WATU wanaoshukiwa kuwa ni Wayahudi wenye msimamo mkali wameyachoma moto makazi ya Wapalestina huko Ukingo wa Magharaibi hii leo na kumuua mtoto wa miezi 18 na kuwajeruhi wengine wanne. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameyaita mashambulizi hayo kuwa ni tukio la kigaidi na kusema kuwa ameshitushwa na kitendo hicho cha kinyama ambacho kina dhamira zote za kigaidi. Msemaji wa Serikali ya Israel Mark Regev amesema wanahakikisha wanawakamata na kuwashitaki waliohusika katika tukio hilo huku wazazi wa mtoto huyo aliyeuawa...
MTU anayedaiwa kubaini ushahidi wa kwanza wa mabaki ya Ndege ya Malysia iliyopotea ameelezea mazingira ya yalipopatikana mabaki hayo,na kwamba yeye alikuwa katika shughuli zake za kawaida katika hoteli moja kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi. Ni takribani miezi sita hadi sasa tangu kupotea kwa ndege hiyo huku kukiwa hakuna taarifa za uhakika kuhusu chanzo cha ajali hiyo Mabaki hayo yaliyopatikana yanapelekwa Ufaransa kwa uchunguzi zaidi ili kubaini kama niya ndege ya Malaysia iliyopotea Boing 777,MH 370 iliyokuwa ikitoka Quala...
MTOTO mchanga wa kipalestina ameuawa baada ya nyumba yao kumwagiwa petroli na kuchomwa moto katika makazi ya West Bank na walioshuhudia wanawashuku walowezi wa kiyahudi kuwa ndio waliotekeleza shambulizi hilo. Inaelezwa kuwa mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu alikuwa ndani ya nyumba yao ilipomwagiwa petroli na kuchomwa. Wazazi wake na kaka yake walinusurika shambulizi hilo ambalo serikali ya Israeili imelitaja kuwa la...
WAZIRI Mkuu wa Uingereza ameibua utata kwa kutoa maneno ya kuwafananisha wahamiaji haramu wanaojaribu kuvuka mpaka na kuingia Uingereza kuwa wao ni kama kundi la nyuki. Baraza linalowashughulikia wakimbizi Nchini Uingereza limesema kuwa hiyo haioneshi thamani kwa watu na ni hatari zaidi kwa kuwa imetoka kinywani mwa kiongozi mwenye hadhi kubwa duniani. Waziri huyo mkuu ambaye yuko ziarani Vietnam alikuwa akitoa maoni kuhusiana na vurugu zinazoendelea katika mji wa Calais nchini Ufaransa ambapo mamia ya wahamiaji wamekimbia kuelekea Uingereza....
SHIRIKA la ndege la Kenya –KQ- limetangaza hasara kubwa ya Shilingi bilioni 25.7 za Kenya sawa na dola milioni 2.57 katika kipindi cha fedha cha mwaka 2014-2015. Hii ni hasara ya asilimia 661 ikilinganishwa na kipindi cha fedha cha mwaka 2013-2014 ingawa mwaka uliopita kampuni hiyo ya ndege ilitangaza kupata hasara ya shilingi bilioni 3.3. Uongozi wa shirika hilo unasema kuwa hasara hiyo kubwa imetokana na kuporomoka kwa thamani ya sarafu ya Kenya ambayo imeporomoka kwa asilimia 11 ya thamani...
RAIS wa Nigeria Muhammadu Buhari ameanza ziara ya siku mbili nchini Cameroon na akiwa huko analenga kuboresha mahusiano na nchi jirani na pia kuimarisha ushirikiano katika kupambana na wanamgambo wa Boko Haram. Buhari alipokelewa na mwenzake wa Cameroon, Paul Biya katika uwanja wa kimataifa wa mji mkuu Yaounde.mbali na mazungumzo yao ya jana, Viongozi hao watakutana na waandishi wa habari leo. Nigeria, Niger, Cameroon na Chad zimeungana katika kuwapiga waasi wa Boko Haram ambao sasa wamekuwa tishio hata...
MAMLAKA ya usafirishaji nchini Ufaransa imesema inachunguza mabaki ya ndege ya yanayodaiwa kupatikana ndani ya Bahari ya Hindi ili kubaini kama ni ya ndege ya Malaysia ya MH370 iliyopotea bila kuwa na taarifa zozote kwa muda mrefu sasa. Taarifa kutoka Marekani zinasema wachunguzi hao ambao wameona picha za mabaki hayo wana uhakika mkubwa kwamba ni ya ndege hiyo ya Malaysia ambapo mabaki hayo ni sehemu ya bawa la ndege. Hata hivyo, Wataalamu wa Ufaransa wanasema ni mapema mno kutoa uhakika...
KIONGOZI wa kundi la wanamgambo la Lashkar-e-Jhangvi linalopinga waislamu wa Kishia, ameuwawa nchini Pakistan katika mapambano na polisi mkoani Punjab. Kwa mujibu wa vyombo vya usalama vya Pakistan, wafuasi wa kundi hilo walivamia gari la polisi lililokuwa limembeba kiongozi huyo, Malik Is-haq, na wanachama wengine 13 wa kundi lake. Lengo la wavamizi hao ilikuwa ni kumkomboa Is-haq....
WATU wawili wanaume wanatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Zimbabwe baadaye leo wakishtakiwa kwa makosa ya uwindaji , baada ya simba maarufu nchini humo kuuawa na mtalii mmoja raia wa Marekani . Simba huyo, anayejulikana kwa jina la Cecil, alipigwa risasi nje kidogo ya mbuga ya wanyama ya taifa ya Hwange na Walter Palmer, daktari wa meno na mtu anayependa uwindaji, ambaye pia anaweza kukabiliwa na mashtaka. Maandamano juu ya kuuawa kwa simba huyo yamefanyika nje ya makaazi ya bwana Palmer katika...
KAMPUNI ya usafiri inayofanya safari zake kati ya Ufaransa na Uingereza ya Eurotunnel imesema maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakijaribu kuingia nchini Uingereza kupitia usafiri huo. Ripoti ya kampuni hiyo imebainisha kuwa idadi ya majaribio ya wahamiaji kutaka kuvuka mpaka kupitia usafiri aina hiyo ya usafiri imeongezeka zaidi, kwani wahamiaji hao wanajificha kwenye magari ya mizigo,kupanda vizuizi. Katika mkutano wa Mawaziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa na Uingereza uliofanyika mjini London,mbinu za pamoja kuweza kudhibiti wahamiaji hao kuvuka...
ASKOFU Desmond Tutu na mshindi wa nishani ya Nobel nchini Afrika Kusini, amerejeshwa tena Hospitali kwa matibabu zaidi. Tutu wiki iliyopita aliruhusiwa kurejea nyumbani baada ya afya yake kuonekana kuimarika ndani ya siku saba za matibabu. Hata hivyo kwa sasa Askofu tutu mwenye umri wa miaka 83 yupo katika uangalizi wa madakatari ambao wanaendelea kutibu maradhi yake....