KATIKA kuhakikisha kuwa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kupitia mfumo wa –BVR- linafanikiwa serikali imeiagiza tume ya Uchaguzi nchini –NEC– kuandaa ratiba itakayosaidia kuonesha shughuli zote za uratibu wa zoezi hilo. Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu Mheshimiwa MIZENGO PINDA mjini Dodoma wakati akifunga rasmi kikao cha kumi na tisa cha Bunge ambapo amesema kuwa ni muhimu kwa ratiba hiyo kutangazwa kwa wananchi kabla ya sikuu ya PASAKA. Waziri PINDA amesema kuwa mbali na suala...
WATANZANIA wameaswa kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Kituo cha Radio cha E FM kwa lengo la kuwasaidia kutimiza ndoto zao za maisha ya baadae pamoja na kuliletea Taifa maendeleo. Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa E FM, FRANCIS SIZA wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanza kwa shughuli za urushaji wa matangazo ya Efm Radio. Hafla hiyo imehudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Meya wa Manispaa ya Kinondoni YUSUPH MWENDA, Mbunge...
MADEREVA wa magari makubwa ya mizigo wamemtaka wakala wa Barabara Tanzania-TANROADS,kujenga mizani mingi kama iliyopo eneo la Vigwaza,Bagamoyo mkoani Pwani,huku wakisisitiza kuwa,itapunguza foleni na rushwa. Wakizungumza na Efm,baadhi ya madereva ambao walikuwa wakielekea nchini Zambia,wamesema tangu mizani hiyo ianze ,kazi ya kupima imekuwa na ufanisi mkubwa tofauti na mizani ya Kibaha. Akizungumzia Mzani huo,Dereva HUSSEIN AMOUR amesema kuwa,kwa sasa hakuna ucheleweshaji wa kupima,jambo ambalo halikuwepo hapo...
WATANZANIA wameaswa kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Kituo cha Radio cha E FM kwa lengo la kuwasaidia kutimiza ndoto zao za maisha ya baadae pamoja na kuliletea Taifa maendeleo. Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa E FM -FRANSIS SIZA wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanza kwa shughuli za Urushaji wa Matangazo wa Kituo hiki ambapo pia imehudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo meya wa Manispaa ya Kinondoni,YUSUPH MWENDA na Mbunge...
WAZAZI nchini wametakiwa kuacha tabia ya kudharau mikakati mbalimbali ya serikali kuhusu afya za watoto na badala yake wawapeleke kupata chanjo na kuchunguza afya zao. Aidha wazazi pia wametakiwa kuwapeleka watoto wenye chini ya umri wa miaka 15 katika zahanati na vituo mbalimbali vya afya kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi. Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha akina mama na watoto wa zahanati ya Arafa Ugweno iliyopo Tandika jijini Dar es salaam Latifa...
SERIKALI imeahidi kuendelea na utekelezaji madhubuti utakaowezesha kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya kutoka mkoani Kigoma hadi Kasuru kwa lengo la kuboresha miundombinu katika mkoa huo. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa JOHN MAGUFULI wakati akijibu swali la mbunge wa Muhambwe mheshimiwa FELIX MKOSAMALI aliyetaka kujua utekelezaji wa serikali juu ya suala hilo. Waziri Magufuli ameahidi kuwa wizara itahakikisha inakamilisha ujenzi wa barabara...
WAKAZI wa Kinondoni mkoani Dar es salaam,wametakiwa kusherehekea Sikukuu ya Pasaka kwa Utulivu na Amani bila kufanya fujo. Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, AUGUSTINO SENGA,wakati akizungumza na Efm,ofisini kwake. Kamanda SENGA amesema ni vema wananchi kutumia Sikukuu hiyo kwa kusherehekea kwa Amani na Utulivu na kurejea nyumbani, kwani kinyume na hapo, jeshi la polisi litawachukulia hatua....
IMEELEZWA kuwa hujuma zinazofanywa na baadhi ya Wafanyabiashara nchini, zimeendelea kuigharimu Serikali kwa kuikosesha mapato. Hatua hiyo inatokana na baadhi ya Wafanyabiashara hao kuingiza bidhaa ambazo, zimekuwa zikilipiwa Ushuru mdogo. Kwa muda mrefu sasa, kumekuwepo na wimbi la Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es salaam, ambapo huandikisha taarifa na maelezo tofauti na bidhaa halisi zilizomo ndani ya makontena, ili kuwawezesha kukwepa kodi kwa kulipia kiasi...
SERIKALI imeondoa Muswada wa Mahakama ya Kadhi uliokuwa uwasilishwe. Katibu wa Bunge Dokta THOMAS KASHILILLAH,amesema Muswada huo hautakuwa kwenye orodha ya shughuli za Bunge. Amesema Suala la Mahakama ya Kadhi, lilikuwa lijadiliwe kwenye Muswada wa Mabadiliko ya sheria ndogo, ambao ulikuwa kwenye orodha ya kujadiliwa leo, hivyo nafasi ya Muswada huo itatumika kuendelea kujadili Miswada iliyoanza kujadiliwa....
POLISI Mkoani Katavi inamshikilia mkazi wa kitongoji cha Ntumba , Kijiji cha Mnyengele Wilayani Mpanda , DEOGRATIAS PASTORI kwa kumjeruhi mkewe kwa kumkata mkono wa kushoto na kupasua tumbo la Mgoni wake kwa panga . Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi , DHAHIRI KIDAVASHARI amethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku katika kitongoji cha Ntumba kijiji cha Mnyagala Kata ya Mnyagala Wilayani Mpanda. KIDAVASHARI amewataja majeruhi hao kuwa ni pamoja na Mke wa mtuhumiwa TABU NESTORY, MASAGA ELIAS ambao ...
SERIKALI imetoa tamko kuhusu utekelezaji wa upatikanaji wa huduma ya Maji safi na uondoaji wa maji taka katika jiji la Dar es salaam ili kupunguza adha na matatizo wanayoyapata wakazi wa jiji ambao idadi yake inaongezeka kila siku. Akizungumza wakati wa kutoa hoja hiyo Bungeni Mjini Dodoma Waziri wa Maji Profesa JUMANNE MAGHEMBE amesema Serikali imechukua hatua hiyo baada ya kuona ukubwa wa Tatizo hilo jijini,kufatia hoja binafsi juu ya tatizo hilo iliyowahi kutolewa na Mbunge wa Jimbo la Ubungo...