BARAZA la usalama la umoja wa mataifa limeunga mkono mpango wa kutuma maafisa wake wa ngazi ya juu nchini Burundi kwa ajili ya kutatua hali ya sintofahamu iliyopo nchini humo. Baraza lililopo kwa sasa chini ya Mnigeria Joy Ogwu limesema kuwa kumekuwepo na wasiwasi mkubwa juu ya hali ya usalama nchini Burundi huku likitoa wito kwa serikali kufanya mazungumzo ya amani na upande wa upinzani. Kiongozi mwandamizi wa umoja wa mataifa kuhusiana na haki za binaadam Ivan Simonovic ambaye alipelekwa...
MAANDAMANO yamefanyika nchini Marekani kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuuawa kwa kijana mweusi, Michael Brown ambaye hakuwa na silaha. Kijana huyo aliuawa na polisi mzungu katika mji wa Ferguson jimboni Missouri Agosti mwaka uliopita. Miezi michache iliyofuata, watu wengine kadhaa weusi wasio na silaha waliuawa na maafisa wa polisi katika miji mbali mbali ya Marekani, ikiwemo New York, Cleveland na Baltimore. Mamia ya watu wamekusanyika katika mji wa Ferguson jana Jumapili, na kufanya matembezi ya kimya ambayo yaliongozwa na baba wa...
JESHI nchini Mali limesema zaidi ya watu kumi wameuawa katika shambulio moja kwenye mji wa Gaberi kaskazini nchini humo. Shambulizi hilo limekuja siku moja baada ya watu kumi na watatu wakiwemo washambuliaji wanne kuuawa ambapo washukiwa wa tukio hilo Wanajeshi wa Kiislam walishambuliana na jeshi la serikali walipowazingira kwenye hotel moja katikati mwa mji wa Sevare. Msemaji wa jeshi la Mali alikaririwa akisema ni mapema mno kujua kama mashambulizi hayo mawili yalikua na uhusiano ama...
NDUGU na jamaa wa abiria waliokuwemo katika ndege ya Malaysia iliyotoweka, yenye namba za safari MH370 wameoneshwa kukasirishwa na kile wanachosema kuwa ripoti zinazotolewa juu ya kupotea kwa ndege hiyo ni za kutatanisha. Jana Malaysia ilithibitisha kuwa kipande cha bawa la ndege kilichogunduliwa katika kisiwa cha Reunion kilikuwa ni sehemu ya ndege hiyo iliyopotea. Hata hivyo nchi ya Ufaransa imesema itapeleka vifaa zaidi vya majini na angani nje ya kisiwa cha Reunion leo kutafuta mabaki zaidi ambapo jumla ya watu...
WATU waliojihami kwa kutumia bunduki wameshambulia zaidi ya hoteli mbili katika mji wa Sevare eneo la katikati ya nchini Mali. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kwamba watu hao waliokuwa wakiendesha pikipiki wameingia katika eneo hilo na kuanza kufyatua risasi kwenye majengo hayo. Imebainika kwamba ingawa Mji wa Sevare una kituo cha jeshi la anga pamoja na wanajeshi kadhaa wa kikosi cha umoja wa mataifa cha kulinda amani lakini bado matatizo kama hayo...
WAASI wa kundi la kigaidi la Boko Haram wamewaua kwa bunduki watu wasiopungua tisa katika vijiji viwili Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Wanakijiji wameelezea namna ambavyo watu waliokuwa wamebeba silaha walivyowasili kwa pikipiki na kuvamia kijiji chao. Wanamgambo walipora mali kwenye nyumba na maduka na kisha kuzichoma moto nyumba zilizokuwa zimeezekwa kwa nyasi. Shambulio hili limewalazimisha mamia ya wakazi wa eneo hilo kukimbilia mji wa Potiskum uliopo kilomita 70 kutoka nyumbani kwao....
WAGOMBE 10 wanaoongoza katika kura za maoni za kumtafuta atakayepeperusha bendera ya chama cha Republican katika uchaguzi mkuu wa Marekani jana usiku wamenadi sera zao katika mdahalo ulioonyeshwa kwenye televisheni. Miongoni mwa walioshiriki ni bilionea Donald Trump ambaye kwa sasa ndiye mwenye nafasi nzuri zaidi ya kushinda, pamoja na senator Rand Paul wa jimbo la Kentucky, seneta wa Florida Marco Rubio na seneta wa Texas Ted Cruz. Mdahalo huo uliodumu kwa masaa mawili uliwapa nafasi wagombea kutoa maoni...
MAREKANI imefanya shambulio lake la kwanza la mabomu dhidi ya wanamgambo wa Dola la Kiislamu kutokea Uturuki. Afisa wa Uturuki amesema ndege isiyokuwa na rubani iliruka kutoka kituo cha jeshi la anga kusini mwa nchi hiyo, na kushambulia maeneo karibu na Raqqa nchini Syria. Viongozi wa mataifa ya magharibi wamekuwa wakiitaka Uturuki muda mrefu kuchukua jukumu kubwa zaidi katika mapambano dhidi ya IS, lakini serikali ya ...
HELIKOPTA ya jeshi la Afghanistan imeanguka katika jimbo la kusini la Zabul leo, na wanajeshi 17 wameuwawa, ikiwa ni pamoja na marubani watano. Mkuu wa polisi wa jimbo hilo Mirwais Noorzai amesema sababu ya kuanguka helikpota hiyo haifahamiki na uchunguzi unafanyika. Wizara ya ulinzi imesema ajali hiyo inaaminika imesababishwa na hitilafu ya kiufundi , lakini hayakutolewa maelezo zaidi....
WAZIRI MKUU wa Australia Tony Abbott amesema kuwa ile sintofahamu juu ya ndege ya MH 370 iliyopotea inakaribia kupatiwa ufumbuzi baada ya Malaysia kutangaza kuwa mabaki ya ndege yaliyopatikana kuwa ni sehemu ya mabaki ya ndege hiyo iliyopotea. Wataalamu wamethibitisha kuwa kipande cha bawa la ndege kilichokutwa katika ufukwe wa bahari ya hindi ni sehemu ya ndege iliyopotea, iliyokuwa mali ya malaysia, waziri mkuu, Najib Razak amethibitisha hilo jana, jumatano. Razak amesema kuwa, ni siku ya 515 tangu ndege ipotee,...
RAIA wa Japan leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 tangu shambulio la kwanza la bomu la Atomiki kutekelezwa mjini Hiroshima. Takriban watu laki moja na arobaini walikadiriwa kupoteza maisha baada ya Ndege ya Marekani kudondosha bomu ambalo liliuharibu mji huo tarehe 6 mwezi Agosti mwaka 1945. Katika hotuba yake, Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema kumbukumbu ya Heroshima inasisitiza uhitaji wa kufanya jitihada ya kupiga vita matumizi ya Nuklia....