RIPOTI kutoka nchini Nigeria zinasema kuwa karibu watu 60 huenda waliuawa wakati wa shambulizi katika kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa nchi hiyo lililoendeshwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa na Boko Haram. Shambulizi hilo lilitokea katika jimbo la Yobe lilifanyika Alhamisi iliyopita na habari hizo zimepatikana kutoka kwa wale walionusurika. Walioshuhudia wamesema kuwa wanamgambo wa Boko Haram waliwasili katika kijiji hicho wakitumia pikipiki ambapo walianza kuwafyatulia watu...
MAREKANI imeanza mazungumzo na mataifa mengine wanachama kwenye Umoja wa Mataifa, juu ya uwezekano wa kuiwekea vikwazo Sudan Kusini, endapo serikali itashindwa kusaini makubaliano ya amani na waasi, ndani ya wiki mbili zijazo. Mshauri wa usalama wa Rais Barack Obama, Susan Rice, amesema Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini kwa mara nyingine ameivuruga nafasi ya upatikanaji wa amani. Juzi Jumatatu, rais huyo wa Sudan Kusini aliishangaza Marekani na mataifa mengine yanayosimamia mazungumzo ya amani ya nchi yake, kwa kukataa kusaini...
SHIRIKA la Umoja wa Ulaya linalopambana na maswala ya uhamiaji haramu na biashara ya binadamu, Frontex limetoa wito kwa nchi wanachama wa umoja huo kutoa msaada zaidi kwa nchi tatu zilizoathirika kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji. Ugiriki, Italia na Hungary ni nchi zinazoelezwa kuathiriwa zaidi. Watu hao wengi wanaelezwa kutoka nchini Syria,Afghanistan na nchi za kusini mwa jangwa la Sahara wakikimbia hali mbaya ya usalama na...
POLISI nchini Bangladesh wamewakamata watu wengine watatu, akiwemo raia mmoja wa Uingereza kuhusiana na mauaji ya mwanablogu maarufu ambaye anaaminika kuwa si-mcha Mungu. Idara ya Polisi imesema kuwa raia huyo wa Bangladesh mwenye asili ya Uingereza anayefahamika kwa jina la Touhidur Rahman anashukiwa kutoa ufadhili wa kifedha kwa washukiwa hao wengine wawili waliokamatwa juzi akiwemo Niloy Neel. Taarifa zinasema kuwa washukiwa wawili ambao wanatuhumiwa kuhusika moja kwa moja na mauwaji hayo walikuwa wamekamatwa tayari juma lililopita....
RAIS wa Gabon Ali Bongo Ondimba ameahidi kutoa urithi wake wote kwa vijana nchini humo. Rais Bongo amesema kuwa mali yote aliyopokea kama urithi kutoka kwa babaake mzazi aliyekuwa rais wa Gabon kwa kipindi kirefu,Omar Bongo itakwenda kwa vijana wa Gabon. Shirika la habari la AFP limesema kuwa rais Bongo ameahidi kuuza majengo mawili yaliyopo Ufaransa aliyopewa na mzazi kwa thamani ya Franka moja kama ishara ya kujitolea kuimarisha hali ya kiuchumi ya vijana wa taifa...
MAMIA ya vijana wamejitokeza nchini Cameroon kujitolea kuwapa damu wanajeshi wanaopambana na kundi la wapiganaji la Boko Haram kaskazini mwa nchi hiyo. Kampeni hiyo imeandaliwa na baraza la muungano wa vijana nchini humo ambao wamesema kuwa huo ndio mchango wao mkubwa na muhimu dhidi ya ugaidi. Hospilitali ya kijeshi ya Yaounde ambayo wanajeshi waliojeruhiwa kutoka Cameroon na Chad hupewa matibabu, imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa akiba ya damu ya...
MUDA mchache baada ya Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini kukataa kusaini makubaliano ya amani na hasimu wake, Riek Machar, Marekani imemtaka kufanya hivyo ndani ya wiki mbili, au akabiliane na hatua kali. Machar alisaini hapo jana makubaliano ambayo yanakusudiwa kukomesha miezi 20 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini Rais Kiir amesema atarejea mjini Addis Ababa, baada ya siku 15 za mashauriano. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani John Kirby, amewaambia waandishi wa habari kuwa nchi...
RAIS Abdel Fattah al-Sisi wa Misri, ameidhinisha hatua mpya za kupambana na ugaidi, ambazo zimezua utata zenye nia ya kuimarisha uwezo wa taifa hilo kukabiliana na maasi ya waislamu wenye itikadi kali. Wale watakaopatikana na hatia ya kubuni au kuongoza makundi ya kigaidi, watakabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha miaka kumi au maisha jela. Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yamesema kuwa rais Abdel Fattah al-Sisi, atatumia sheria hizo mpya kuwafungia wapinzani wake na pia kuwazima waasi au...
PANDE zinazozozana nchini Sudan Kusini zinafanya mazungumzo nchini Ethiopia hii leo ikiwa ni siku ya mwisho ya mazungumzo ya amani kabla ya vikwazo vya kimataifa kuwekewa pande zote. Lakini serikali ya Sudan Kusini pamoja na waasi wamesema huenda wakahitaji muda zaidi kutatua maswala kama vile mgawanyo wa madaraka katika serikali ya mpito. Mwakilishi maalum wa Muungano wa Ulaya, Alexander Rondo, ameonya kuwa ucheleweshwaji wa kufikia makubaliano hautavumiliwa. Marais wa Uganda, Kenya na Ethiopia pia wanashiriki mazungumzo...
MIILI ya watu imeendelea kuopolewa zaidi katika eneo lilitokea mripuko katika mji wa bandari wa Tianjin, nchini China, na kufanya idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mkasa huo kufikia 122. Hayo yanafanyika wakati wataalamu wakiharakisha kuondosha kemikali hatari katika eneo hilo na waendesha mashitaka wanajitayarisha kuwachunguza wale wote waliohusika na maafa hayo. Zaidi ya watu 700 walijeruhiwa na wengine 95, wakiwemo wazima moto...
VIONGOZI wa Mataifa 15 ya Jumuia ya Nchi za Kusini mwa Afrika- SADC, wanatarajia kukutana leo nchini Botswana katika Mkutano wao wa Mwaka. Mkutano huo unafanyika wakati eneo hilo linakumbwa na upungufu wa chakula ambapo watu wanaokadiriwa kufikia milioni 27.4 kutoka idadi ya jumla ya wakazi 292, wa eneo hilo wanategemea msaada wa chakula ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Msemaji wa Shirika la Mpango wa chakula wa Dunia-WFO, David Orr, ameliambia shirika la habari la Ufaransa-AFP kuwa Zimbabwe na Malawi...