Global News

TENISI: GRIGOR DIMITROV AOMBA RADHI
Global News

Mcheza tenisi wa Bulgaria Grigor Dimitrov ameomba radhi baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu pale alipoibamiza chini mara tatu fimbo yake ya kuchezea baada ya kukubali kichapo dhidi ya Diego Schwartzman katika michuano ya wazi ya Istanbul. Mbulgaria huyo aliyekuwa akilisaka taji lake la kwanza katika kipindi cha miaka miwili alipoteza kwa seti 6-7,5-7,7-6, 7-4,na 6-0. Dimitrov alipewa onyo kali aliporusha kwa mara ya kwanza na kwa hasira fimbo yake ya kuchezea mapema mnamo seti ya tatu na kisha akapewa...

Like
194
0
Monday, 02 May 2016
VIRUSI VYA ZIKA NI HATARI ZAIDI
Global News

WANASAYANSI nchini Brazil wamesema kuwa virusi vya ZIKA ambavyo vimehusishwa na kuzaliwa kwa watoto wakiwa na vichwa vidogo huenda ni hatari zaidi kuliko ilivyofikiriwa awali. Madaktari bingwa wamesema kuwa virusi vya Zika vinaweza kuwa sababu ya kutokea kwa matatizo ya neva za fahamu kwa mwanamke mmoja mjamzito kati ya watano wanaoathiriwa na Virusi hivyo. Madaktari wengi na watafiti kwa sasa wanakubali kuwa kuna uhusiano kati ya mbu anayeeneza virusi na tatizo la watoto kuzaliwa na dosari kwenye...

Like
170
0
Monday, 02 May 2016
CIA YADAI KUIVURUGA AL QAEDA
Global News

MKURUGENZI wa CIA John Brennan amesema kwa miaka mitano iliyopita Marekani imeharibu kwa kiasi kikubwa kundi la Al Qaed baada ya kuuawa kwa kiongozi wake mkuu Osama bin Laden kutokana na uvamizi wa vikosi maalum nchini Pakistan. Brennan amesema kuwa Bin Laden alikuwa nembo na mwenye mikakati imara na muhimu na ilikuwa lazima kumuondoa mtu huyo ambaye amehusika katika mashambulizi ya kigaidi mjini Washington na New York Septemba 11. Mkuu huyo wa CIA ameongeza kuwa kumuondoa kiongozi wa IS Abu Bakr Al-Baghdadi...

Like
171
0
Monday, 02 May 2016
SAKHO APEWA MARUFUKU YA SIKU 30 NA UEFA
Global News

Beki wa Liverpool Mamadou Sakho amepewa marufuku ya siku 30 na shirikisho la soka barani Ulaya Uefa baada ya kuanzisha harakati za kumuadhibu baada ya kuaptikana ametumia dawa za kusisimua misuli. Marufuku hiyo ni ya mda hadi pale uamuzi wa mwisho utakapoafikiwa na kitengo cha maadili cha shirikisho hilo. Sakho mwenye umri wa miaka 26 alipatikana ametumia dawa za kusisimua misuli kufuatia ushindi wa mechi ya taji la Europa dhidi ya Manchester United mnamo tarehe 27 mwezi Machi. Aliamua kutopinga...

Like
222
0
Friday, 29 April 2016
MMAREKANI AHUKUMIWA KIFUNGO NA KAZI NGUMU KOREA
Global News

RAIA wa Marekani amefungwa jela miaka 10 na kazi ngumu nchini Korea Kaskazini baada ya kupatikana na makosa ya kufanya ujasusi, shirika la habari la Uchina la Xinhua limeripoti. Kim Dong-chul, raia wa Marekani aliyezaliwa Korea Kusini, alikamatwa mwezi Oktoba mwaka jana.   Kim alifikishwa kwa wanahabari mjini Pyongyang mwezi jana na akaoneshwa akikiri makosa, na kusema kwamba alilipwa na Korea Kusini kufanya ujasusi...

Like
214
0
Friday, 29 April 2016
URUSI NA MAREKANI ZATAKIWA KUIMARISHA USITISHAJI TETE WA MAPIGANO SYRIA
Global News

MJUMBE  wa  Umoja wa  Mataifa  nchini  Syria  Staffan de Mistura  amezitaka  Urusi  na  Marekani  kuimarisha usitishaji tete wa  mapigano  nchini  Syria  kabla  ya mazungumzo  ya  amani  yenye lengo  la  kumaliza  miaka 5 ya mzozo  nchini  humo.   Kauli hiyo ya  de Mistura  inakuja  muda  mfupi baada  ya kulifahamisha  baraza  la  Usalama  la  Umoja  wa  Mataifa juu  ya  mazungumzo  ya  amani, ambayo amesema yamepiga  hatua  licha  ya  vikwazo  vya  hivi ...

Like
242
0
Thursday, 28 April 2016
KINSHASA: MAMIA YA WATU WAKUSANYIKA KUUPOKEA MWILI WA PAPA WEMBA
Global News

MAMIA ya watu wamekusanyika nje ya uwanja wa ndege wa Kinshasa kuupokea mwili wa mwanamuziki Papa Wemba uliowasili nchini humo kutoka Abidjan. Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya mwili huo kuwekwa katika uwanja wa mpira kwa raia kutoa heshima zao za mwisho. Maafisa wa serikali na wanadiplomasia watahudhuria ibada ya kumkumbuka mwanamuziki huyo katika uwanja wa ndege kabla ya mwili huo kupelekwa katika chumba cha...

Like
272
0
Thursday, 28 April 2016
MGOMO WA WAFANYAKAZI WAKWAMISHA SHUGHULI ZA KAWAIDA UJERUMANI
Global News

MGOMO wa  wafanyakazi  wa  sekta  ya  umma umevuruga shughuli  za  kawaida nchini  Ujerumani  hii leo. Wanachama  wa  chama  cha  wafanyakazi  wa  sekta  ya umma Verdi wamegoma  kufanya kazi  kutokana na madai  ya nyongeza ya mshahara.   Viwanja  vya  ndege  vya Frankfurt, Dusseldorf  na  Munich vimeathirika  na  mgomo  huo  ikiwa  ni  pamoja na  usafiri wa mjini katika miji  mbali  mbali,  lakini  uwanja  wa  ndege wa mjini  Berlin unafanyakazi  kama ...

Like
212
0
Wednesday, 27 April 2016
UBELGIJI YAMPELEKA UFARANSA MSHUKIWA WA PARIS
Global News

SALAH ABDESLAM , anayetuhumiwa  kuchukua  nafasi  ya juu  katika mashambulizi  ya  mjini  Paris ambayo yamesababisha  watu  130  kuuwawa, anafikishwa mahakamani  nchini  Ufaransa  leo, kwa mtazamo  wa kuwekwa  chini  ya  uchunguzi  rasmi.   Hatua  hiyo inakuja  baada  ya  Abdeslam  kupelekwa nchini  Ufaransa  kutoka  Ubelgiji  mapema  leo Jumatano. Mtuhumiwa  huyo  aliwasili  nchini  Ufaransa  mapema  leo...

Like
183
0
Wednesday, 27 April 2016
TRUMP APETA MAJIMBO MATANO MUHIMU MAREKANI
Global News

NCHINI Marekani, tajiri Donald Trump amesema kuwa anajihisi sasa kama mgombea mteule wa urais wa chama cha Republican. Amesema hayo alipokuwa akiwahutubia wafuasi wake baada ya vyombo vya habari kutangaza kuwa amepata ushindi katika majimbo yote matano kaskazini mashariki mwa Marekani. Katika shughuli za upigaji kura wa mchujo kwenye majimbo hayo, mtafuta nafasi katika chama cha Democratic Bi Hillary Clinton alimpiku muwaniaji mwenzake Bernie Sanders, ambaye alishinda katika jimbo moja tu la Rhode...

Like
276
0
Wednesday, 27 April 2016
WATU KUFANYA KAZI SIKU MBILI KWA WIKI VENEZUELA
Global News

SERIKALI ya Venezuela imebuni mikakati ambayo itapelekea wafanyakazi wapatao milioni mbili wa serikali, kufanya kazi kwa siku mbili pekee kwa wiki katika kipindi cha majuma mawili. Hatua hii inalenga kusaidia kukabiliana na uhaba wa umeme ambao unayumbayumba nchini humo. Wafanyakazi hao wa umma na wale wanaofanya kazi katika sekta zinazomilikiwa na serikali watafika kazini siku za Jumatatu na Jumanne pekee hadi matatizo hayo ya nguvu za umeme...

Like
232
0
Wednesday, 27 April 2016