Mcheza tenisi wa Bulgaria Grigor Dimitrov ameomba radhi baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu pale alipoibamiza chini mara tatu fimbo yake ya kuchezea baada ya kukubali kichapo dhidi ya Diego Schwartzman katika michuano ya wazi ya Istanbul. Mbulgaria huyo aliyekuwa akilisaka taji lake la kwanza katika kipindi cha miaka miwili alipoteza kwa seti 6-7,5-7,7-6, 7-4,na 6-0. Dimitrov alipewa onyo kali aliporusha kwa mara ya kwanza na kwa hasira fimbo yake ya kuchezea mapema mnamo seti ya tatu na kisha akapewa...
WANASAYANSI nchini Brazil wamesema kuwa virusi vya ZIKA ambavyo vimehusishwa na kuzaliwa kwa watoto wakiwa na vichwa vidogo huenda ni hatari zaidi kuliko ilivyofikiriwa awali. Madaktari bingwa wamesema kuwa virusi vya Zika vinaweza kuwa sababu ya kutokea kwa matatizo ya neva za fahamu kwa mwanamke mmoja mjamzito kati ya watano wanaoathiriwa na Virusi hivyo. Madaktari wengi na watafiti kwa sasa wanakubali kuwa kuna uhusiano kati ya mbu anayeeneza virusi na tatizo la watoto kuzaliwa na dosari kwenye...
MKURUGENZI wa CIA John Brennan amesema kwa miaka mitano iliyopita Marekani imeharibu kwa kiasi kikubwa kundi la Al Qaed baada ya kuuawa kwa kiongozi wake mkuu Osama bin Laden kutokana na uvamizi wa vikosi maalum nchini Pakistan. Brennan amesema kuwa Bin Laden alikuwa nembo na mwenye mikakati imara na muhimu na ilikuwa lazima kumuondoa mtu huyo ambaye amehusika katika mashambulizi ya kigaidi mjini Washington na New York Septemba 11. Mkuu huyo wa CIA ameongeza kuwa kumuondoa kiongozi wa IS Abu Bakr Al-Baghdadi...
Beki wa Liverpool Mamadou Sakho amepewa marufuku ya siku 30 na shirikisho la soka barani Ulaya Uefa baada ya kuanzisha harakati za kumuadhibu baada ya kuaptikana ametumia dawa za kusisimua misuli. Marufuku hiyo ni ya mda hadi pale uamuzi wa mwisho utakapoafikiwa na kitengo cha maadili cha shirikisho hilo. Sakho mwenye umri wa miaka 26 alipatikana ametumia dawa za kusisimua misuli kufuatia ushindi wa mechi ya taji la Europa dhidi ya Manchester United mnamo tarehe 27 mwezi Machi. Aliamua kutopinga...
RAIA wa Marekani amefungwa jela miaka 10 na kazi ngumu nchini Korea Kaskazini baada ya kupatikana na makosa ya kufanya ujasusi, shirika la habari la Uchina la Xinhua limeripoti. Kim Dong-chul, raia wa Marekani aliyezaliwa Korea Kusini, alikamatwa mwezi Oktoba mwaka jana. Kim alifikishwa kwa wanahabari mjini Pyongyang mwezi jana na akaoneshwa akikiri makosa, na kusema kwamba alilipwa na Korea Kusini kufanya ujasusi...
MJUMBE wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Staffan de Mistura amezitaka Urusi na Marekani kuimarisha usitishaji tete wa mapigano nchini Syria kabla ya mazungumzo ya amani yenye lengo la kumaliza miaka 5 ya mzozo nchini humo. Kauli hiyo ya de Mistura inakuja muda mfupi baada ya kulifahamisha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mazungumzo ya amani, ambayo amesema yamepiga hatua licha ya vikwazo vya hivi ...
MAMIA ya watu wamekusanyika nje ya uwanja wa ndege wa Kinshasa kuupokea mwili wa mwanamuziki Papa Wemba uliowasili nchini humo kutoka Abidjan. Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya mwili huo kuwekwa katika uwanja wa mpira kwa raia kutoa heshima zao za mwisho. Maafisa wa serikali na wanadiplomasia watahudhuria ibada ya kumkumbuka mwanamuziki huyo katika uwanja wa ndege kabla ya mwili huo kupelekwa katika chumba cha...
MGOMO wa wafanyakazi wa sekta ya umma umevuruga shughuli za kawaida nchini Ujerumani hii leo. Wanachama wa chama cha wafanyakazi wa sekta ya umma Verdi wamegoma kufanya kazi kutokana na madai ya nyongeza ya mshahara. Viwanja vya ndege vya Frankfurt, Dusseldorf na Munich vimeathirika na mgomo huo ikiwa ni pamoja na usafiri wa mjini katika miji mbali mbali, lakini uwanja wa ndege wa mjini Berlin unafanyakazi kama ...
SALAH ABDESLAM , anayetuhumiwa kuchukua nafasi ya juu katika mashambulizi ya mjini Paris ambayo yamesababisha watu 130 kuuwawa, anafikishwa mahakamani nchini Ufaransa leo, kwa mtazamo wa kuwekwa chini ya uchunguzi rasmi. Hatua hiyo inakuja baada ya Abdeslam kupelekwa nchini Ufaransa kutoka Ubelgiji mapema leo Jumatano. Mtuhumiwa huyo aliwasili nchini Ufaransa mapema leo...
NCHINI Marekani, tajiri Donald Trump amesema kuwa anajihisi sasa kama mgombea mteule wa urais wa chama cha Republican. Amesema hayo alipokuwa akiwahutubia wafuasi wake baada ya vyombo vya habari kutangaza kuwa amepata ushindi katika majimbo yote matano kaskazini mashariki mwa Marekani. Katika shughuli za upigaji kura wa mchujo kwenye majimbo hayo, mtafuta nafasi katika chama cha Democratic Bi Hillary Clinton alimpiku muwaniaji mwenzake Bernie Sanders, ambaye alishinda katika jimbo moja tu la Rhode...
SERIKALI ya Venezuela imebuni mikakati ambayo itapelekea wafanyakazi wapatao milioni mbili wa serikali, kufanya kazi kwa siku mbili pekee kwa wiki katika kipindi cha majuma mawili. Hatua hii inalenga kusaidia kukabiliana na uhaba wa umeme ambao unayumbayumba nchini humo. Wafanyakazi hao wa umma na wale wanaofanya kazi katika sekta zinazomilikiwa na serikali watafika kazini siku za Jumatatu na Jumanne pekee hadi matatizo hayo ya nguvu za umeme...