SERIKALI ya Kenya inatarajiwa kuharibu boti moja iliyopatikana imebeba takriban kilo 7 za mihadarati aina ya Heroini. Boti hiyo inayoitwa ‘Baby Iris’ ilikamatwa na polisi kwa tuhuma za ulanguzi wa mihadarati katika bahari ya Kenya huko Mombasa na itaharibiwa kulingana na sheria za Kenya. Ripoti ya polisi inasema kuwa ‘Baby Iris’ inamilikiwa na bwenyenye mmoja raia wa Uingereza na kwamba Jeshi la wanamaji la Kenya ndilo lililokabidhiwa jukumu hilo la...
WAFUASI wa rais Yoweri Museveni wamewashambulia wafuasi wa Amama Mbabazi nyumbani kwake katika kitongoji kimoja cha mji mkuu wa Kampala. Vijana hao waliokuwa wamevalia shati zenye maandiko ya kumuunga mkono rais Museveni walishambulia boma la kiongozi huyo ambaye ameahidi kuwania kiti cha urais dhidi ya rais Museveni katika uchaguzi mkuu ujao. Vijana hao walimtuhumu waziri huyo mkuu wa zamani kwa kuwapa ahadi hewa kuwa angewapa...
MIEZI miwili baada ya kukamatwa na kuzuiliwa nchini Uingereza mkuu wa ujasusi wa Rwanda Luteni Jenerali Karenzi Karake hatimaye amerejea nchini Rwanda jana. Kiongozi huyo alikamatwa Uingereza mwezi Juni mwaka huu baada ya kukamilisha ziara ya kikazi nchini humo kwa tuhuma za uhalifu wa kivita. Jenerali Karenzi ni mmoja wa maafisa 40 wa jeshi la Rwanda ambao majina yao yapo kwenye waranti uliotolewa na jaji wa Uhispania kutaka wakamatwe kutokana na tuhuma za uhalifu wa kivita wakati wa mauaji ya ...
RAIS wa zamani wa Cuba Fidel Castro ametimiza umri wa miaka 89 kwa kuandika barua ya wazi kwa taifa lake. Barua hiyo ilichapishwa katika gazeti la serikali la Granma ambapo hajazungumzia lolote kuhusu ufunguzi wa ubalozi mpya wa Marekani jijini Havana utakavyofanya kazi na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry. Badala yake ameituhumu Marekani kwa kuisababishia hasara ya mamilioni ya dola baada ya miaka mingi ya vikwazo vya biashara baina ya nchi hizo...
BOMU kubwa lililokuwa katika gari limeripuka katika soko lililokuwa na watu wengi mjini Baghdad leo na kusababisha watu 50 kuuwawa na wengine 150 wamejeruhiwa. Polisi mjini Baghdad imesema gari hilo liliripuriwa katika soko la chakula la Jamila katika mji wa Sadr, ambao wakazi wake wengi ni Washia , Mashariki mwa Baghdad. Maafisa wa hospitali wamesema wengi wa wahanga wamepata majeraha makubwa ....
WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry amesema iwapo Marekani itajitoa kutoka katika makubaliano ya nyuklia na Iran na kutaka washirika wake watekeleze hatua za vikwazo vya Marekani, kutakuwa na kitisho cha kupotea imani na uongozi wa Marekani pamoja na kupoteza mwelekeo wa sarafu yake ya dola. Akitetea makubaliano ya Julai 14 yaliyoafikiwa mjini Vienna kati ya Iran na mataifa makubwa yenye nguvu duniani, Kerry ametoa utetezi mpya katika ...
MAAFISA wa Uholanzi wanaochunguza kuangushwa kwa ndege ya Malaysia yenye nambari ya safari MH17, wametangaza kwamba wamepata kitu ambacho kinaweza kuwa kipande cha roketi aina ya BUK inayotengenezwa na Urusi, katika eneo ilikoanguka ndege hiyo Mashariki mwa Ukraine. Tangazo hilo lililotolewa jana ni la kwanza kutoka kwa maafisa hao, linalohusisha ushahidi wa matumizi ya roketi katika kuangushwa ndege hiyo. MH17 iliangushwa tarehe 17 Julai mwaka jana katika eneo la Mashariki mwa Ukraine eneo linalokumbwa na mzozo, na kuuwa watu wote...
RAIS wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameapa kutolegeza kamba katika operesheni ya kijeshi inayoendelea dhidi ya wanamgambo wa Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi, PKK. Erdogan ameyasema hayo katika hotuba yake kwenye sherehe ya kijeshi, wakati serikali yake ikianzisha mashambulizi mapya dhidi ya waasi wa kikurdi ndani ya mipaka ya Uturuki. Wiki hii ndege za jeshi la Uturuki zimefanya mashambulizi kuvilenga vituo 17 vya wakurdi katika mkoa wa Hakkari, katika juhudi mpya dhidi ya chama cha PKK ambacho kimepigwa...
BUNGE la Iraq limepiga kura kwa wingi kuunga mkono mapendekezo yaliotolewa na waziri mkuu Haider al Abadi kwa lengo la kukabiliana na ufisadi pamoja na kupunguza matumizi ya fedha serikalini. Spika wa bunge hilo Salim al Juburi amesema kuwa muswada huo umepitishwa bila upinzani wowote ambao unalenga kupunguzwa kwa baadhi ya nyadhfa serikalini, kumaliza ubaguzi wa kidini pamoja na wa kisisasa. Hatua hiyo imefikiwa wakati ambapo kumekuwa na maanadamano ya raia kuhusu kukatika mara kwa mara kwa umeme wakati ambapo...
NCHI ya Uturuki imeanzisha tena msururu wa mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi yanayolenga maeneo 17 kusini mashariki mkoani Hakkari katika mpaka na Iran. Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Uturuki imeshuhudia ghasia zaidi katika wiki za hivi karibuni kati ya wanajeshi na wapiganaji wa Kikurdi wanaotaka kujiondoa katika utawala wa jeshi. Mashambulio hayo yanajiri siku moja baada ya watu tisa kuuawa katika msururu wa mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama huku wengine wakiwa katika eneo la kusini mashariki mwa nchi...
SERIKALI ya Marekani imesema kwamba ina wasiwasi mkubwa kuhusiana na kuzuiwa kwa wapinzani tisini katika mji mkuu wa Cuba, Havana mwishoni mwa wiki iliyopita. Wajumbe wa kundi moja la kipinzani la wasichana wanaovaa nguo nyeupe wamesema kuwa wanausalama wa Cuba waliwazingira na kuwashililia kisha kuwaachilia huru baada ya saa nne unusu kupita. Kukamatwa huko kumekuja siku chache kabla ya ziara ya John Kerry jijini Havana, ziara ambayo ni ya kwanza kutoka kwa kiongozi wa marekani baada ya miaka saba....