwasilisha hoja binafsi katika kikao kijacho cha Bunge kuhusu mauaji ya JAMES JOHN. Katika hoja hiyo,NDESAMBURO anatarajia kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kuliambia Bunge sababu zinazolifanya Jeshi la Polisi kushikwa na kigugumizi kuwakamata watuhumiwa waliohusika katika mauaji hayo. JOHN, ambaye alikuwa meneja wa Baa na Car wash ya Mo-Town iliyopo Mjini Moshi Mjini,anadaiwa kutekwa June 09 mwaka 2009 na Ndugu Wanne wakiongozwa...
Kutokana na Sesrikali kushindwa kutoa tamko dhidi ya Muswada wa Mahakama ya Kadhi, Jumuiya ya Waislam na Taasisi 11 za Waislam, wameitaka Serikali kuonesha dhamira ya dhati kwa kurejesha mchakato wa mazungumzo baina yake na Waislam juu ya suala hilo. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Sheikh MUSSA KUNDECHA, amesema kuwa ,Serikali imeshindwa kutoa tamko kamili na badala yake Makanisa na Viongozi wa dini ndiyo wamekuwa wakitoa tamko juu...
IMEELEZWA kuwa, kuongezeka kwa Mifugo katika Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinganya,ni mojawapo ya sababu inayopelekea kuongezeka kwa tatizo la Maji katika Wilaya hiyo. Akizungumza na Waandishi wa habari Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Diwani wa Kata ya Ukenyenge, MAKANASA KISHIWA, amesema kuwa ili kuhakikisha tatizo la Maji linakwisha wameweza kuchimba Mto umbali wa Kilometa 15 kutoka Shinyanga na wataweza kusambaza Maji hayo. KISHIWA amesema kuwa, wamekuwa wakikaa vikao vya Kata kuweza kuzuia Wanakijiji kupeleka Mifugo katika vyanzo vya maji,...
UJENZI holela uliopo katika Kijiji cha Lamadi, umechangia kijiji hicho na baadhi ya Vitongoji vyake kukumbwa na mafuriko yaliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita. Akizungumza na Wananchi wa maeneo yaliyokumbwa na maafa hayo kwa nyakati tofauti, Mbunge wa jimbo la Busega mkoani humo, Dokta TITUS KAMANI amesemapamoja na kwamba kuna visababishi vya mafuriko yakiwemo mabadiliko ya Tabia ya nchi, ujenzi huo ni kikwazo cha maji. Dokta KAMANI amesema hayo wakati akitembelea Wahanga wa Maafa hayo na kuwapa pole wahanga,huku akimabatana na...
HALI ya Afya ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,JOSEPHAT GWAJIMA,imebadilika ghafla baada ya kushindwa kupanda ngazi katika ofisi za Kituo Kikuu cha polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam. Askofu GWAJIMA amefika kituoni hapo akiwa ameongozana na maaskofu zaidi ya Watano. Katika hali ya kushangaza,wakati akipanda ngazi kuelekea kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam,aliweza kupanda ngazi mbili,lakini alipojaribu ya tatu...
SERIKALI kwa kushirikiana na Wananchi wametakiwa kuendeleza jititihada zinazofanywa na wadau mbalimbali nchini,hasa katika kuhakikisha wanazuia na kupunguza vifo vya Akinamama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano. Changamoto hiyo imetolewa na Meneja wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na masuala ya Afya nchini-AMREF health Africa,mkoani Simiyu GODFREY MATUMU,wakati wa mkutano wa kufunga Mradi wa Uzazi Uzima. Amesema kuwa mashirika au taasisi binafsi ambazo zimekuwa zikijihusisha na masuala ya Afya zimekuwa zikibeba...
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania-TCRA,imesema Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutekeleza maazimio ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC pamoja na ya Jumuiya ya Afrika Mashariki-EAC katika kutumia mfumo wa matangazo wa Dijiti. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam,Meneja Mawasiliano wa TCRA-INNOCENT MUNGI,amesema nchi Wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mawasiliano ya Simu Duniani-ITU,kwa pamoja zimeridhia makubaliano ya kusimamisha mfumo wa Utangazaji wa television unaotumia Teknolojia ya...
WATANZANIA wameaswa kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Kituo cha Radio cha E FM kwa lengo la kuwasaidia kutimiza ndoto zao za maisha ya baadae pamoja na kuliletea Taifa maendeleo. Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa E FM,FRANCIS SIZA wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanza kwa shughuli za urushaji wa matangazo ya Efm Radio. Hafla hiyo imehudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Meya wa Manispaa ya Kinondoni YUSUPH MWENDA, Mbunge wa...